Mwanafunzi ajiua kwa kujirusha kutoka kwenye ndege ikiwa angani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,592
2,000
mwanafunzi+picha.jpg

Madagasca. Mwanafunzi wa Chuo cha Kikuu cha Cambridge, Uingereza, Alana Cutland amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka katika ndege umbali wa futi 5000 angani.

Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 19 inadaiwa alilazimisha kufungua mlango wa ndege hiyo kisha kujirusha katika eneo la Anjajavy.

Polisi nchini Madagasca wamedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa kwa sasa wanaangalia nini kilitokea sekunde chache kabla ya msichana huyo kufa.

Mkuu wa Polisi wa Madagasca, Sinola Nomenjahary alisema kuwa taarifa za awali zinaonyesha kwamba rafiki wa karibu wa msichana huyo, Ruth Johnson na rubani wa ndege hiyo walijaribu kumzuia kwa kumshika mguu kwa sekunde kadhaa bila mafanikio.


“Lakini baada ya sekunde kadhaa Alana alijikwamua na kujirusha chini,” alisisitiza Nomenjahary.

Msichana huyo ambaye alikuwa mwaka wa pili katika masomo ya Biolojia alikuwa akisafiri kwenda nchini India kwa ajili ya safari ya kimasomo ambako inadaiwa walibakiza dk 10 pekee kutua.

Hata hivyo, polisi nchini humo ilisema kuwa wana wasiwasi huenda mwili wa msichana huyo usipatikane kutokana na eneo aliloangukia kutofikika kirahisi.
 

Ligogoma

JF-Expert Member
Aug 27, 2010
3,353
2,000
Alifunguaje mlango wa ndege ya abiria?

Nahisi kalikuwa kandege kadogo maana maelezo yanasema rubani na rafiki yake walimzuia kwa kumshika!!

Sijaona muhudumu mahali popote hapo!! Rubani alihama kwenye usukani 🤣🤣🤣
 

Dalmine

JF-Expert Member
Sep 8, 2016
5,066
2,000
Alifunguaje mlango wa ndege ya abiria?

Na mimi hapo ndio nashangaa, coz all passengers wakishaingia ndani ya pipa na milango hufungwa, na haifunguliwi tena mpaka wawasili sehemu husika.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom