Mwanafunzi Akamatwa na Vocha za Vodacom za Tsh. Mil. 90

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20
Na Chondoma Shdabani, Dar es Salaam

Mwanafunzi anayesoma chuo cha biashara cha CBE jijini Dar es Salaam amekamatwa pamoja na wenzake wawili akijaribu kuziuza vocha za wizi za kampuni ya simu ya Vodacom zenye thamani ya Tsh. Milioni 90.

Akiongea na waandishi wa habari, kamanda wa polisi wa kanda maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema kwamba mwanafunzi huyo wa CBE aliyejulikana kwa jina la Muhsini Amin mwenye umri wa miaka 21 alikamatwa pamoja na watuhumiwa wengine wawili Sadick Jediwa (21) mkazi wa Tandale na Rashidi Maulidi (28) mkazi wa Mwananyamala wakijaribu kuziuza vocha hizo.

Kamanda Kova alisema kwamba watuhumiwa hao walikamatwa kwenye viwanja vya Leaders Club wakijaribu kuziuza vocha hizo za Ths. 10,000 na Tsh. 5,000 zenye thamani ya jumla Tsh. Milioni 90.

Kova aliendelea kusema kuwa watuhumiwa hao walinaswa na polisi kufuatia mtego uliowekwa na polisi baada ya kupewa taarifa.

Kova alisema kwamba polisi aliyejifanya mnunuzi wa vocha hizo alifanikiwa kuafikiana na watuhumiwa hao kuzinunua vocha hizo za Tsh.
Milioni 90 kwa malipo ya nusu ya pesa hizo Tsh. Mil. 45.

Watuhumiwa hao walikamatwa na kushikiliwa na polisi huku polisi ikiendelea na uchunguzi kugundua walizipata vipi vocha nyingi kiasi hicho.

Chanxo cha hao wanafunzi kuzipata Vocha zenye thamani ya pesa hiyo ni kipi??

Lazima baadhi ya wafanyakazi wa Voda watakaokuwa wanafahamu hiyo issue
 
Hapo ni mtandao mrefu ila mshikwa na ngozi ndiye mwizi. Vijana msipende utajiri wa haraka haraka, misheni town zina wenyewe. Oneni sasa mmeanza kuharibu future yenu, maana mpaka kesi imalizike na hatima yake ndivyo hivyo tena sahauni shule!!!

Poleni wazazi, ndugu, jamaa na marafiki.
 
Chanxo cha hao wanafunzi kuzipata Vocha zenye thamani ya pesa hiyo ni kipi??

Lazima baadhi ya wafanyakazi wa Voda watakaokuwa wanafahamu hiyo issue

Mbona unakurupuka!!! Are you a great thinker?? Why are you jumping into weak conclusions??

Kweli watz tuna kazi kubwa ya kujenga taifa la watu wanaojua kufikiri!!
 
[/COLOR]

eeeh nahisi wewe ni mfanyakazi wa hiyo kampuni maana umenichenjia lol
Hivi katika akili za kufikirika hizo Vocha kibao hao wanafunzi wamezitoa wapi.??

Ni kama vile wewe ukaibe bank:Dhuo ni mtazamo na fikira zangu tu
 
1st lady hiyo ni sahihi kabisa jamaa kakurupuka kujibu, kuwa great thinker haimaanishi ufikiri the way mtu mwingine anavyotaka, inawezekana jamaa kahusika maana alivyo mind!
 
[/COLOR]

Mbona unakurupuka!!! Are you a great thinker?? Why are you jumping into weak conclusions??

Kweli watz tuna kazi kubwa ya kujenga taifa la watu wanaojua kufikiri!!

ndugu mbona umekuwa mkali sana, kuwa great thinker hakumnyimi mtu kutoa maoni yake.....kuna uwezekano watu wa voda wakawa wanahusika au ni maagent wao. cha ajabu hapo ninini?amekurupuka nini sasa?
 
Jamani mngekuwa mnajua hizi vocha zinatengenezwa vipi na logistic zake, mngefikiri mara 2x2 kabla ya kufikia conclusions kama hizo!!

Kukurupuka huku ndiko kunakofanya watu smart kama kina Zombe kuwa vinara mwisho wa siku!!!
 
[/COLOR]

Mbona unakurupuka!!! Are you a great thinker?? Why are you jumping into weak conclusions??

