Mwamnyeto, Mkude, Shomari,Tshabalala Watemwa Stars

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,293
24,173

September 13, 2022




Kocha mkuu wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’, Honour Janza ametaja kikosi cha wachezaji 23 kitakachoingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mechi za kirafiki zilizopo kwenye kalenda ya FIFA akiwatema Bakari Mwamnyeto na Mohamed Hussein 5‘Tshabalala’.

Kocha Honour Janza pia amemrejesha kikosini beki Abdi Banda anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Chipa United ya Afrika kusini akiongeza nguvu katika kikosi kitakachocheza mechi za kirafiki zilizopo kwenye kalenda ya FIFA.

Banda mara ya mwisho kuitwa kwenye timu ya taifa ni kipindi alichokuwa anacheza soka la kulipwa katika klabu ya Baroka ambayo baadae aliachana nayo na kurejea nchini msimu uliopita na kucheza Ligi Kuu akiwa na Mtibwa Sugar.

Ingizo la Abdi Banda kwenye kikosi kunamuondoa nahodha wa Yanga, Bakari Mwamnyeto wakati huo huo David Luhende ameingia akichukua nafasi ya Mohamed Hussein ‘Tshabalala’.

Wachezaji wengine walioachwa kwenye kikosi hicho ni Shomari Kapombe, George Mpole, Reliants Lusajo, John Bocco, Farid Mussa, Kibu Denis na Jonas Mkude.


Na nafasi zao zimechukuliwa na Datius Peter (Kagera Sugar) Abdalah Mfuko (Kagera Sugar) Carlos Protas Kirenge (Tusker Fc), David Richard Ulomi (Moroka Swallows) na Said Hamis (Hatta Club)

Akizungumzia upande wa kuita sura mpya nyingi, kocha Janza amesema imetokana na viwango ambavyo wamevionyesha kwenye timu zao.

“Sisi benchi letu ni kuangalia kila mchezaji ambaye anafanya vizuri na tunamuita kwa ajili ya kuipambania timu ya Taifa, milango bado ipo wazi kwa wachezaji wengine.” amesema Janza.


Upande wa kocha msaidizi, Mecky Maxime akizungumzia upande wa kukosekana mchezaji Tepsi Evance amesema , ”Sio yeye tu hata Sopu (Abdul Suleiman) tumewaweka kwenye timu chini ya miaka 23 kwa sababu wana mashindano yao.”

Stars inatarajia kuanza kuingia kambini Jumamosi na Jumatatu watafanya mazoezi mepesi kisha Jumanne wataondoka kwenda nchini Libya kucheza mechi za kirafiki mbili na timu hiyo kuanzia tarehe 20.


1663072032741.png

Kalos Protas Kirenge mlinzi wa kati, urefu 6.2ft timu alizochezea Tusker ya Kenya na Namungo FC ya mkoani Lindi ameitwa Taifa Stars.


1663072210016.png

Winga hatari David Richard Ulomi mchezaji wa Moroka Swallows ya South Africa.

Timu alizochezea Al Hillal Sudan, , Dodoma Jiji, Alliance FC ya Mwanza na Ruvu Shooting stars amekataa kabisa kuja kuchezea klabu za Dar es Salaam

13 September 2022

Kocha mkuu wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’, Honour Janza ataja kikosi cha wachezaji 23



Kocha huyo raia kutoka Zambia ambaye pia aliwahi kuzifundisha Timu ya Taifa la Zambia almaarufu kama Chipolopolo, Red Arrows pia ya Zambia na Namungo FC ya Lindi Tanzania kwa mafanikio, amewataja wafuatao kujiunga na Taifa Stars

1663073040252.png
 
Nilipata mshtuko nilipowakosa Tepsi na Sopu kikosini lakini kocha msaidizi Mecky amefafanua kuwa wapo kwa ajili ya U23 na wana mashindano yao,, ndipo nikapata ahueni vinginevyo nisingekaa nikawaelewa kabisa
 
Nilipata mshtuko nilipowakosa Tepsi na Sopu kikosini lakini kocha msaidizi Mecky amefafanua kuwa wapo kwa ajili ya U23 na wana mashindano yao,, ndipo nikapata ahueni vinginevyo nisingekaa nikawaelewa kabisa
Kuna mwamba rafiki anasema naye alikua player anasema amecheza sana na Sopu game za michangani mbagala nk nikimcheki jamaa Age imeenda kwenye 26 -29 halafu Sopu bado yupo U23.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom