Mwamposa na wenzake waachiwa kwa dhamana. Najiuliza kesi ya mauaji ina dhamana? Ila ya uchochezi/ kutakatisha haina?

Laiti kama ule mkanyagano ungetokea kwenye kumbi za starehe aidha vibanda umiza vya mpira sijui leo hii mmiliki wa eneo kama angeachiwa kwa dhamana.
 
Utajiri hauji kwa kwa kukanyaga mafuta, acheni kudanganya watu, waambieni wakajishughulishe na wafanye kazi kwa bidii
Utajijua utajiri bila kushirikisha mambo ya kiroho hutoki piga ua hata uwe wa dini yeyote na mchapakazi kupindukia hutoki
 
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limewaachia kwa dhamana watu wanane akiwemo Mtume na Nabii, Boniface Mwamposa wanaotuhumiwa kuendesha kongamano lililosababisha vifo vya watu 20 mjini Moshi. Msemaji wa Polisi, David Misime amethibitisha

Chanzo: MwananchiUpdates
Hivi kesho us Akwilina, watuhumiwa wamewekwa ndani
 
Ila heri wamepoteza maisha kwenye maisha ya kumtafuta Mungu kuliko kufa kwenye disko au kwenye kudanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio suala la kumtafuta Mungu bali miujiza tu na ndiyo hata watu wa imani zengine huwa wanakuwepo na si ajabu walikuwepo,Mwamposa ni maarufu kwa sababu ya hiyo miujiza na si kwamba labda ana mahubiri mazuri wala nini.
 
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limewaachia kwa dhamana watu wanane akiwemo Mtume na Nabii, Boniface Mwamposa wanaotuhumiwa kuendesha kongamano lililosababisha vifo vya watu 20 mjini Moshi. Msemaji wa Polisi, David Misime amethibitisha

Chanzo: MwananchiUpdates
in love in life in war nothing is fair
 
Sio suala la kumtafuta Mungu bali miujiza tu na ndiyo hata watu wa imani zengine huwa wanakuwepo na si ajabu walikuwepo,Mwamposa ni maarufu kwa sababu ya hiyo miujiza na si kwamba labda ana mahubiri mazuri wala nini.
Ni kweli watu wanaifuata miujiza na wanaipata.Hata YESU WATU KIBAO WALIMFUATA KUFUATA MIUJIZA NA WALIIPATA

Mimi mmojawapo mpenzi wa miujiza kwa Mwamposya na huwa naipata

Wafuasi wa YESU WAKO AINA MBILI KUNA WALE WANAOMFUATA KWA SABABU YA NENO TU NA WAKO WANAOMFUATA KWA SABABU YA MIUJIZA

WOTE NI WAFUASI WAKE
 
Tatizo Polisi wameona nao wanakosa la kutokuweka ulinzi wa kutosha sasa wameanza kufichana ...Hakuna kesi hapo so longer polisi nao wanahusika
Kwa mfano polisi wangekuwepo wangefanyaje?huoni kuwa pengine tatizo lingezidi zaidi?
 
Kwa hili sioni mantiki ya kuendelea kumshikilia mwamposa wakati watu wamekufa kwa ujinga wao

Nadhani serikali ilimuifafhi tu kwa usalama wake na baada ya kujiridhisha uhakika wa usalama wake ndipo wakaamua kumuachia

It's Scars
Usiseme watu wamekufa kwa uzembe bali sema kuna watu walifanya uzembe,kumbuka katika hao waliyokufa miongoni mwao ni watoto hivyo huwezi kujua kama walijikuta wamezongwa na watu na kukanyagwa na kupelekea umauti.
 
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limewaachia kwa dhamana watu wanane akiwemo Mtume na Nabii, Boniface Mwamposa wanaotuhumiwa kuendesha kongamano lililosababisha vifo vya watu 20 mjini Moshi. Msemaji wa Polisi, David Misime amethibitisha

Chanzo: MwananchiUpdates

Haya mambo ya kidini yasichanganywe na mambo ya kisheria. Kuna watu wa dini fulani wanajisikia au wana inferiority complex, na hata wakifanya makosa wakichukuliwa hatua, basi wanaona wameonewa na hizo hatua zimechukuliwa kwa ajili ya kuwakomoa.

Katika makosa, sheria inaagalia motive behind. Kuna kosa la kukusudia na kosa la kuto kukusudia, japo yote ni makosa.

Sasa hili la Mwamposa, yawezekana uchunguzi wa hawali unaonesha hakukusudia na ndiyo maana amepewa mdhamana. Upelelezi ukikamilika, basi hatua stahiki zitachukuliwa.

Tukio lililotokea linahumiza, lakini si tukio la kwanza kutokea. Kuna wakati mahujaji wengi tu wanakufa kwa kukanyagana huko wanapoenda kuhiji. Sujawahi kusikia wakisema hiyo shughuli isitishwe au ipige marufuku kwa kusababisha vifo.
 
Wanasheria wetu wanasema kesi ya kuua bia kukusudia ina dhamana,. Lakini kwa sisi wabobevu wa Elimu ya ulimwengu wa roho tunajua nini maana yake na nini kitafuatia.
 
Back
Top Bottom