Mwana JF aaga dunia!

Status
Not open for further replies.
Mungu umpokee kwenye nuru ya uso wako mwana jf mpiganaji mwenzetu. Mme mfiwa, BWANA AKUTIE NGUVU, Bwana alitoa bwana ametwaa jina lake lihimidiwe-AMEN.
 
Rest in eternal peace.
Mme mfiwa, pole sana kwako na familia. I wish you all the strength in the world.
 
Ee Bwana utufundishe kuhesabu siku zetu, umlaze mwenzetu huyu mahali pema peponi amin
 
Pole sana mme na familia yote ,Mungu akupe nguvu ,MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI,AMIN.
 
Sisi wote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea.Mwenyezi Mungu ampe mapumziko mema.
 
Msiba umetufika, wa mwenzetu mwanachama
kwa huzuni naandika,msikie wote hima
mioyo yahuzunika,furaha imetuhama
Upumzike kwa Amani,dada yetu Mpenzi

ee bwana ulitoa, binadamu uliumba
na saa umetwaa, ndugu ulompenda
majonzi yametukaa,simanzi imetukumba
Upumzike kwa Amani,dada yetu Mpenzi

Mwenzetu tulikupenda, Kwa michango bodini
Mola naye kakupenda ,akakuita peponi
japo pumzi imekwenda,daima u mioyoni
Upumzike kwa Amani,dada yetu Mpenzi

Sote sisi tunalia, Kumpoteza mwenzetu
Sote twajiinamia, kumuwaza mtu wetu
Mioyo yetu yaumia,imepata kali kutu
Upumzike kwa Amani,dada yetu Mpenzi

Ewe baba mpokee, Mwenzetu huko mbinguni
Ewe Mola mtolee, Adhabu za kaburini
Malaika msichelee, Kumwongoza mbinguni
Upumzike kwa Amani,dada yetu Mpenzi

MAY THE SOUL OF OUR BELOVED SISTER REST IN HEAVENLY BLISS.
 
Jamani pole sana kwa kumpoteza mwa JF. Hili ni pigo hapa. Pole nyingi pia kwa mme uliyempoteza mke. Huu ni wakati wake mgumu. Lakini jipe moyo. Na uwe na faraja ya Mungu mwenyewe.
 
Pole sana Ndugu mfiwa!,
Wafiwa wote poleni ikiwa ni pamoja na wana JF. Tumeondokewa na mpiganaji mwenzetu. Ila tufahamu kuwa yeye ametutangulia tu katika hiyo safari.
 
Poleni sana kwa msiba huu mzito
Mungu mwenyewe aliye Faraja, awafariji
Awatie nguvu na kuwasimamia
Na ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.

Amin
 
Sisi tulimpenda ila mwenyezi Mungu kampenda zaidi yetu ndo maana kamwita kwake....
Bwana uilaze mahala pema peponi Amina..
Pole sana ndugu wa marehemu katika kipindi hiki kigumu..
 
Members nimetoka msibani muda sio mrefu.Nimeongea na Max akirudi atutangazie utaratibu mzima wa Kumuaga dada yetu ili kwa yule atakaye kuwa na nafasi tujumuike pamoja.

Bwana ametoa na bwana ametwaa,jina la Bwana libarikiwe.
 
Pole sana Bwana mfiwa kwa Msiba mzito uliokukumba..poleni sana na wana JF wote kwa kupotelewa na kamanda wetu tunayeamini kuwa mchango wake ulisaidia sana kwa namna moja au nyingine kuendeleza gurudumu ya kutaka kuona mwangaza katika nchi yetu. may her soul Rest In in Peace.. AMEN.....!!
 
pole kaka mfiwa na familia yako yote kwa ujumla....mpo kwenye sala zangu!! mwenyezi mungu amrehemu marehemu, amin.
 
Pole kwa mme mfiwa na familia nzima katika kipindi hiki kigumu...Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi.
Amin
 
Pole kwa mme mfiwa na familia nzima katika kipindi hiki kigumu...Mwenyezi Mungu amlaze mahali pema peponi.
Amin
 
Pole sana nzugu yetu (mme) mwenzetu katangulia tu sisi tuko nyuma yake.....allah akbar
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom