Mwanadada una-date na mume wa mtu ukitegemea akuoe, hiyo haipo kabisa

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
13,216
2,000
Mwanadada una-date na mume wa mtu ukitegemea akuoe, hiyo haipo kabisa. Kama umeangukia kwenye hayo mahusiano, jua kinachowaunganisha ni kulana kimasihara tu. Ni vigumu kwa mwanaume mwelewa aliyesota na mkewe kupigania maisha yao kiuchumi n.k, leo hii amuache aje akuoe wewe.

Hata kama ikatokea umezaa naye, jua huyo mtoto ni wa kwako, pambana uwezavyo uweze kumuhudumia na sio kumshurutisha mume wa mtu uliyezaa naye atoe majukumu. Wakati uko naye hukujua ni mume wa mtu? na mpaka ukazaa naye ulikuwa unategemea nini?

Elewa ukiwa na mahusiano na mume wa mtu, pale ni starehe tu kwa muda ule au wakati mwingine atakapokuitaji; na si kujichukulia nafasi ya kujifanya wewe ni mke wa pili au kutaka kufanya mapinduzi.

Nadhani nimesomeka.
 

ledada

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
14,506
2,000
Tunajuaa

Usinishushue
IMG_20200828_061635.jpg
 

Misako

JF-Expert Member
Jul 15, 2020
1,155
2,000
Huwa wanatumia nguvu za ziada, lakini mwisho wake huwa sio mzuri; ramani ya maisha ya mwanaume huaribika kabisa. Mwanaume anatakiwa kuwa makini sana, lasivyo majuto yatakuwa yake
Lakini Mara nyingi mwanaume ndo huwa haweki wazi Kama ana mke na familia, mchepuko unajiaminisha mwisho wa cku ukijajua unatumia nguvu kubwa kummiliki...kwahiyo hapa hakuna wa kumlaumu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom