Mwanafunzi ajiua kwa kujirusha kutoka kwenye ndege ikiwa angani

mwanafunzi+picha.jpg

Madagasca. Mwanafunzi wa Chuo cha Kikuu cha Cambridge, Uingereza, Alana Cutland amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka katika ndege umbali wa futi 5000 angani.

Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 19 inadaiwa alilazimisha kufungua mlango wa ndege hiyo kisha kujirusha katika eneo la Anjajavy.

Polisi nchini Madagasca wamedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa kwa sasa wanaangalia nini kilitokea sekunde chache kabla ya msichana huyo kufa.

Mkuu wa Polisi wa Madagasca, Sinola Nomenjahary alisema kuwa taarifa za awali zinaonyesha kwamba rafiki wa karibu wa msichana huyo, Ruth Johnson na rubani wa ndege hiyo walijaribu kumzuia kwa kumshika mguu kwa sekunde kadhaa bila mafanikio.

“Lakini baada ya sekunde kadhaa Alana alijikwamua na kujirusha chini,” alisisitiza Nomenjahary.

Msichana huyo ambaye alikuwa mwaka wa pili katika masomo ya Biolojia alikuwa akisafiri kwenda nchini India kwa ajili ya safari ya kimasomo ambako inadaiwa walibakiza dk 10 pekee kutua.

Hata hivyo, polisi nchini humo ilisema kuwa wana wasiwasi huenda mwili wa msichana huyo usipatikane kutokana na eneo aliloangukia kutofikika kirahisi.
Private jet au?
Inakuaje rafiki wa karibu asijue sababu?
Rubani alifuata nini mlangoni?
Kwann wamshike mguu mmoja badala ya mwili mzima?
Katika suala la kufa na kupona wa2 wawili watashidwaje na mtu mmoja?

Kwa akili zangu ndogo nafikir Rubani na Rafiki wasukumwe ndani.
 
Inasemekana wakati anajirusha huenda alikuwa katika 'Hallucinations' kutokana na dawa za Malaria alizokuwa akitumia.
 
mwanafunzi+picha.jpg

Madagasca. Mwanafunzi wa Chuo cha Kikuu cha Cambridge, Uingereza, Alana Cutland amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka katika ndege umbali wa futi 5000 angani.

Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 19 inadaiwa alilazimisha kufungua mlango wa ndege hiyo kisha kujirusha katika eneo la Anjajavy.

Polisi nchini Madagasca wamedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa kwa sasa wanaangalia nini kilitokea sekunde chache kabla ya msichana huyo kufa.

Mkuu wa Polisi wa Madagasca, Sinola Nomenjahary alisema kuwa taarifa za awali zinaonyesha kwamba rafiki wa karibu wa msichana huyo, Ruth Johnson na rubani wa ndege hiyo walijaribu kumzuia kwa kumshika mguu kwa sekunde kadhaa bila mafanikio.

“Lakini baada ya sekunde kadhaa Alana alijikwamua na kujirusha chini,” alisisitiza Nomenjahary.

Msichana huyo ambaye alikuwa mwaka wa pili katika masomo ya Biolojia alikuwa akisafiri kwenda nchini India kwa ajili ya safari ya kimasomo ambako inadaiwa walibakiza dk 10 pekee kutua.

Hata hivyo, polisi nchini humo ilisema kuwa wana wasiwasi huenda mwili wa msichana huyo usipatikane kutokana na eneo aliloangukia kutofikika kirahisi.
ckujua kumbe mlango wa ndege mkiwa angani unafungua tu bila shida kama wa hice za mbagala
 
Hata gari dereva unaweza kulock mlango wa abiria usifunguke,sasa hii imekaaje?
 
Uongo huu, alipitia wapi mpaka ajirushe mlangoni ?? dirishani?? hizo sehemu 2 hakuna uwezekano kama ndege ipo hewani
 
Ilikua ni ndege ndogo ya kukodi,
Alishikwa na tatizo la akili akawa na wasi wasi atapelekwa jela kwa kua hakumaliza kazi yake hivyo akapata uamuzi wa kujiua.
 
Back
Top Bottom