Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,340
- 21,719
Kuna patashika katika kurithi kiti cha uongozi wa chama cha PPP.
Mwanae marehemu Benazir aitwae Bilawal Bhutto na mpwa wake aitwae Fatima Bhutto, wote wanafikiriwa kuongoza chama hicho ambacho kiliundwa na marehemu mama yao ambapo baba yao atakuwa ni mlezi wao.
Bilawal mwenye umri wa miaka 19 anasoma chuo kikuu cha Oxford nchi UK akisomea shahada ya siasa na Fatima mwenye umri wa miaka 25, anasomea shahada ya pia ya siasa katika chuo kikuu cha SOAS ambacho ni sehemu ya chuo kikuu cha London.
Bilawal ana mkanda mweusi katika masuala ya mchezo wa kujihami uitwao Taekwondo na anapenda kuwinda ndege wakati akiwa mapumzikoni.
Vyuo vya Oxford na SOAS au (School of Oriental and African Studies) ni baadhi ya vyuo maarufu ambavyo vinapika baadhi ya watu ambao wanakuja kuwa viongozi katika sehemu mbalimbali duniani pamoja na vyuo kama Cambridge na LSE cha London ambacho pia raisi anaeshindwa uchaguzi nchini Kenya bwana Mwai Kibaki amesoma hapo.
Sasa napenda kuuliza swali Je, ni sahihi kuwa na viongozi ambao wamesomea nje ya nchi na kuishi huko iwe UK au USA na kuwa na nyumba huko na pia kuwa na maisha nusu nje na nusu ndani yaani kwa mfano Uk na Pakistani au kwingine?
Nauliza swali hili kwa sababu sijaona hata kiongozi mmoja ambae ameleta maendeleo ya kweli anaporudi nyumbani kwake.
Hongera Raila Odinga! na huu ndio uwe mwamko wa siasa kwa watanzania ambao bado tumelala usingizi mzito.