Kweli watz tuna kazi kubwa ya kujenga taifa la watu wanaojua kufikiri!!
kesi ngapi za wizi wa bank zimeprove kwamba wahusika wanakuwa watu wa ndani wa bank wafanyakazi au walinzi, sasa hizo vocha za mil 90 , mtu wa nje atazipataje bila ya kuwa na inside info en help?
mtazamo wangu wewe ndo umekurupuka kumchenjia dada hapo juu.na kama kweli great thinker as you claim kubali kushindwa omba msamaha coz umeutukana uwezo wake wa kufikiri.
 
Jamani mngekuwa mnajua hizi vocha zinatengenezwa vipi na logistic zake, mngefikiri mara 2x2 kabla ya kufikia conclusions kama hizo!!

Kukurupuka huku ndiko kunakofanya watu smart kama kina Zombe kuwa vinara mwisho wa siku!!!
kama ndo hivyo usemavyo basi jukumu lako kutueleimisha kwanza jinsi ugumu wa hiyo issue kushirikishwa wafanyakazi wa voda badala ya kushambulia uwezo wa mtu wa kufikiri, kumbuka kila mtu ana field yake kama wewe mtaalam wa IT,haimaanishi unayajua mambo ya sheria au accounts, and viceversa.
 
Hawa vijana walifanya kosa moja kubwa sana. Haya mambo hukurupuki kuuza zote. Unauza kidogo kidogo na hadi unakuja kupata FISADI ndipo unaliuzia zote. Ikibidi unaenda kwa watu kama Mpakanjia na unamuuza kwa hela ndogo na yeye atajua aende wapi kupata hela yake....... Vinginevyo, nenda mikoani.

Rostam Azziz naona alifoka na mambo yakawekwa sawa.....
 
[/COLOR]

Mbona unakurupuka!!! Are you a great thinker?? Why are you jumping into weak conclusions??

Kweli watz tuna kazi kubwa ya kujenga taifa la watu wanaojua kufikiri!!
teh teh jamaa kanikumbusha kisa cha ditto na membe na nyoka wa mdimu pale aliposema simtaji lakini ye anajua na atajitaja mwenyewe.maana hapa mzee tumekushtukia kama uko ndani ya hilo dili nini?haiwezekani kukurupuka tu na maneno makali kama haya
 
[/COLOR]

Mbona unakurupuka!!! Are you a great thinker?? Why are you jumping into weak conclusions??

Kweli watz tuna kazi kubwa ya kujenga taifa la watu wanaojua kufikiri!!
hata ingekua wewe ungefikiri hivyo katika hali ya kwaida kabisa, na wakibanwa utasikia kuwa kuna wafanyakazi wanahusika. Hivi unafikiri hizi deal kubwa nani wanaanzisha kama sio wahusika wa ile sehemu? Mfano tanesco kuiba umeme ili mlipe bili kidogo ni nani kama sio hao wafanyakazi??????????????
 
sisi wananshi wa nje ni ngmu kujua bana kama kuna ishu pale, lazima
 
[/COLOR]

Mbona unakurupuka!!! Are you a great thinker?? Why are you jumping into weak conclusions??

Kweli watz tuna kazi kubwa ya kujenga taifa la watu wanaojua kufikiri!!
hata ingekua wewe ungefikiri hivyo katika hali ya kwaida kabisa, na wakibanwa utasikia kuwa kuna wafanyakazi wanahusika. Hivi unafikiri hizi deal kubwa nani wanaanzisha kama sio wahusika wa ile sehemu? Mfano tanesco kuiba umeme ili mlipe bili kidogo ni nani kama sio hao wafanyakazi??????????????

sisi wananshi wa nje ni ngmu kujua bana kama kuna ishu pale, lazima mnahusika kama nawe ni mfanyakazi hapo
 
ml 90 nyingi sana hata agent wengine hawana mzigo kama huo, lazima watakua voda wenyewe wamefanya mchongo
 
Jamani mngekuwa mnajua hizi vocha zinatengenezwa vipi na logistic zake, mngefikiri mara 2x2 kabla ya kufikia conclusions kama hizo!!

Kukurupuka huku ndiko kunakofanya watu smart kama kina Zombe kuwa vinara mwisho wa siku!!!

Hebu tusaidie hapo kwenye pink mambo yanakuwaje?? Hapa ni sehemu ya kuelimisha.
 
Back
Top Bottom