Mwamposa inabidi amheshimu sana Mwakasege

nashukuru mzima

JF-Expert Member
Jul 11, 2017
1,014
1,896
Habari wana JF,

Tukianza kuangalia kiuhuduma, kiumri, kiujuzi wa neno la Mungu tutakubali Mwakasege ni baba wa Imani kwa Tanzania hii.

Kinachonileta hapa,

1. Inakuaje hawezi kumwachia hata siku moja Mwalimu Mwakasege pindi anapokuwa na semina yake mfano tar 12/10 Mwakasege ana semina ya neno la Mungu kawe na yeye mwamposa ameamua kuweka kongamano lake la maji na mafuta. Huu siyo uugwana na ustraabu kwa mtumishi wa Mungu, kama Pastor Tony Kapola aliweza kumpisha Mtumishi wa Mungu kwanini yeye asiweze kufanya hivi.

Mkutano wa mwisho alioufanya Mwakasege, Mtume Mwamposa aliweka sauti ya juu sana Ilibidi kamati ya Mwalimu Mwakasege wamuombe Mwalimu wakamuombe apunguze sauti ila Mwakasege alikataa na akasema acha mkutano uendelee.View attachment 2382980View attachment 2382983View attachment 2382982View attachment 2382981
 
Kila mtu ataenda atakapoona panafaa si eti wote wanahubiri neno la Mungu? Au unataka kusema wananyanganyana mashiki kama show za mziki.

Mwakasege namkubali
 
hekima ni kuachiana, kila mmoja ana waumini wake mkuu
Kaka kama unafuatilia vizuri mambo ya kiroho hauwezi kumfananisha mwakasege na mtu yoyote hapa Tanzania.

Hekima aliyotakiwa kutumia mwamposa ni kumwachia eneo mbona alikuwa anafanya hivyo mwanzoni naona kwa sasa Jeuri imemjaa.

Soma biblia uone Elisha alivyokuwa ananyeyekea kwa Elia.
 
Kuna siku palikuwa na Mwakasege, Mwamposa na huku Majizzo Komaa Concert na kote nilihudhuria.

Kuna muda upo kwa mtume halafu majizo kule anaachia goma la hakuna mungu kama wewe, ah! Ila jamani lile goma kijitonyama walilitengeneza aisee, yaani hadi club linarukika.
 
Back
Top Bottom