Mwampamba Amjibu Dr Slaa

Tatizo siyo kumsikiliza Mwampamba tatizo kwa nini Dr Slaa akope pesa za ruzuku katibu ya Chadema inasemaje.

Bora hutu anachukua na kurudisha,hata km katiba hairuhusu.huko kwingine wanachukua jumla jumla, a k a kufisadi!
 
acheni ----- wenu nchi ina mambo mengi ya maana ya kujadili au ndo mnatumika!!!

Wanatumika kama nanii na kutupwa,kazi yao kubwa kuwatoa watu katika kujadili mustakabali wa taifa hili na kutuletea upuuzi
 
heko sana mkuu,tunataka vijana wa wazi na si wanafiki,asante kwakuendelea kutufungua macho!
 
Mtela kama una hoja jaribu kuwa na staha, huwezi kutukana kiasi hicho kwa mtu anaye kuzidi umri alafu ukaachwa tu uendelee dogo nakwambia hivi utapata laana ambayo hukuitegemea, nimeamini ya kuwa kweli ulipogombea umbunge mbozi mashariki na vijana wengi wakakuunga mkono , hukuwa na nia hiyo ila ulikuwa na malengo fulani ( Hasa ya kutumika)
 
mi nadhani hoja hii iangaliwe kwa pande mbili, 1.kwa maana ya utaratibu uliotumika kukopesha. 2. Ni je kuna ubadhirifu wowote uliokutwa na CAG? je mwampamba anawezaje kuhoji akiwa nje km co kuendelea kutumika? Hebu alete hoja za viongoyi wa ccm kukamatwa na nyara za serikali, mambo ya mabilion yanayokwibwa kila kukicha, na ugumu wa maisha unaowakumba watanzania labda zitamsaidia mwampamba na siyo hoja mfilisi km hii.
 
mkuu upo? habari ya leo?

katiba ya chama chochote inataratibu zake, kuhusu hili

1. Katiba inasemaje ya chadema? maana sisi wengine mtufumbue macho.

2. Kutokana na jibu la 1 utaratibu umefutwa kuwakilisha malalamiko panapohusika kama upo na nani kawasilisha, kama haujafuatwa nini mtazamo wako, tuite haya majungu au uzushi? au malalamiko yasiyo rasmi

Nipo kama unavyoona. Hebu nirushie katiba na financial policies za CHADEMA kama zipo karibu hapo tuangalie taratibu za kukopa kama zilifuatwa.
 
Kukopa sio kuiba ndugu yangu ila kama utaratibu haukufuatwa hapo ndipo penye tatizo.

Utaratibu upi haukufuatwa. Mwampambaism? Umeambiwa kwenye katiba kama mpaka kukopa na kukopeshana kutakuwepo basi hiyo siyo katiba maana itakuwa inabeba kila kitu. Sasa kama unafikiri kuna utaratibu ulikiukwa mbona husemi au mbona mtoa tuhuma hasemi. Katiba iko silent na labda utaratibu haukuwepo wa kukopeshana. Sasa kwakuwa haukuwepo mwenye shida asipate mkopo. Kila kitu kina mwanzo kama haukuwepo basi ulianza na Dr. Slaa na mweingine akitaka mkopo kama pesa ipo ni kuwekeana makubaliano ya kurudisha katika wakati mwafaka.
 
Nipo kama unavyoona. Hebu nirushie katiba na financial policies za CHADEMA kama zipo karibu hapo tuangalie taratibu za kukopa kama zilifuatwa.

mkuu kumbe unapiga kelele kufuata mlio wa ngoma? nimesema mtufumbue macho nasisi nikiamini unachokilalamikia unakifaham

inamaana unafata upepo? angalia kwenye blue hapo chini.

quote_icon.png
By adolay

mkuu upo? habari ya leo?

katiba ya chama chochote inataratibu zake, kuhusu hili

1. Katiba inasemaje ya chadema? maana sisi wengine mtufumbue macho.

2. Kutokana na jibu la 1 utaratibu umefutwa kuwakilisha malalamiko panapohusika kama upo na nani kawasilisha, kama haujafuatwa nini mtazamo wako, tuite haya majungu au uzushi? au malalamiko yasiyo rasmi
 
Mkuu Freshthinking.

Kwanza hongera kwa kuona kuwa matusi haya kubaliki hasa kwa kijana kumuita mtu aliye kuzidi umri majina yasio faa! Hii ni kinyume na mila na desturi za kijana wa kitanzania.

