Mwana JamiiForums Mwenzangu asikudanganye Mtu na usivunjike Moyo unaweza ukakimbiwa na kudharauliwa na wengi, ila Mungu 'atakuteulia' tu wa Kukusaidia

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,546
108,875
LIPO JAMBO KUBWA SANA LA KUJIFUNZA KWENYE STORY HII.

Simulizi ya Maisha ya Kweli:

Ronaldinho 'Gaucho' alipokamatwa pamoja na kaka yake Roberto Assis kutokana na kesi ya matumizi ya pasipoti bandia huko nchini Paraguay na kuwekwa kizuizini katika gereza lenye ulinzi mkali la Agrupacion Especializida kwa siku 32.

Ni wachezaji WAWILI tu walifika kumtembelea akiwa gerezani; anatajwa Samuel E'too na nyota wa kimataifa wa Paraguay Nelson Cuevas.

Etoo alifika kumtembelea Gaucho huko gerezani, na hakuacha bali aliendelea kumpigia simu kila jioni kujua Gaucho anaendeleaje na kumpa matumaini kuwa mambo yatakuwa sawa.

Unaambiwa hata mama yake, mkewe au ndugu zake Ronaldinho hawakufanya hivyo kama alivyokuwa akijitoa Etoo.

Baada ya kukiri mashtaka hayo, Gaucho na kaka yake walitozwa faini ya Pauni 200,000 pamoja na adhabu ya uvunjaji sheria yenye jumla ya takribani Pauni 27,000.

Inaripotiwa kuwa Gaucho alimjulisha Etoo juu ya faini hiyo, na Etoo alijibu: "Usijali kaka, nitashughulikia kila kitu" na akalipia pesa yote ili Ronaldinho aachiliwe.

Katika marafiki zake wote mastaa ambao Ronaldinho alikuwa nao katika mafanikio yake ya maisha yake ya soka, ni huyu Mwafrika tu ambaye wakati mmoja aliitwa "nyani" na mashabiki Wabaguzi huko Uhispania na Italia lakini wakati huu yeye ndiye alikuwa mbele kwa ajili ya kumsaidia.

Jifunze kuwa; marafiki wa karibu ambao unatengeneza leo wanaweza wasiwepo kesho, lakini kutakuwa na mmoja siku zote ambaye atakuwa zaidi ya familia kwako.

Urafiki unapimwa kwa uwezo wa kusimama pamoja wakati mmoja anapokuwa kwenye uhitaji.

Cloudstvtz

Asikudanganye Mtu wala Usivunjike Moyo juu ya yale unayoyapitia hata kama utakwepwa na kudharauliwa yupo Mtu Mungu Kakuteulia Kukusaidia.
 
Nimesikia mtu anasema Urais ni kazi ngumu kweli, analalamika eti hiyo kazi anajitolea kweli
cha ajabu hataki kuiacha amewafukuza chama mpaka waliotaka kugombea nae huko ccm.... nimemkumbuka mtu mmoja anaitwa Chief Nanga kwenye kitabu cha “A Man of the people.”
 
Una uhakika ulichokiandika kwa 100% 'Kimaudhui' kinaendeana na 'Uzi' unavyosema?
Kwa watu walio soma vileee vitabu vya literature kuna mambo Yana reflect kabxaa mfano kwenye “An Enemy Of The People” Tundu Lissu anasimama kama Dr. Stockman pia kuna “His Excellency the Head of The State” Humu unamkuta Makonda na Magufuli By the way Literature is real my young broo
 
kwa watu walio soma vileee vitabu vya literature kuna mambo Yana reflect kabxaa mfano kwenye “An Enemy Of The People” Tundu Lissu anasimama kama Dr. Stockman pia kuna “His Excellency the Head of The State” Humu unamkuta Makonda na Magufuli By the way Literature is real my young broo

Nadhani kuna 'Jibu' baya na ambalo litakufanya uupate 'Usingizi' wako haraka ukalale unalitafuta kwa 'lazima' kutoka Kwangu. Tusilaumiane sawa?
 
Kuna wakati unaitendea haki picha ya Benjamin Netanyahu aka Bibi (sayeret matkal) alumni ila sasaaaa ukishaanza kuanguka kifafa jf inakuwa shida unafanana na Don nalimison Don Nalimison
 
Back
Top Bottom