Mwana Siasa Safi wa Tanzania (Dr Slaa, Dr Kikwete, Maalim Seif, Hamad Rashid au Mboe)

Pepombili

JF-Expert Member
Dec 20, 2010
439
58
Jamii ya kitanzania ni jamii ya watu wa aina mbali mbali kama zifuatazo:

1-Wakulima
2-Wafanyakazi
3-wafanyabiashara
4-Wanasiasa
5-Wafugaji

Lakini kwa hali ya sasa inaonesha ya kwamba fani ya siasa imevamiwa na jamii ya watu wenye asili ya Ukulima na ufugaji, na asili hii ya watu hawa wengi wao wana sifa ya kutokuwa wavumilivu na wenye hasira na wanaoshindwa kudhibiti hasira zao yaani hawana subra. Siasa ni fani nzito sana inayohitaji uvumilivu wa hali ya juu maana unahusika na jamii moja kwa moja na wala sio ufugaji au ukulima ambao unahusika na ardhi na wanyama. jamii hii ya wakulima walivamia fani ya siasa wengi wao hawana lugha nzuri kwenye vinywa vyao na wala hawana hekma ya siasa ambayo ni lugha safi na matamshi mazuri yenye hekma na bashasha, siasa si hasira.

kwa mtazamo huo mfupi hivi ni nani anastahilikuitwa mwanasiasa maana wengi wamekosa luhga safi na maneno mazuri yenye hekma
 
Sophia Simba na Sokwe ndiyo wanasiasa safi kwa tanzania.

images
 
Nafikiri si vema kumwita mwinzio jina la mnyama hata kama humpendi au huipend chama chake. Sijakubaliana na wewe
 
Mwanasiasa safi ni yule mwenye hasira nyingi dhidi ya wale mafisa wa fedha za umma hapo anayefaa zaidi ni DR.Slaa. tumetofautiana mitazamo
 
Jamii ya kitanzania ni jamii ya watu wa aina mbali mbali kama zifuatazo:

1-Wakulima
2-Wafanyakazi
3-wafanyabiashara
4-Wanasiasa
5-Wafugaji

Lakini kwa hali ya sasa inaonesha ya kwamba fani ya siasa imevamiwa na jamii ya watu wenye asili ya Ukulima na ufugaji, na asili hii ya watu hawa wengi wao wana sifa ya kutokuwa wavumilivu na wenye hasira na wanaoshindwa kudhibiti hasira zao yaani hawana subra. Siasa ni fani nzito sana inayohitaji uvumilivu wa hali ya juu maana unahusika na jamii moja kwa moja na wala sio ufugaji au ukulima ambao unahusika na ardhi na wanyama. jamii hii ya wakulima walivamia fani ya siasa wengi wao hawana lugha nzuri kwenye vinywa vyao na wala hawana hekma ya siasa ambayo ni lugha safi na matamshi mazuri yenye hekma na bashasha, siasa si hasira.

kwa mtazamo huo mfupi hivi ni nani anastahilikuitwa mwanasiasa maana wengi wamekosa luhga safi na maneno mazuri yenye hekma

Ikiwa una ufahamu wa kutosha, siasa ni sanaa iliyoanza zamani sana, kwa taarifa yako, kutongoza ndiyo jiwe la msingi wa siasa, jiulize kama wakulima hawatongozi basi jaribio lako la kutushawishi kuwa siasa haiwafai wakulima tutafikiria kuijadili.
 
Nafikiri si vema kumwita mwinzio jina la mnyama hata kama humpendi au huipend chama chake. Sijakubaliana na wewe

Kuna mtu nilisikia wanamwita simba wa vita, mwingine simba wa yuda, kuna jamaa wanaitwa kondoo wa bwana na wanafurahia, halafu kuna nchi ambapo marafiki wanaitana dogs, halafu Gerald Hando wa Clouds anamwita bonge 'mnyama', Yesu alimwita Herode Mbweha, kuna watangazaji wa mpira walikuwa wakimwita Oliver kahn nyani, walinzi wa baadhi ya Ikulu wanaitana 'Eagle', kuna watu wanasema kimapenzi 'usinipeperushie njiwa wangu'

Kama hiyo haitoshi kuna watu wanaitwa na kufurahia kuitwa kisiki cha mpingo na mengine mengi.

Huenda mwandishi anafaamiana na aliyemwita nyani, pengine ni golikipa mzuri wa timu yake zamani kama Oliver Kahn.
 
Wanasiasa safi ni Yusuph Makamba, EL, RA, EC, Mbangusiro na......orodha ni ndefu sana
 
Mtu msafi duniani kama yupo...na akaingia kwenye siasa basi huyo amevamia siasa, maana manabii na mitume wote ambao tunawakubali kuwa walikuwa wasafi kwa kadri ya kila mtu na imani yake hawakuingia kwenye siasa.

Mara nyingine mahaba ya moyo hayaoni uchafu wa mwanasiasa, na chuki ya moyo haiwezi kuona jema la mwanasiasa. Kama mtu kakupa uwaziri ubaya wake utauonaje, na kama unaamini kakunyima umahiri wake utauonaje?

Mwenye mapenzi ya kweli na nchi ni shabiki wa siasa, na sio mwanasiasa. Na ndio maana mashabiki mnauana wakati Seif anaula, Odinga anaula, Tsvangarai anaula.

Kwa hiyo wasafi ni mashabiki wa siasa, na ndio walioitunisia dunia na kuimisri kabla hawajailibya. Lakini sio wanasiasa.

Labda tuulize kati ya wachafu hawa ni nani ana afadhali!!!!
 
Back
Top Bottom