1. Katiba za vyama vingi hazina kanuni au sheria za kukopesha au kukopeshana, cha msingi tambua kuwa kutokuwepo kwa kanuni au sheria za kukopeshana hakuondoi uhalali wa mhusika kuomba mkopa au kukopeshwa kama kuna makubaliano ya kimaandishi au yaki ofisi na utayari wa kutoa mkopo huo kwa mhusika.

Ndio maana nikasema aachwe apige kelele na kutukana akichoka ataenda kulala.

Mimi nakubaliana na wewe bwana Mohamed Mtoi inawezekana hata taratibu zikapindwa wakati fulani pale ambapo kuna dharura. Inawezekana huo mkopo aliuchukua kwa ajili ya matibabu, mazishi, au dharura nyingine za kibinaadamu.

kwa hiyo hoja za msingi ni:

1) Lengo la huo mkopo ni lipi kwa sababu chama hakiwezi kutoa mkopo kwa ajili ya kwenda kuoa!

2) Qualification criteria za hiyo mikopo ni ipi ili na wanachama wengine waende kukopa

3) Kukopa kama utaratibu umefuatwa sio ufisadi lakini ukiukwaji wa taratibu katika mambo ya fedha kama haya ndio hupelekea ufisadi kutokea.
 
Utaratibu upi haukufuatwa. Mwampambaism? Umeambiwa kwenye katiba kama mpaka kukopa na kukopeshana kutakuwepo basi hiyo siyo katiba maana itakuwa inabeba kila kitu. Sasa kama unafikiri kuna utaratibu ulikiukwa mbona husemi au mbona mtoa tuhuma hasemi. Katiba iko silent na labda utaratibu haukuwepo wa kukopeshana. Sasa kwakuwa haukuwepo mwenye shida asipate mkopo. Kila kitu kina mwanzo kama haukuwepo basi ulianza na Dr. Slaa na mweingine akitaka mkopo kama pesa ipo ni kuwekeana makubaliano ya kurudisha katika wakati mwafaka.

You are shootingi in the dark boss!
 
Kalaniwa huyu kijana! Nadhani CCM watawauwa vijana wote waliowatuma na kushindwa kazi ili kuficha siri, isije siku moja wakaanza tena kuropoka walivyotumwa. Maana mi sioni hoja. Mimi kunakipindi nilikuwa nafanya kazi kampuni binafsi tulikuwa tunakopeshwa kama motivation ya kuendelea kufanya kazi kwenye kampuni na nilichukua mil 12, nikamaliza kulipa nikaongeza tena mil 8 kumalizia kujenga nyumba yangu, sembuse huyu Dr Slaa. Hoja zake huyu kijana zimejaa majungu na ninadhani wazee wa mtandao wa CCM watawamaliza wapumzike mapema.
 
Jibu hoja ya msingi katiba ya cha inasemaje kuhusu pesa za chama.
Ritz, hatujui yanayoendelea CCM na vyama vingine kwakuwa wao mambo yao wanayafanya kwa usiri mkubwa sana. Hivi unafikiri mabilioni kwa mabilioni wanayokusanya CCM kutokana na miradi waliyopora kwa wananchi (viwanja, ofisi, na kumbi) wanayatumiaje? Je unajua CCM wanapokea kiasi gani cha ruzuku kila mwezi? Je wanafanyia nini? Kinachowasaidia hawa wenzetu, ni kwamba mambo yao hufanywa kwa usiri mkubwa. Mtu mpuuzi kama Mwampamba hapati nafasi ya kujua kinachoendelea humo ndani. Uwazi wa CHADEMA katika utendaji wa mambo yao ndiyo unaowafanya wafike mahali wasakamwe kiasi na wachumia tumbo kama akina Mwampamba.
Sasa Ritz utajiuliza, Mwampamba ameshafukuzwa CHADEMA, na tayari yupo NCCR, sasa hasira zake na CHADEMA ni za nini? Si akatulie huko?
 
Last edited by a moderator:
Sikia Mwigulu Nchemba, Dr Slaa hawezi kujibu upuuzi huu, Mwambamba ni mtu mdogo sana, tuna mambo muhumu ya kushughulikia lkn si yeye. Zaidi tunaona tabia yake halisi, hana adabu kwa wakubwa zake.
 
Back
Top Bottom