OgwaluMapesa
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 10,942
- 428
Leo Majira ya saa moja na dakika 45 Asubuhi nikiwa nimepanda daladala pale kituo cha moroco kwenda kawe kwa bahati mbaya sikupata siti mpaka kwa Mwalimu, lakini tangu napanda kulikuwa na mwanafunzi wa kike ameketi katika siti amefunga hijabu lakini alikuwa anaonekana amesinzia ikafika njia panda ya coca colla konda akawa anakusanya nauli kufika kwa yule mwanafunzi akamuamsha lakini Binti alikuwa harespond chochote konda akajua ni usanii labda hataki kulipa nauli akamtikisa wapi!!... Ndipo watu wakaanza kumsaidia Kumuamsha, Lakini kumuangalia mapigo alikuwa kimya ,ndipo watu wazima walipomcheki na kugundua ameshafariki Imenisikitisha sana maana kabinti kamefia usingizini wakat mjada wa Budget wizara ya Afya ukiwa unaendelea dodoma