Mwamposa aliiga huku kwa baba lao TB Joshua

Kitaja

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
2,836
1,381
Jumla ya watu wanne wamefariki Jumapili nchini Ghana, walipokuwa wakikanyagana kwenye huduma ya “Mafuta ya Upako” katika kanisa la Synagogue Church of All Nations lililoanzishwa na Mtume TB Joshua wa Nigeria. Msemaji wa polisi wa Mkoa wa Greater Accra kamanda Freeman Tetteh alisema wengine 15 walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini.

Mr Tetteh alisema waliokufa walikuwa wanawake watatu na mtu mmoja lakini umri haukujulikana. Kufuatia vifo vya watu hao “polisi wameshauri viongozi wa kanisa kuacha usambazaji wa mafuta ya upako,” alisema.

Baadhi ya viongozi wa makanisa wamelaani jinsi anavyoendesha ibada zake, wakati wengine wamehoji historia yake kama mkristo.

Hata hivyo Mtume Joshua, amekanusha madai hayo kwamba hayana msingi na ni wivu kwa watu wanaotishiwa na mafanikio yake.

Africareview
 
Back
Top Bottom