Mwanachuo aliyekuwa akisoma katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Tawi la Mbeya Jofrey J. Nyoni auawa na wananchi wenye hasira

Polisi hawatakiwi kuchunguza kama amekutwa na simu ya wizi nafikiri wanatakiwa kutafuta wahusika walioshiriki kumpiga marehemu mpaka wakamuua.

Nilicheza mpira na mshkaji mmoja hivi jamaa kwao wana hela kiasi chake, yaani ni ile familia inayoweza kumpa mtoto mtaji wa 3M na kumruhusu alete mke aishi naye hapo nyumbani.

At one point mshkaji akaanza wizi wa bajaji na pikipiki. Mwanzo alianza kuiba za pale pale mtaani kesi ikifika kwao wazazi hawaamini kwakua mtoto hakosi kitu pale home pia hana muonekano huo. Basi jamaa akaiva akaanza kupiga dili za mbali na na mtaani pale.

Kipindi hicho nilipokua naishi ni karibu na eneo maarufu kwa giza na kujificha ikifika usiku. Alfajiri nasikia kelele kwamba kuna mwizi anapigwa lile eneo, nikaamka hai hai kufika pale ndiyo namkuta mchizi niliyecheza naye mpira.

Niliganda.

Macho hakuna. Damu kila mahali.

Jamaa alifia pale pale.

Naambiwa ilikua ni nondo na mawe tu.

Na siyo kwamba hawamjui ,wanamjua vizuri tu.

Baada ya hilo tukio ndiyo yakazuka mengine kwamba alikua anashirikia na K huyu ni amekubuhu kuliko. Na lile eneo maarufu kwa giza ndiyo maeneo yao ya uhalifu na wiki moja nyuma walimbaka na kumpora mdada simu. Huyo mdada (inasemekana ana connections zake) akasimamia hilo swala washkaji wakakamatwa wakamlipa mpunga mrefu tu.

So hii next week walikua wamekodi bajaji wakampitisha kule na kutaka kumpora yule dereva alivyoona vile akachomoa funguo akaitupa akaanza kukimbia huku anaitia mwizi. Walinzi wa yale maeneo wakawa wa kwanza kufika kisha raia wa huku uswahilini wakaunga tera.

Basi bwana wazazi wake wakapata taarifa juu ya hiyo ishu wakafungua kesi polisi walioshiriki wakakamatwa. Kesi mahakamani.

Tho watu wanadai walitoka hawa wahusika ila wametumia zaidi ya miaka 3 segerea. Hiyo ni kwakua awe ameiba ama la haihalalishi kufa hata katika hii ishu iwe kweli simu ni ya wizi, kaiba ama la haihalalishi kuuawa.

Now kama ni hivyo askari wanatakiwa wachunguze nini? Kama simu ni ya wizi au wajue wahusika waliompiga? Wakianza na mwenye simu.
 
Hao wananchi wote walio husika katika hayo mauaji, wachukuliwe hatua kali za kisheria. Haiwezekani uhai wa mtu upotezwe kirahisi tu na kwa sababu ya kipuuzi kama hiyo.
 
Umasiki, ujinga na kukosa elimu au Elimu duni. ndio mazao ya haya yanayotokea sasa hivi.

Sijawahi sikia china kuna mwanafunzi ameuwawa kisa simu ambayo hujui kama kweli ya wizi au ya kwake ila labda zimefanana tu sababu simu zina matoleo.

Bila kutatua hivyo vitu japo juu itakuwa ngumu kuendelea kama taifa na haya mambo yataendelea kutokea kila siku.
Inauma sana
 
Lugha rahisi kakutwa na simu sio yake, sasa haijulikani kama kaiba ama kauziwa na mtu mwingine aliyeiba.
Wangemsikiliza pengine angemsema aliyemuuzia, ila kama hajataja aliyemuuzia basi atakuwa kaiba yeye.
Hapo Tunasubiri uchunguzi
 
Uchunguzi wakati mwanafunzi ameshauwa? Nilifikiria hao waliomuua walivyomkamata wakaona simu ni ya wizi wangempeleka polisi uchunguzi ufanyike.
Tatizo nchi yetu wanachukua maamzi mkononi
 
Mwanachuo aliyekuwa akisoma katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Tawi la Mbeya Jofrey J. Nyoni aliuawa na wananchi mwenye hasira kali katika kata ya Sinde jijini Mbeya.

Mwanachuo huyo aliuliwa ikidaiwa kumiliki simu ya wizi wengine wakidai kuwa ameiba simu siku ya tarehe17-05-2021

Taarifa rasmi zilitolewa chuoni tarehe 18-05-2021.

Uchunguzi wa kifo hicho bado unafanyika kubaini kua aliiba au alikutwa na simu ya wizi.

Tuwe wazalendo



wengi wanakutwa na mikasa ya namna hii siyo kwamba wameiba simu hizo ila wanakuwa wamenunua mtaani kwa bei nafuu, kumekuwepo na wimbi kubwa la watu kukamatwa na kutiwa matatani kutokana na kadhia hii.
 
wengi wanakutwa na mikasa ya namna hii siyo kwamba wameiba simu hizo ila wanakuwa wamenunua mtaani kwa bei nafuu, kumekuwepo na wimbi kubwa la watu kukamatwa na kutiwa matatani kutokana na kadhia hii.
Yaani kuchukua sheria mkononi si jambo jema kabisa mkuu
 
Haya yote ni mambo ya watu tu.

Huyo Bwana anasingiziwa na hata ukiomba uthibitisho kwamba yupo hutaupata.

Inasikitisha kuona umasikini na ujinga unavyosababisha watu kuuana.
Nchi ya kutuhumiana na kuuana. Mungu pigania watu wako
Hasira zote hizo ni ugumu wa maisha.
 
KWA MIMI NILIYEIBIWA SIMU JUZI TU NA KUPOTEZA VITU VYA MSINGI NA KAMA KWELI ALIKUWA MWIZI BASI SINA CHA KUSIKITIKIA.

JIFUNZE UISLAMU KUTOKUNUNUA VITU MTAANI KWA KIGEZO CHA BEI YA CHEE.

MIMI BADO NAMTAFUTA MWIZI WANGU, SIKU NIKIMPATA NITAMKAMATA KWA UNYENYEKEVU
 
KWA MIMI NILIYEIBIWA SIMU JUZI TU NA KUPOTEZA VITU VYA MSINGI NA KAMA KWELI ALIKUWA MWIZI BASI SINA CHA KUSIKITIKIA.

JIFUNZE UISLAMU KUTOKUNUNUA VITU MTAANI KWA KIGEZO CHA BEI YA CHEE.

MIMI BADO NAMTAFUTA MWIZI WANGU, SIKU NIKIMPATA NITAMKAMATA KWA UNYENYEKEVU
Dah hii nayo Kali, kazi njema katika utafutaji wa adui yako
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom