Mwanafunzi ajifungua katikati ya mtihani!

Masatu

JF-Expert Member
Jan 29, 2007
3,276
125
Mwanafunzi ajifungua katikati ya mitihani


*Apumzika siku moja na kurejea darasani

Na Patrick Mabula, Shinyanga


MWANAFUNZI wa Sekondari ya Mhongoro wilayani hapa, amejifungua huku akiwa anafanya mitihani ya Taifa ya kidato cha nne na kuruhusiwa kuendelea baada ya siku moja.

Mwanafunzi huyo, Felista Musa (17), alijifungua mtoto wa kike Oktoba 17 mwaka huu, katika hospitali ya Wilaya ya Kahama, akiwa katika mtihani na baadaye kuruhusiwa na Mwalimu Mkuu na wasimamizi kuendelea na mitihani.

Habari zilizopatikana shuleni hapo jana zilieleza kuwa Felista alikuwa alipewa ujauzito huo na mwanafunzi anayesoma katika Sekondari ya Muslim ya mjini hapa.

Kutokana na mimba hiyo na kuwa na tumbo kubwa, inadaiwa wazazi wake walikuwa wakifanya jitihada za kwenda kwa waganga wa jadi kwa imani kuwa amerogwa.

Ndugu wa karibu wa familia hiyo ambaye hakupenda jina lake litajwe, alidai kuwa mimba ya binti hiyo ilisababisha wazazi wake wampeleke hadi kwa wachungaji wamwombee kwa imani kuwa ukubwa wa tumbo hilo ulitokana na sababu za kishirikina.

Alidai kuwa baada ya kufika kwa wachungaji, jitihada hizo hazikufanikiwa baada ya ushauri na kuwaeleza wazazi wampeleke mtoto wao kwa wataalamu hospitalini kwani huenda ni ujauzito.

Wazazi hao wakiwa wamekosa imani na kauli ya wachungaji, walimpeleka hospitali ya wilaya ya Kahama na alipofanyiwa uchunguzi, ilibainika kuwa alikuwa na ujauzito na alijifungua siku moja, baada ya kufikishwa hapo, wakati akiendelea na mitihani.

Mwanafunzi huyo alijifungua Oktoba 17 mwaka huu na kupumzika siku moja na Oktoba 19 akaruhusiwa kuendelea na mitihani.

Waandishi wa habari walipotembelea shule hiyo ya Mhongolo ili kupata ukweli zaidi juu ya tukio hilo, Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo, Bw. Jeremia Gunda, alikataa kuzungumzia suala hilo.

“Mimi sitaki kuzungumzia suala hilo ninyi si mmezoea kupata taarifa za shule hii kutoka kwa Mkuu wa Wilaya, basi nendeni kwa Mkuu huyo,'' alisema Mkuu wa Shule.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Bw. Christopher Jakoracha, alipoulizwa alikiri kujifungua kwa mwanafunzi huyo katika hospitali hiyo na kusema walimpa ruhusa baada ya kujifungua, kutokana na kutokuwa na matatizo yoyote.

Shule ya Sekondari ya Mhongolo ambayo ni ya binafsi, hivi karibuni, ilikuwa imefungwa kwa mwezi mmoja, baada wanafunzi wake wapatao 80 kulazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama, baada ya kula chakula kilichodhaniwa kuwa kibovu.

My Take

Makubwa haya!
 
Mie naona ni hatua nzuri kama karuhusiwa kufanya mtihani.......maana nakumbuka zamani mtoto wa shule akipata mimba anafukuzwa shule.!!Sina maana kuwa kupata mimba @ 17 ni sawa, la bali hilo ni tatizo lingine na ufumbuzi wake ni mwingine.
 
Back
Top Bottom