Mwanafunzi akimbilia TBC; kisa kudaiwa sh 250 tuition na 100 ya uji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanafunzi akimbilia TBC; kisa kudaiwa sh 250 tuition na 100 ya uji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Mar 25, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,654
  Trophy Points: 280
  Kweli sasa nchi inatia aibu sijui ni laana ama shida
  kwa wanaoangalia tbc muda huu mtaona kwa huzuni kubwa
  mwanafunzi mmoja aitwae arafat amekimbilia ofisi za tbc kuomba msaada baada ya kuwa anachapwa kila siku kwa kukosa kuwa na sh 250 za tuition na sh 100 za uji.....mwanafunzi huyo analalamika wamekuwa kama mzigo kwa walimu tangu mwaka jana...akimtaja mwalimu husika arafat anasema mwalimu....amekuwa kila akija darasani anafundisha dk 30 kabla ya kumaliza anaanza kukusanya pesa za uji sh 100 na sh 250 kwa masomo ya ziada....anasema kila anaekosa hela anawekwa pembeni alafu akimaliza kukusanya anaanza kutuchapa ona mama huku kumebadilika hadi rangi tunavyopigwa!!!alisema arafat wa shule ya muungano....

  Tbc ilifika moja kwa moja na kwenda kwa mwalimu mkuu ambae alitaka kujificha kabla ya mwandishi kumwelekea pale alipokuwa akikimbilia...bi fatma alipohojiwa anasema awezi sema ndio au hapana maana anavyojua tuition si lazima na ni baada ya madarasa ya kawaida...alipobanwa zaidi akakiri atalishugulikia
  ila akasema ana uhakika akuna kitu kama hicho ambapo alimpeleka kwa watoto wengine na kukiri akuna kitu hicho...

  Akionekana tena mwandishi wa bbc aliitwa na watoto wengine pembeni na kuambiwa kweli tunapigwa sana bila kutoa sh 250 za tuition na sh 100 za uji tena anakupiga kweli kweli wengine tunakimbia tunarusi nyumbani kesho yake ukitoa akupigi

  jamani mh waziri unalijua kweli???afisa elimu wa wilaya mnawashugulikiaje walimu kama hawa;msije tuundia tume kama dk asha wa temeke watu wakifa na mwisho kukalia matokeo huku wauwaji wakiendelea kuua...kama mnahitaji pesa tunajua mna shida kuna biashara nyingi mmeruhusiwa jamani tengenezeni ice cream,juice karanga wapeni watu wawauzie na si kulazimisha mtoto asome tuition kwako;;huu ni uovu.....

  Shetan umtokew mwalimu huyu mwenye roho ya kifisadi
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,654
  Trophy Points: 280
  Arafat alipoulizwa ameshaenda kwa mwalimu mkuu anasema tumelalalmika sana lakini kila tukipigwa tukimwambia anasema tuwaambie wazazi tumepigwa kesho tuje na hela arafat alisema.....

  Pole sana kijana;wengine tumetoka kimaskin hivyo hivyo bila tuition sababu ya bugudha kama hizo ....
   
 3. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2010
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Hakuna cha Waziri wa Elimu wala nini; Watawala wetu ndo mahali walipotufikisha hapo. Huyo mwanafunzi ameweza kufika TBC sasa wale waliopo kule Buhoro watatoa malalamiko yao kupitia wapi? Labda Redio Burundi maana ndo inapatikana kwa urahisi na ni karibu zaidi kuliko Dar!

  SIku TBC wakifika huko Kasebuzi, Muyovosi, Kaseke, Kalema, Mahurunga na Kyaka ndipo ule msemao Ukishangaa ya Musa utayaona ya Firauni utakapotiamia.
   
 4. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Maskini weee!
   
 5. C

  Chuma JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2010
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kweli kuna kazi ikiwa kila Jambo basi twamtupia Wazir....!!!

  By the way Wahusika ktk Level za Utawala wa ELimu wanapaswa kuchukua Hatua Kali...!!!

  Tunahitaji kuwasaidia Waalim wetu...lkn Pia tunahitaji kuwaamsha Wazazi wetu pia kujua roles zao ktk Jamii...!!!
   
 6. E

  EAGLE Member

  #6
  Mar 26, 2010
  Joined: Oct 17, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa wazazi kama mimi, more is to come. Huu utandawazi sijui niite "media proliferation" nahisi umesababisha walimu (wa msingi na hata sekondari) wawe na tamaa ya maisha ya hali fulani wakati kipato chao ni kidogo. Wanatamani kuwa na flat screen TV, fanicha nzuri nk. Kwa kweli wanastahili (kwani sote tunastahili maisha bora) lakini vipato haviruhusu ghafla bin vup! Now we are headed to a whole new level of child abuse, favouratism (kwa watoto wa vigogo hata at village level) na mbaya zaidi wizi wa mitihani mpaka ya mihula. Hivi vyuo vya ualimu si vinafundisha mambo ya ethics?
   
 7. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Hivi hili swala la kupiga wanafunzi primary school bado lipo? Sheria zetu zinasemake? Je wazazi wanafahamu kwamba watoto wanapigwa kwa kukosa fweza za kulipia? Sasa wakishapigwa wanapewa hiyo elimu?

  Follow the bee here
   
 8. E

  EAGLE Member

  #8
  Mar 26, 2010
  Joined: Oct 17, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wacha
  Kuna directive (mwongozo) wa wizara kuhusu adhabu ya viboko. Hakuna sheria as such. Tofauti na nchi nyingine, kuchapa viboko mwanafunzi siyo kosa bora uwe katika kiwango kilicho amriwa.
   
 9. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #9
  Mar 26, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,579
  Likes Received: 3,881
  Trophy Points: 280
  "HABARI ZA LEO HUMU NI ZA KUHUZUNISHA TU, KUANZIA ASUBUHI AJALI, HII YA HUYU MTOTO"

  God help our country! huyo mtoto akisoma na akaja kupewa ofisi akawa na roho ya kulipiza kisasi kwa kusoma kimaskini, ufisadi utaisha?
   
 10. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,303
  Likes Received: 22,105
  Trophy Points: 280
  Huyo mwalimu anafikiri wanafunzi wana mradi gani wa kuwaingizia fedha?
  Mzazi ndiye aliyeshindwa kulipa hela kwa ajili ya mtoto, iweje adhabu apewe mtoto?
   
 11. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #11
  Mar 26, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  mimi naona adhabu ya viboko iendelee ila kwa kesi kama hii kama ni kweli mwanafunzi kapigwa kwasababu ya pesa ya tution hapo mwalimu ana makosa au pesa ya uji nafikiri alitakiwa aitwe mzazi au wazazi na ndio maana huwa kunakuwa na kamati za shule ambazo mwenyekiti huwa anakuwa mzazi na wajumbe wanachanganyika kati ya waalimu na wazazi so matatizo yote ya wanafunzi yanakuwa solved na hii kamati na kama kuna mchango wa uji au tution hii kamati ya shule ndiyo itakayokubaliana!kama hilo halikupitishwa kwenye kamati ya shule huyu mwalimu ana makosa pili kwanini mwalimu mkuu alipoona kuna tatizo hili alikaa kimyaa?wanajamii kazi ya ualimu kwa tanza nia ni ngumu sana na ni ya lawama sana kutoka serikalini na pamoja kwa wazazi pia na ukiferisha wanafunzi unaonekana hauna maana na tatizo kubwa unaweza kuta darasa moja lina wanafunzi 200 embu nambie bila kiboko hapo pataenda kwasababu kumbuka kati ya hawa wanafunzi kuna kila tabia kutokana na mazingira wanayotoka!ni vigumu sana ndio maana unakuta nguvu lazima itumike mie naunga mkono viboko viwepo ila adhabu itolewe tu pale inapobainika kuna tatizo na kweli linastahili na uchapaji pia uzingatie sheria sio kuua au kusababisha majeraha ni kukumbushana tu jamani nimefanya hii kazi ningumu ati msifikirie kama mnavyoichukulia juu juu jaribuni tu muingie muone!kwasababu kuna wazazi tu unakuta wanashindwa ku control familia zao then mwalimu anapewa darasa lenye wanafunzi 200 afundishe,asahihishe,atunge mtihani,awaandalie uji sidhani serikali kama inatoa hizo fedha za uji kwasababu mwanafunzi hawezi kusoma akiwa na njaa sasa utamsaidieje mtoto kama huyu,bado mwalimu huyohuyo aangalie familia yake na mshahara ndio huo mnaousikia redioni kila siku!mie nadhani ifike mahala serikali isilichukulie mzaha suala la elimu kweli waalimu wanateseka sana!na mbaya zaidi inapotokea mmoja kama huyu akaharibu basi mzigo wote wa lawama ni kwa sekta nzima hawa nao ni binadamu jamani kama sisi!kwa hilo lililotokea nadhani panahitajika kamati ya shule ikae na serikali iangalie pia kwamba huu uji na hii fedha ya uji anayetakiwa kutoa ni nani??na sheria inasema mwanafunzi asiyetoa achapwe viboko au mzazi zitwe na kuulizwa na mzazi akisema hana inakuweje?je mwanafunzi anywe uji kwa fedha waliotoa wazazi wengine??kwakweli jambo hili lina mambo mengi sana ukiliangalia kiundani panahitajika kukaa chini hapo!
   
 12. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #12

 13. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #13
  Mar 26, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Haya mambo ya kufunja sheria za haki za watoto zipo nyingi sana mashuleni. You can imagine kama hapa dar yanaweza kutokea hayo, huko kijijini ambapo walimu wanaonekana kama mungu watu itakuwaje?

  Mnakumbuka kuna case moja ilitokea Iringa mjini miezi ya nyuma, mwalimu wa kiume aliwafua nguo wasichana na kuwapa adhabu ya kuruka kuchura chura??..........insanity ya juu kabisa...akini huyo mwalimu bado yupo na anafundisha..........
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Mar 26, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Nilimuona huyo mtoto na kubakia na masikitiko
  nawahurumia watoto wetu ..wanatakiwa wapewe adhabu wanapokosea lakini hizi adhabu zisivuke mipaka
   
 15. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #15
  Mar 26, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Kinachosikitisha ni kwamba hilo suala la uji wanalazimishwa, kuna shule ya jirani kwangu kila mwanafunzi analazimishwa 200. Kwanza ukiuona ule uji utaogopa, mazingira wanayopikia ni hatarishi kwa afya na wakimaliza kuchemsha wanaweka kwenye ndoo ndogo za plastic ndipo unaingizwa madarasani. Hakuna mesi ya kulia chakula hivyo darasa ni chakari kwa uchafu na inzi. Cha kusikitisha zaidi nilipojaribu kumuuliza mzazi ambaye mtoto wake anasoma pale kama walishirikishwa suala la uji kwa watoto alijibu "Hatujashirikishwa". Nilipojaribu kuchimbua zaidi nikagundua kuwa ule ni mradi wa Mwalimu mkuu. Waalimu wengine pia wana miradi yao pale kama ya chips, mihogo, barafu, vitafunio vingine, ubuyu n.k.

  Chanzo cha yote hayo ni kipato kidogo cha waalimu!! je wafanyeje kupambana na gharama za maisha??? Hili ni tatizo ambalo liko kimamlaka zaidi zinazohusika na serikali kwa ujumla waone ni kwa namna gani wataboresha mishahara ya waalimu. Inanishangaza kuwa wafanyakazi wa serikali wanalipwa extra duty allowance ya sh. 30,000 kwa siku na kwa mwezi not less than 600,000 -900,000 kwa extra duty nje ya mshahara japo ni kidogo, na mikutano na semina, etc. Sasa huyu mwalimu na 120,000 itamfikisha wapi kwa mwezi? Hata kama atalipwa net 300,000 bado kwa mwalimu na hasa kama amepanga ni ndoto kabisa? Je utategemea mwalimu huyu aipe kazi yake kipaumbele wakati anadaiwa kodi ya nyumba, jana hajala, bado ada ya watoto wake na gharama zingine za maisha?

  Ni wakati sasa serikali itizame zile proffession ambazo ziko low paid na ni muhumu basi waone ni namna gani waboreshe mapato yao, mfano, afya, na elimu.
   
 16. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #16
  Mar 26, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Safi sana!

  Lakini kwanini mnadhani alienda kwenye chombo cha habari badala ya chombo cha dola?
  Hii kali, ila nampongeza mtoto kwa kutokaa kimya na kutoa dukuduku lake kwa watanzania wengine wenye mioyo...! iwe fundisho
   
 17. madangwa

  madangwa Member

  #17
  Mar 26, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Tatizo njaa tu. Njaa hizo zipo kila sehemu hata vyuooni ila kwa mtindo mwingine.
   
 18. Mom

  Mom JF-Expert Member

  #18
  Mar 26, 2010
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 708
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kweli walimu wanamaisha magumu, lakini kwa mambo ya pesa haipaswi kumwadhibu mtoto ni bora basi anwite mzazi wake amweleweshe kuhusu mahitaji ya uji na tution. Pse walimu tupende taaluma yetu ni kweli mishara ni midogo saaaaaana, but matendo yanasababisha pia tusithaminike na kupewa heshima tunayostahili
   
 19. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #19
  Mar 26, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Hii ya michango ya tuition na uji mbona yapo tu sehemu nyingi!
   
 20. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #20
  Mar 26, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  100tsh au 250tsh kwa 2010 inakuwa ishu ya kuchapana bakora?
  Ee Mungu uwasamehe kwani hawajui wakitendacho......lol!
   
Loading...