Mwamunyange na Mwema watakiwa kujiuzulu

calmdowndear

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
605
271
Mkuu wa Majeshi Nchini, Davis Mwamunyange na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema nao wametakiwa kujiuzulu kutokana na uozo uliobainika katika ripoti ya Operesheni Tokomeza Ujangili, iliyosababisha Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa mawaziri wake wanne.

2.JPG

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam katibu wa madiwani wa jiji hilo, Julian Bujugo alisema wakuu hao wanapaswa kujiuzulu kwa kuwa wao ndio wanaotoa amri kwa askari wao na siyo mawaziri.

“Nao wanatakiwa kuchukua uamuzi wa kujiuzulu kama hatua ya kuonyesha uwajibikaji wao, askari wao wamefanya maovu makubwa,” alisema. Alisema kama wakuu hao wa watakaidi agizo la madiwani watalipeleka suala hilo kwa Rais Kikwete.

“Watendaji wa Serikali ndio chanzo cha uonevu, hata mawaziri ‘mizigo’, nao wanatakiwa kujiuzulu. Alimtolea mfano Waziri wa Chakula na Ushirika, Christopher Chiza, Bujugo alisema ameshindwa kuwasimamia wakulima na kusababisha mvutano na vurugu katika Sekta ya Kilimo.

Chiza alitajwa kama waziri ‘mzigo’ na Kamati Kuu ya CCM iliyokutana wiki mbili zilizopita chini ya uenyekiti wa rais Kikwete.

Bujugo ambaye ni diwani wa Kata ya Magomeni alisema mbali na wakuu hao wa ulinzi na usalama, pia wakuu wote wa wilaya waliohusika kusimamia operesheni hiyo nao wanapaswa kuwajibika kwa kuwa walijua na waliona wazi vitendo vichafu walivyofanyiwa wananchi lakini walikaa kimya.

Ripoti ya tume ya kuchunguza Operesheni Tokomeza Ujangili ilisomwa bungeni mjini Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita na mwenyekiti wa Kamati hiyo, James Lembelii na kuwango’a mawaziri hao.

Waliong’olewa ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki, Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dk Mathayo David na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Shamsi Vuai Nahodha, huku Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa njia panda kutokana na wabunge kuendesha mpango wa chini chini wa kupiga kura ya kutokuwa na Imani naye kwa maelezo kuwa ameshindwa kuwasimamia mawaziri wake.
Dar News Line: ‘Mwamunyange, Mwema wajiuzulu'
 
Mi naunga Mkono hoja.maana maaskari na wanajeshi ndio waliokuwa wanatesa watu,sasa nao pamoja na wakuu wao lazima wawajibike,Tanzania hii tunaoneana sana,ila mwisho wake umekaribia,haiwezekani hao wajinga waende kuua ng'ombe wa watu kisa wanatafuta majangili wanaoua tembo,wakati wauza meno tembo waliwaacha dar na wanawajua mpaka majina,afu wanaenda kuonea watu vijijini.
 
Ndipo mnapoishia, kila kitu policcm, usilete siasa kwenye mambo serious. Hivi operesheni hiyo ilifanywa na Polisi peke yao? Vyombo vyote vilihusika ila wenye kimavi ni Polisi tu!
 
Ndipo mnapoishia, kila kitu policcm, usilete siasa kwenye mambo serious. Hivi operesheni hiyo ilifanywa na Polisi peke yao? Vyombo vyote vilihusika ila wenye kimavi ni Polisi tu!

Mbona unahsira mkuu ulishiriki kuwapiga mtungo kwa vijiti ndgu zetu nii, tupa hao wote nje na tupia ndani kama mnaogopa kupinduana
 
Mi naunga Mkono hoja.maana maaskari na wanajeshi ndio waliokuwa wanatesa watu,sasa nao pamoja na wakuu wao lazima wawajibike,Tanzania hii tunaoneana sana,ila mwisho wake umekaribia,haiwezekani hao wajinga waende kuua ng'ombe wa watu kisa wanatafuta majangili wanaoua tembo,wakati wauza meno tembo waliwaacha dar na wanawajua mpaka majina,afu wanaenda kuonea watu vijijini.

Kinana hajakamatwa wakati hata mtoto mdogo anajua kuwa Kinana ni jangili number moja(according to Msigwa)
 
IGP Mwema na CDF Mwamunyange hawana namna ya kukwepa kitanzi.Ni LAZMA WAACHIE NGAZI BILA SHURUTI!Sio kuachia ngazi tu baali WASHTAKIWE pia.
Lazima waelewe kuwa kilicho wang'oa Mawaziri wao kimesababishwa na wao kama Watendaji wakuu kwenye idara zao!

Rais Kiwete ataendelea kudhihirisha UDHAIFU wake kama atawaacha hawa jamaa waendelee kukalia afisi hizo.

Kama anataka kuwa FAIR lazima LUNGU LISHUKE MPAKA kiongozi wa chini kabisa aliyehusika na unyama huu!
 
Mbona unahsira mkuu ulishiriki kuwapiga mtungo kwa vijiti ndgu zetu nii, tupa hao wote nje na tupia ndani kama mnaogopa kupinduana

Sina hasira Chikutentema, Jeshi ni amri na maelekezo. Askari walipewa bunduki, hawakupewa kondom, chupa wala vijiti. Sasa hawa wakiondoka atakaekuja atatokea mbinguni ajue askari wana nini mioyoni mwao? Vile vile siku nyingine wasifanye operesheni zinazochanganya wanaotafuta ushahidi wa kwenda mahakamani na wanaotoa hukumu ( mitazamo ya majeshi yetu iangaliwe).
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom