Mwanae Benazir Bhutto kurithi kiti alichoacha Mama?

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,398
Kuna patashika katika kurithi kiti cha uongozi wa chama cha PPP.

Mwanae marehemu Benazir aitwae Bilawal Bhutto na mpwa wake aitwae Fatima Bhutto, wote wanafikiriwa kuongoza chama hicho ambacho kiliundwa na marehemu mama yao ambapo baba yao atakuwa ni mlezi wao.

Bilawal mwenye umri wa miaka 19 anasoma chuo kikuu cha Oxford nchi UK akisomea shahada ya siasa na Fatima mwenye umri wa miaka 25, anasomea shahada ya pia ya siasa katika chuo kikuu cha SOAS ambacho ni sehemu ya chuo kikuu cha London.

Bilawal ana mkanda mweusi katika masuala ya mchezo wa kujihami uitwao Taekwondo na anapenda kuwinda ndege wakati akiwa mapumzikoni.

Vyuo vya Oxford na SOAS au (School of Oriental and African Studies) ni baadhi ya vyuo maarufu ambavyo vinapika baadhi ya watu ambao wanakuja kuwa viongozi katika sehemu mbalimbali duniani pamoja na vyuo kama Cambridge na LSE cha London ambacho pia raisi anaeshindwa uchaguzi nchini Kenya bwana Mwai Kibaki amesoma hapo.

Sasa napenda kuuliza swali Je, ni sahihi kuwa na viongozi ambao wamesomea nje ya nchi na kuishi huko iwe UK au USA na kuwa na nyumba huko na pia kuwa na maisha nusu nje na nusu ndani yaani kwa mfano Uk na Pakistani au kwingine?

Nauliza swali hili kwa sababu sijaona hata kiongozi mmoja ambae ameleta maendeleo ya kweli anaporudi nyumbani kwake.

Hongera Raila Odinga! na huu ndio uwe mwamko wa siasa kwa watanzania ambao bado tumelala usingizi mzito.
 
huo ni ujinga...kwa hiyo siasa pakistan lazma iwe ya kwenye chama chao tuuuu??wakafie mbaliii hamna wengine?
 
Benazir Bhutto alikuwa anataka kurudisha demokrasi ndani ya Pakistan. Kufanya hivyo inabidi demokrasi ianzie ndani ya PPP na ingekuwa vizuri kama kungefanyika uchaguzi na nadhani kijana huyu ambaye ana umri wa miaka 19 angeshinda kwa asilimia nyingi tu. Kwa maoni yangu wanampa mzigo mkubwa huyu kijana. Babu yake mzaa mama alikufa kwa siasa, Mama yake naye ndiye huyo kauawa juzi na huyu naye anaingia kwenye siasa wakati kuna machafuko makubwa ndani ya Pakistan lolote linaweza kutokea.
 
Washampa kiti cha mama tayari.....Source-BBC.COM

Bhutto's son named as successor

Bilawal says his father will run the party while he is away
Benazir Bhutto's 19-year-old son Bilawal has been chosen to take over her Pakistan People's Party, after her assassination on Thursday.He will become president in a ceremonial capacity while he finishes his studies at Oxford University.

Bilawal told journalists at the Bhutto family home: "My mother always said democracy is the best revenge". Ms Bhutto's widower, Asif Ali Zardari, who will run the party day-to-day, said it would contest January elections.And he appealed to the former prime minister Nawaz Sharif - a long-time Bhutto rival - to drop his threat to boycott the polls.

Mr Zardari and his son were speaking at a news conference after a meeting of the PPP leadership in Naudero, near Larkana in southern Pakistan.Asif Ali Zardari,Benazir's widower and former political ally, has faced corruption and other charges
Another senior party official, vice-chairman Makhdoom Amin Fahim, said Ms Bhutto had named Mr Zardari as her successor as party chairman.But he said Mr Zardari had turned it down in favour of his son - a decision he said the party leadership had endorsed. Mr Zardari also announced that the couple's children would now change their names and be called Bhutto Zardari.

Sitting between his father and Mr Fahim, Bilawal himself said his father would run the party while he was away at university.
"When I return, I promise to lead the party as my mother wanted me to," he said. But Mr Zardari blocked any further reporters' questions to Bilawal, saying that although party chairman, he was still of "tender age"."We are all in mourning," he said.
Mr Zardari also said he had refused to allow an autopsy on Ms Bhutto's body. "I've lived here long enough to know how and where an autopsy would have been conducted," he said. Instead, he said the party was asking the United Nations and the British government to conduct an investigation similar to the one carried out after the killing of the former Lebanese Prime Minister Rafik Hariri. And he appealed for an end to the unrest in Pakistan, which has killed at least 38 people since Ms Bhutto's killing.
 
yah ni kweli wamempa huyo mtoto wa miaka 19 uenyekiti wa chama hicho cha mama yake...its kind of funny mie nilijua kidooogo family ilitaka irudi in power for the sake ya demokrasia...lakini now nimeona kuwa therez something else beyond their mawazo in they are using mijihela kuwin hata hao PPP wenyewe as now mtoto uko oxford uk anasoma huku analead lichama yeye na baba yake aka mme wa benaziri ndio co mwenyekiti!!!sasa naona yaelekea kuwa kampuni flani
 
au labda kuna mijihela waliiacha wakati ule walipotimuliwa tena kwa kashfa za rushwa now the only way ya kuzipata lazma mrudie post ile!!!
pia it is possible its kind of a movie sasa part 1 ikawa kwa babu yake kijana,part 2 ndio kwa mazake juzi hapo now part 3 which is still sokoni kutengenezwa ndio itakua ya huyu kijana!!

can u immagine leo CCM iongozwe na kijana wa miaka 19 aliyeko chuo kikuu??hata viziwi watasikiza bongo fleva
 
Hawajifunzi tu? Familia ya Gandhi huko India imeandamwa na mauaji kutokana na hayahaya mambo ya kurithishana madaraka kifamilia. Ni ufalme huu? Hivi hawa wana nini? Wafanye tu uchaguzi, na ikiwa huyo mtoto akigombea na kushinda, sawa! Huyo Bhutto familia yake imeandamwa kuanzia mzee wake Zulfikar Alli Bhutto aliyenyongwa na Gen Mohamed Zia ul-Haq, na sasa bi Benazir kauawa, wanamwingiza kijana wa miaka 19 kwenye mgogoro bure tu. Wangemwacha amalize shule, arudi aingie mwenyewe kwa utashi wake.

Duru mbalimbali zinaeleza kuwa lengo la Benazir kurudi kugombea uongozi si sana kurudisha demokrasia kama wengi wanavyodai, bali ni kujilinda dhidi ya tuhuma nyingi zinazomkabili. Kwa kuwa Musharraf naye ni fisadi, wakaingia deal kwamba arudi kugombea lakini afutiwe kesi zote za rushwa alizoshitakiwa, na kweli Musharraf akafuta zile kesi. Ajabu ni kwamba nchi takriban 5 za Ulaya zilikuwa na ushahidi dhidi ya familia ya Benazir Bhutto na mumewe Asif Zardari. Ingekuwa ni serikali tu inayomshitaki, tungesema anabambikiwa kesi, lakini anazo kesi nyingine nyingi Ulaya, na mojawapo Bw Zardari alifungwa kifungo cha nje na account yake kuwa frozen. Na siku chache kabla ya kurudi Pakistan kulikuwa na "red alert" ya Interpol ya kutaka Benazir na mumewe wakamatwe. Lakini katika deal yake na Musharraf (ambaye naye ana mengi angependa kuyaficha kifisadi), wakakubaliana kesi zifutwe na akaunti zake nje ziachiwe atoe hela yake atumie. Na aliye-broker hiyo deal ni mwingereza, ambaye yeye na binamu yake Marekani wote wanamtumia sana Musharraf katika vita yao Afghanistan, na kwa sababu fulani za kifisadi wanawahitaji wote wawili (Bhutto na Musharraf) wawe upande wao, na wanaona wanawafaa. Kwa hiyo kwa vyovyote, yeyote ambaye angeshinda katika uchaguzi huu licha ya mizengwe iliyokuwa ikionekana, bado hawa wawili wangekuwa kwenye utawala kwa mechanism fulani ambayo ilishaandaliwa na mafisadi wenzao waingereza.

