Mwanafunzi ajiua baada ya mwalimu kumkejeli kwa kupatwa hedhi akiwa darasani

Jollie

Member
Jul 26, 2019
35
125
Jeshi la Polisi nchini Kenya linaendesha uchunguzi juu ya tukio lililopelekea mwanafunzi wa umri wa miaka 14 kujiua saa kadhaa baada ya nguo zake kuloa damu ya hedhi alipokuwa shule, Ijumaa Septemba 6, 2019.

Mama wa Jackline Chepngeno, Beatrice Chepkurui Koech amesema kuwa mtoto wake alikejeliwa na mwalimu wa kike katika Shule ya Msingi Kabiangek baada ya damu hiyo kuchafua nguo zake akiwa darasani.

“Hakuwa na chochote cha kutumia kuzuia damu hiyo. Wakati damu ilipoloanisha nguo yake, aliamriwa kutoka darasani, asimame nje,” amesema mama huyo.

Kundi la wazazi waliandamana nje ya shule hiyo na kufunga barabara inayoelekea shuleni humo wakishinikiza mwalimu huyo achukuliwe hatua, kabla ya kutawanywa na vyombo vya ulinzi vilivyotumia mabomu ya kutoa machozi.

Baada ya tukio hilo Jackline Chepngeno alirudi nyumbani majira ya saa 4 na 30 asubuhi, ambapo baada ya kuzungumza na mama yake, mzazi huyo alimwambia akachote maji mtoni, ajisafishe, kisha waende wote shule.

Hata hivyo mtoto huyo alitumia mwanya huo alipokwenda mtoni na kujinyonga hadi kufariki dunia.

Mwaka 2017 serikali ya Kenya ilipitisha sheria iliyolenga kutoa taulo za kike bure kwa wanafunzi wote wa shule za msingi wenye uhitaji.

Kwa sasa, kamati ya Bunge ya Kenya inafanya uchunguzi kubaini kwanini mpango huo wa bure ambao unaigharimu serikali takribani TZS 10.4 bilioni kwa mwaka hautekelezwi katika shule zote.
 

Belzera

Senior Member
Feb 22, 2019
143
250
Wote! Mtoa post hakumtakia marehemu rip!Mwalimu kusababisha mwanafunzi kuchukua maamuzi magumu,mwanafunzi kujinyonga kulikoleta simanzi na taharuki kuu,na wewe kuuliza swali la kipuuzi!
Naomba Mungu amsamehe na amlaze mahala pema peponi huyo binti.
Huyo mwalimu hastahili kusimamia watoto kwani anakosa ubinadamu.Na si ajabu hana mtoto kabisa.
Hizi changamoto za watoto wa kike,ni mzigo unaohitaji uelewa,staha na kusaidia sana. Changamoto zingine za mazingira ya mabinti,mtu akizijua kiuhalisia na kiundani,ataelewa watoto wa kike ni wa kuwalinda sana na kuhurumiwa kwa hizi changamoto zao za kimaumbile,licha ya mengine pia.
 

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
21,255
2,000
Huyo mwalimu achukuliwe hatua kali sana, halafu cha kushangaza ni wa kike, pumbavu tu.
RIP mwanafunzi.
 

Nguto

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,127
2,000
Sasa mama naye!!!!! Mtoto yuko stressed kwa tukio lililomtokea wewe unamtuma tena mtoni akachote maji halafu iende naye tena shule kwa mwalimu yule yule ukafanye nini na mtoto? Kesho mtoto anafanyaje anapoenda shule kwa walimu hao hao??? Ndiyo maana alijinyonga. Mama naye alimstress mtoto bila kujua!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom