Mwanafunzi afa kwa kupigwa na radi porini alikokuwa amejificha

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi Swaila, kata ya Mkwamba wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Maria Pangani (14) amekufa papo hapo baada ya kupigwa radi.

Mwanafunzi huyo aliyekuwa akisoma kupitia Mpango wa Memkwa, alipigwa na radi akiwa amejificha porini baada ya mama yake kumtishia kuwa atafikishwa katika Serikali ya kijiji hicho baada kugundua kuwa alikuwa akiimiliki kwa siri simu ya kiganjani bila kufahamika aliyemnunulia.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwarunda alithibitisha tukio hilo na kueleza kuwa lilitokea Machi 22 , saa 11:00 jioni katika kijiji cha Swaila wilayani Nkasi.

Akizungumzia mkasa huo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Swaila, Juvenary Mmanzi alisema, mama mzazi wa mtoto huyo alishangaa kuona binti yake akiwa na simu.

“ Ndipo mama yake alipomhoji alikoipata simu hiyo, binti alikataa kumtaja mtu aliyemnunulia ndipo mama yake alipohamaki na kumtishia kuwa atampeleka katika Serikali ya Kijiji afungwe asipomtaja mtu aliyemnunulia simu hiyo “ alieleza Mmanzi.

Kwa mujibu wa Mmanzi, mtoto huyo alijawa na hofu kubwa ya kufungwa jela akakimbilia porini kujificha na ghafla mvua ilianza kunyesha na ndipo alipigwa na radi.

Inadaiwa kuwa, wakazi wa kijiji hicho walifika kwenye pori hilo na kukuta mwili wa marehemu ukiwa umeunguzwa.

Simu na matunda aina ya mapera vilikutwa kwenye mfuko wa sketi aliyokuwa ameivaa.

Kwa mujibu wa Mwaruanda, uchunguzi wa kitabibu umeonesha kuwa kifo cha mtoto huyo kimesababishwa na radi iliyompiga, mwili wake ulikabidhiwa kwa wazazi wake kwa maandalizi ya maziko.

Chanzo: Habari Leo
 
Mkoa wa Rukwa, Kigoma, na Iringa hususani kule Mafinga ni maeneo yenye radi sana, ivi nini kinapelekea kuwa na radi nyingi kule.
 
Mkoa wa Rukwa, Kigoma, na Iringa hususani kule Mafinga ni maeneo yenye radi sana, ivi nini kinapelekea kuwa na radi nyingi kule.
Rukwa inaongoza, nilikuwa pale kwa muda, wenyeji wanakuambia rad ya kichawi, radi inaweza piga masaa 6 mfululizo,
 
Hata mkoa wa Kagera kuna radi sana, na mwaka jana imeua watu kibao pamoja na mifugo.
 
Ukiona radi usikae chin ya mti au maji.zima simu yako au gari
 
Kweli mkuu kuna siku nilikua kibaha, usiku ikanyesha mvua kubwa yenye radi kali, niliona kila radi kali ikpiga gari inawaka hazadi.
 
Kweli mkuu kuna siku nilikua kibaha, usiku ikanyesha mvua kubwa yenye radi kali, niliona kila radi kali ikpiga gari inawaka hazadi.
Siku nyingine zima gari na radio ya gari.. maana zile radio waves ni non ionizing kama electromagnetic waves za simu.
 
kwenye Nchi zilizoendelea wanaweka minara mirefu juu ya magorofa kwa ajili ya kupoteza nguvu ya radi ili isidhuru ivi hatuwezi kuweka na huku kwetu iyo minara ikasaidia kupunguza madhara ya radi..naomba ufafanuzi wa kitaalamu kuhusu ile minara..
 
Mkoa wa Rukwa, Kigoma, na Iringa hususani kule Mafinga ni maeneo yenye radi sana, ivi nini kinapelekea kuwa na radi nyingi kule.
Kiukweli haya maeneo huwezi kumaliza msimu wa mvua bila majanga ya Radi
 
H
kwenye Nchi zilizoendelea wanaweka minara mirefu juu ya magorofa kwa ajili ya kupoteza nguvu ya radi ili isidhuru ivi hatuwezi kuweka na huku kwetu iyo minara ikasaidia kupunguza madhara ya radi..naomba ufafanuzi wa kitaalamu kuhusu ile minara..
Hata hapa kwetu inawezekana juu ya mnala au nguzo, hufungwa mercury, na waya ule wa S. Eneo lilliwekewa hivyo radi haina madhara. Hata hapa baadhi ya maeneo hufungwa mfano baadhi ya majumba misikiti, makanisa, maofisi na huko jeshini sehemu za kutunzia miripuko. Hata hivyo kwenye taarifa ya habari saa mbili usiku, nimeona huko Sumbawanga watoto wanne wametangazwa kufa, baada ya kupigwa na radi wakiwa shuleni. Katika tukio hilo wapo waliojeruhiwa na wammelazwa hospiali, nadhani ni matukio tofauti haya.
 
Bila shaka mvua ilipoanza kunyesha alikwenda kujificha chini ya mti mkubwa!

Na bora ubaki kwenye mvua kuliko kwenda chini ya miti mikubwa kwa sababu kuna mvutano mikubwa kati ya miti mirefu na radi

RIP Maria
 
kwenye Nchi zilizoendelea wanaweka minara mirefu juu ya magorofa kwa ajili ya kupoteza nguvu ya radi ili isidhuru ivi hatuwezi kuweka na huku kwetu iyo minara ikasaidia kupunguza madhara ya radi..naomba ufafanuzi wa kitaalamu kuhusu ile minara..
Zile ni Lighting arrestors mkuu zina act kama earthing Hatuwezi kuziweka tu sehemu ambapo hakuna kitu cha muhimu but ktk majengo marefu na minara zipo kwa ajili ya kuchukua umeme wa radi na kuuzika ardhini kabla haujadhuru jengo au Mnara Sasa nini kifanyike radi inapoanza kumbuka radi si uchawi ni mtengano wa charges huko angani ambapo negative na positive zina seperate na kama tujuavyo unlike charges zinavutana sasa huo mvutano huleta radi ikiwa ni thunder mngurumo na lightning ule mwangaza ardhi kuna wakati ina act kama positive charge ivo anga linakuwa negative ambapo vikivutana hupelekea madhara hayo kufika kabisa ground, kama radi ni umeme basi tuepuke kuwa karibu na conductivity materials wakati inatokea mfano miti au tuzime vifaa vyetu vinavyo radiate Em waves ili kujiweka salama zaidi zima simu,Radio na Tv kama ni Tv weka movies au zima kabisa system ya umeme kuepusha umeme wa Tanesco kuingiliana na wa radi japo tanesco now wanalinda line zao na arrestors
 
Ni bora angemtaja huyo anayemgegeda na kumuhonga simu ili atumbuliwe jipu,

Lala panapostahili binti
 
Back
Top Bottom