Bora hiyo harusi ifanyikie hapo inafanyikia mbaaaliiiiii nauli ya kwenda kurudi malazi, unanunua ng'ombeNitoe pesa ya mchango,
Nitoe pesa ya nguo sijui sare,
Nitoe pesa ya zawadi,
Bado sijafanya make up,
Hehehehe
Tena usiombee waoane wakiwa washatiana mimba, hujakaa sawa kidogo mtoto kazaliwa upeleke zawadi bado arobaini ya mtoto ukinusurika kuchangishwa basi zawadi lazima, looooh!
Sio harusi, showers, birthday maana siku hizi hadi vipaimara tunaletewa kadi..hii jamii imekujankuwaje ... Yaaani mtoto aende mafundisho miezi 6-8 usijipange uje uchangishe watu !!??Kuna mambo mengine kwenye jamii hayaepukiki moja wapo ni hili la kuchangia mambo ya kijamii.
Toka hapo ulipo nenda kanuunue nguo duiani, kanunue maredio na ma tv na Kodi bodaboda zunguka mji wote utasaidia watu kupata ajira ati.Haikupi raha kuona mchango wako unatoa ajira kwa watu?
Siku hizi mpaka birthday watu wanataka michango.
Nakubaliana na MwanaFA, ajira sio lazima utegemee michango yetu. Hebu tupumzisheni, hapa Nina kadi za ndoa sita harusi kabla ya xmas ambazo naona moja ndio labda watavuka miaka mitano.Najua Hamisi Mwinyijuma au Mwana FA ni miongoni mwa wasanii wachache wasomi tulionao hapa Tanzania.
Ukiwa msomi, tunatarajia uwe na fikra pana na za kina kwenye masuala mbalimbali ya kijamii na mazingira yanayokuzunguka, ukiachana na yale ya fani uliyosomea.
NATAKA KUSEMA NINI?
Nimeona video fupi ikisambaa inayomuonesha MwanaFA akizungumzia suala la michango ya harusi. Kwamba, yeye hachangii harusi kwani ni suala la mtu binafsi na linahitaji maandalizi. Yuko tayari kuchangia Msiba, si harusi.
Kwanza, huo ni mtazamo unaofikirisha lakini pia ni mtazamo wa watu wengi. Watu wamechoka na utaratibu wa kuchangia harusi. Mimi ni mmojawapo
Hata hivyo, nikiangalia mnyororo wa thamani uliopo kwenye hizi sherehe na ajira zilizozalishwa, nabaki kuona ni jambo zuri na lenye tija.
Ukichangia harusi, unatoa ajira kwa watu wengi sana. Kuanzia MC, watu wa mapambo, chakula, wapiga picha, maids, watoa burudani n.k.
Faida nyingine ni mzunguko wa fedha kuchochea uchumi wa eneo husika, kuimarisha undugu na ujamaa, kutengeneza kumbukumbu na mengine mengi.
Wapo wasiochangisha watu kwenye mambo ya sherehe, lakini hao ni wale wanaojiweza, vipi wale wasiojiweza?
USHAURI WANGU
Tusiache kuchangiana kama tunapendana na kushirikiana. Umoja ni nguvu. Sherehe za harusi sio suala binafsi tena, ni suala la kiuchumi na maisha ya watu wengi yanategemea hapo.
Mwezi wa 6 mwakani nafunga ndoa. Nitatoa kadi za michango. Mnichangie. Puuzeni maneno laini laini ya Hamisi.
Nendeni kanisani barikini ndoa Kisha nendeni kwenu kale ugali dagaa siku inakwisha.Sherehe sio lazima mkuu. Anaweza funga ndoa vizuri kabisa bila ya sherehe kama uwezo ni mdogo.