Nani kamuua Bhutto? Duru zinaonesha nadharia mbili, circles za Musharraf's intelligence units na wale wanaoitwa Islamist extremists (lakini sio al-Qaeda, maana wale huwa hawakawii kuchukua credit yao wanapofanyiza, wangeshatangaza tangu siku ya kwanza). Musharraf anaiona hiyo rivalry na anaogopa kugeukwa licha ya makubaliano waliyowekeana. Kumbuka Zulfikar Bhutto ndiye aliyemteua Gen Mohamed Zia ul-Haq kuwa mkuu wa majeshi kwa kuwaruka majenerali wengine 5 waliokuwa senior zaidi yake, ili amlindie maslahi yake, lakini mwaka uliofuata tu akampindua na kumnyonga! Na Musharraf alimgeuka Nawaz Shariff, na kumshitaki kwa ulawiti (ambako pia alifungwa) ili kumharibia kabisa asirudi. Kwa hiyo tabia ya kugeukana Musharraf aliijua, ndiposa akawa hana imani sana na huyu Bhutto. Kuhusu hawa Islamists wanaotajwa, ni wale wanaosupport Taliban kule Afghanistan, na base yao kubwa iko mpakani mwa nchi hizo. Tatizo hapo sio dini kwani Pakistan kikatiba ni nchi ya kiislamu, ambayo kwenye katiba wameweka wazi kabisa definition ya muislamu kuwa ni mtu anayekiri "kalimah" (lailailallahu Muhammad Rasulullahu), na kusisitiza "finality of Muhammad's prophecy", kwa kutaja wazi kuwa Ahmadiyya, kwa definition hiyo, sio waislamu. Taliban hawapingi hilo. Tatizo liko kwenye kuunga mkono wamarekani. Huyu Bhutto ndiye aliyeanza kuwasapoti Taliban wakati wa utawala wake, na ndiye aliyekuwa akiwanunulia silaha na ndiye pekee aliyeanzisha ubalozi pekee wa Taliban duniani ambao ulikuwa Pakistan. Lakini alivyorudi mara hii, akiwa na pesa za wamarekani na waingereza, akarudi na ajenda ya kupambana nao. Sasa hapo pakawa pagumu. Japo hata Musharraf anadai anapambana nao, bado kuna uhusiano wa ki-intelijensia kati ya shirika lake la ISI na hao jamaa wa Taliban, anafanya nao kazi kisiri. Na kuna wanaodai kwamba yule muuaji alipata support kubwa sana kutoka vyombo vya serikali kutimiza azma yake, maana yake walifanya hiyo dili pamoja. Kwa hiyo Musharraf hapo "amemgeuka" mwenzie. Alijaribu "kumkanya" kuwa asirudi Pakistan, ati akirudi extremists watamuua kwa suicide bombing, akadai anamwonya hayo kwa faida yake! Benazir akakaidi, akasema atarudi liwalo na liwe! Na likawa! Mshangao wa yeyote ni kuwa inakuwaje rais wa nchi awe ndie medium ya kupitishia vitisho vya watu anaowaita terrorists kama yeye si mmoja wao? Kama ana taarifa hizo, kwa nini asiwazuie kutimiza azma hiyo?

Siasa za Pakistan kwa ujumla ni ngumu, zina mambo mengi sana ya kibabe na ya kimafia, na kila aliyeko kwenye utawala ni paranoid opportunist.

Hadi General Mohamed Zia ul-Haq anafariki kwenye plane crash mwaka 1988, miaka 11 tangu aingie madarakani kwa mapinduzi, bado alikuwa anaahidi uchaguzi and hand over to civilian authority in the next 90 days! Aliingia na ahadi hiyo, akawa anaiahirisha kwa miaka 11, akafa nayo bila kuitimiza! Na ya Musharraf ni hayohayo!
 
Hapa ndipo Siasa za Pakistan zinaposhangaza...Let us forget this Bhutto story..as long as USA wanakutaka na hakuna the so called DEMOCRASY...CCM itaendelea kushinda hadi hapo USA itakaposema achieni Madaraka...Msiwafanye wa TZ woote wajinga hawajui mbivu na mbichi...
 
Now see it is like a family enterprise. For sure as i know Pakistanis, still they will be loyal to him, no democracy inside the party how can you build democracy for the country or mostly likely she was not trusting any body only her husband.
 
the funniest thing is leo nilikua naangalia channel za huku huku zashow kabsa jamaa akiwa nyuma ya gari aki mshoot mama Benazir..na kisha jilipua...lakini bado serikali ya musharaf yapiga kuwa hakuna risasi iliyompata mama huyo bali alikufa kwa ajili ya shockwave which resulted from the bomb akagonga kichwa kwenye kitu cha roof ya juu!which was alaso proven to be wrong and a lie ya serikali....

pia wamelalamikiwa as to kwanini soon after tukio the place was cleaned as in kusafishwa hadi kwa maji kabsaaa ni ili kupoteza ushahidi??

sasa swali langu labda nisaidiwe ubongo wangu kufikira ni why serikali hiyo yapinga kuuwawa kwa risasi kwa mama huyoo?na kushikilia kauwawa kwa bomu na kujigonga kwake kwenye gari?
 
sasa swali langu labda nisaidiwe ubongo wangu kufikira ni why serikali hiyo yapinga kuuwawa kwa risasi kwa mama huyoo?na kushikilia kauwawa kwa bomu na kujigonga kwake kwenye gari?[/
QUOTE]

Jibu lake ukisoma kwenye post niliyoweka hapo juu utaliona. Kifupi ni kwamba serikali na hao wauaji wameshirikiana, kwa hiyo lazima wavuruge taarifa hizo ili iwe vigumu kuwafuatilia. Hebu shangaa, risasi zilizotumika kwenye tukio zimeokotwa na kuhifadhiwa na wananchi wa kawaida, si polisi! Risasi, sizungumzii maganda, zile risasi zilizodondoka baada ya kupiga ile gari! Polisi walipofika, badala ya kuzingira crime scene na kuchukua materials za evidence, waliharakisha kufagia na kuosha kabisa na maji kila kitu ili yeyote asipige picha au asipate kitu cha ku-incriminate serikali. Hawa walikuwa wamejiandaa kabisa na tukio hilo! Madaktari waliomhudumia hospitali ambako alifia kwenye meza ya upasuaji walithibistisha tundu la risasi iliyoingilia shingoni kwa nyuma na kutokea mbele kwenye taya, na wanasema hii ilivunja uti wa mgongo sehemu ya shingoni. Risasi nyingine iliingilia mgongoni na kutokea kifuani, lakini wanadai iliyomuua ni ile ya shingoni. Wale waliokuwa naye kwenye gari, hasa yule aliyemwangukia baada ya kupigwa risasi walithibitisha hayohayo na wameshayasema hata kwenye TV. Sasa madaktari wa serikali walipokuja kuandika ripoti ya kifo (hata Tz katika kesi za mauaji au ajali ni daktari wa serikali pekee ndiye anayeruhusiwa kuandika ripoti ya kifo), wakabadili! Mazingira yote yako wazi wala hayahitaji mjadala mrefu.
 
A very interesting thread, back then nilipokuwa naandika thesis yangu ya PhD. Nilipata exposure ya mambo mengi na ninayatumia sana kama reference kwenye vipindi vyangu kwa wale wanaobahatika kuwa kwenye darasa langu. Anthropology haichoshi, hasa hasa political anthropology, maana hii ndiyo base inayoweza kuelezea history, yaani behind the events.
 
A very interesting thread, back then nilipokuwa naandika thesis yangu ya PhD. Nilipata exposure ya mambo mengi na ninayatumia sana kama reference kwenye vipindi vyangu kwa wale wanaobahatika kuwa kwenye darasa langu. Anthropology haichoshi, hasa hasa political anthropology, maana hii ndiyo base inayoweza kuelezea history, yaani behind the events.
jesus christ of Nazareth!na wewe una Phd,kwa uandishi wa hovyo namna hii?
 
Back
Top Bottom