BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,832
- 287,782
Mwanafunzi afariki katika ghasia Chuo Kikuu
Mwandishi wetu
Daily News; Sunday,February 24, 2008 @00:02
FAMILIA ya Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandala, juzi usiku ilinusurika wakati wanafunzi wa chuo hicho, sehemu ya Mlimani, kuvamia nyumbani kwake wakishinikiza wapatiwe huduma ya maji.
Wanafunzi hao walifanya fujo katika maeneo mbalimbali ya chuo na mmoja kuzama katika bwawa la kuogelea chuoni hapo na kufariki dunia saa 4.30 usiku wakati akipata tiba katika hospitali ya chuo hicho.
Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala, aliieleza HabariLeo Jumapili kuwa aliyefariki ni Deogratius Dominick aliyekuwa akisoma mwaka wa kwanza chuoni hapo.
Profesa Mukandala alisema jana jioni kuwa wanafunzi hao waliingia kuogelea baada ya kufanya vurugu katika maeneo mbalimbali ya chuo, ikiwa ni pamoja na kuvamia makazi yake, kuwashambulia wahadhiri na watu wengine katika eneo la UDASA.
Wakati makazi ya Profesa Mukandala yakishambuliwa alikuwa Zanzibar, hivyo endapo wanafunzi wangefanikiwa kuingia ndani ya nyumba anayoishi wangemkuta mkewe na watoto wake wawili.
Kwa mujibu wa Profesa Mukandala, kabla ya kuivamia familia yake na kuvunja geti la nyumba ya mlinzi, wanafunzi hao walikutana katika eneo la Hall 2 saa nne kasorobo usiku, baadaye walikwenda katika eneo la ofisi za utawala wakakubaliana kuwa wakamvamie.
Alieleza kusikitishwa pia na kitendo cha wanafunzi hao kuwavamia wahadhiri na watu wengine, wakiwamo wanafunzi wa kike Hall 3, kuharibu ofisi katika jengo la Hall 4, kuharibu milango 21 na mali nyingine.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Liberatus Barlow, jana aliwaeleza waandishi wa habari kuwa mwanafunzi aliyefariki dunia alijirusha katika bwawa, lakini haikufahamika endapo alikuwa na lengo la kuogelea au kufanya uharibifu wa miundombinu ya bwawa hilo.
Kwa mujibu wa Kamanda Barlow, wanafunzi hao walikwenda katika eneo hilo baada ya kufanya vurugu nyumbani kwa Profesa Mukandala, UDASA, nyumbani kwa Meneja makazi wa chuo hicho na katika makazi ya wanafunzi.
Vurugu hizi chanzo chake ni kukatika huduma ya maji katika eneo la Chuo Kikuu. Uchunguzi umeonyesha kuwa maji hayo yalikatwa kutokana na ukarabati unaofanyika Lower Ruvu, alisema.
Aliwaeleza waandishi wa habari kuwa, wanafunzi hao waliharibu magari mawili kwa kuyavunja vioo, likiwamo aina ya Corolla Limited lenye namba za usajili T 824 ABL lililovunjwa kioo cha nyuma.
Kwa mujibu wa Barlow, wanafunzi walifanya vurugu UDASA kwa takribani saa moja na nusu, baadaye walivamia nyumba ya Meneja Makazi wa Chuo wakavunja vioo vya madirisha 13.
Kwa mujibu wa polisi, walipotoka hapo walikwenda katika jengo liitwalo Hall 7 wakawalazimisha wenzao waungane nao kwenye vurugu hizo, milango 15 ikaharibiwa kidogo. Pia vurugu hizo zilienea katika eneo la Hall 2 na 1.
Hata hivyo, maeneo hayo mawili hayakupata madhara, alisema Barlow na kubainisha kuwa walipotoka hapo walikwenda katika bwawa la kuogelea wakavunja geti la kuingilia katika eneo hilo.
Wanafunzi wanadai vurugu hizo zilichochewa na kukatwa huduma ya maji, hata hivyo ni mapema mno kutamka kwamba kilichopelekea kutokea kwa vurugu hizo ni tatizo hilo, alisema. Alisema, uongozi wa Chu,o sehemu ya Mlimani, ulitoa huduma kwa kuweka maboza ya maji na kwamba haikuwa mara ya kwanza maji kukatika katika eneo hilo.