Mwamko wa Kuikimbia CCM: CDM inaachwa nyuma...wakati CCM wanajipanga? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwamko wa Kuikimbia CCM: CDM inaachwa nyuma...wakati CCM wanajipanga?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, May 11, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 11, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Kuna kasi ya ajabu tunayoishuhudia ya mwamko wa wananchi waliofunguliwa kuikataa CCM. Karibu kila kona ya nchi makundi ya mamia ya watu wanajitokeza pasi ya hofu wala utata kusema wanaikataa CCM na mambo yake yote. Baada ya mabadiliko nusunusu na hasa baada ya mjadala wa Bungeni kuna watu walitarajia kuwa wananchi watatulia lakini ndio wanazidi. Kuna wimbi la mwamko huo ambalo sasa linatangulia mikutano ya viongozi wa kitaifa wa CDM; viongozi wa mahali (local leaders) na wa sehemu ambazo hata kwenye ramani ni vigumu kuziona wanazidi kuongoza kuchochea mabadiliko.

  Umebakia mwezi kama mmoja tu kabla ya kikao cha Bajeti hakijaanza ambapo viongozi wa kitaifa wengi watakuwa wamebanwa Dodoma; je nini kitaendelea wakati huo? Najiuliza mwamko huu yaweza kuwa umetangulia mwendo wa viongozi wa kitaifa - yaani wananchi wameamka na wanatangulia wao kuleta mabadiliko?

  Swali la msingi ambalo linahitaji fikara zaidi ni ninihutokea baada ya maandamano na watu kurudisha kadi na shangwe na nyimbo za kufurahia? Nini hutokea baada ya viongozi wa kitaifa kuja na kuondoka; wakifanya mikutano yenye hamasa kubwa? Nini kimetokea Kiteto, Biharamulo, Buchosa, Tarime, Mwanza, Arusha, Songea, Mbeya, Iringa, Mbozi, Magu, Kirumba, Kiwira na kwingine huko kote? Baada ya kurudisha kadi na baada ya viongozi wa kitaifa kuondoka nani anaangalia hawa ambao 'wamekata shauri' kuikataa CCM na kukubali CDM kuwa tumaini leo?

  Je CDM inayo miundo mbinu ya kutosha na ya kisasa ya kudumisha (sustain) mwamko huu kabla ya CCM hawajaanza counter attack - na kweli inakuja? Ikumbukwe kuwa baraza la mawaziri lilivyobadilishwa kimsingi limeweka makada mahiri wa chama kwenye nafasi nyeti. Ukiangalia wizara wote ambazo watu wake wamebadilishwa zote zimewekwa makada wa chama cha Mapinduzi kwa kile ambacho nakiita ni 'strategic preparation before war". Ni sawasawa na vikosi vya majeshi vinavyo amass kwenye eneo kabla ya kuleta mashambulizi.

  Ninachoweza kukiona kutoka mbali ni kujipanga huku kwa vikosi vya CCM chini ya makamanda wapya na watakapoanza kurudisha majibu kuna watakutwa off guard. Mabadiliko ya Sektretariati ya CCM yanayotarajiwa kuja wiki ijayo utakuwa ni mwendelezo ya kujipanga huku na CDM kama wasipoangalia watajikuta wanajibu (react) na kulazimishwa kwenda kwenye kujitetea (defensive positions).

  CCM watakapoanza kujibu mashambulizi hakutakuwa na huruma; hata mtandao wetu huu wa JF na mfumo wake wa kufanya kazi utakiona cha moto kwani watawala hawatoacha waende kwenye uchaguzi mwingine mkuu mitandao kama hii ikiwa kama ilivyokuwa kabla ya 2010. Hili nina UHAKIKA nalo wa kutosha. CDM ikitegemea nguvu ya wananchi tu kuisukuma inaweza - isipoangalia - kujikuta ikiwa imebanwa katika kuzunguka 'mlima huu'.


  CDM ifanye nini basi? au isubiri liwalo na liwe kwa sababu 'wananchi wanaipenda'?
   
 2. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2012
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Hali ngumu ya maisha inayowakabili wananchi (inazidi kuwa ngumu na sioni ikibadilika chini ya serikali hii) ndio itakayowafanya CDM kukubalika zaidi na zaidi. Mabadiliko yanayotarajiwa ndani ya ccm ni ya kimtandao na sioni jinsi yatavyo yaondoa makundi yaliyomo ndani ya ccm (na hili la kuwepo makundi ndani ya ccm hata wenyewe wanakiri). Labda CDM wenyewe wafanye mambo ya kipuuzi kupindukia, lakini wakiendelea kuwa makini sioni jinsi watakavyo kuwa nje ya serikali 2015.
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  May 11, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mzee Mwanakijiji,
  Huu ni wakati mgumu sana kwa CCM hasa baada ya wananchi wenyewe kuchukua hatua, na kutoa maamuzi yao wenyewe kuhusiana na imani yao kichama. Nguvu hii haiwezi kuzuiawa kwa ukubwa wa chama ama serikali maana ni kama wimbi la Tsunami linapoikumba nchi kavu. CCM wanachoweza kufanya leo hii ni kukimbilia juu mlimani kuhakikisha kwanza usalama wao, Tsunami hii inapita kisha wapime maafa yake. Kujipanga wakati wa harakati hizi zinaendelea kutawaumiza zaidi pengine hata kuongeza hesabu ya majeruhi.

  Kama JK alivyosema Wadanganyika ni watu wa kusahau na kusamehe, hili halina Ubishi, wimbo hili litapita na wala sii kwa sababu ya Chadema isipokuwa sababu inatoka ndani ya chama CCM chenyewe kama wataweza yaliyowashinda kiroho. Makosa makubwa waliyoyafanya CCM ni pale walipotangaza kujivua Gamba kwa viongozi mafisadi wakashindwa kutimiza hayo kutokana na nguvu kubwa ya magamba wenyewe, na hivyo kuachia mwanya kwa Chadema kufanya counter attack ya kuijivua Gamba na kuvaa Gwanda.

  Hivyo basi ukitazama wanaojivua gamba toka CCM ni wananchi walio chini, hawana nguvu kubwa kiutawala yaani ni wale ambao hata Ufisadi wenyewe hawakuwa nao na pia wala sii kati ya magamba bali washabiki ambao ndio nguzo ya chama hicho ktk sanduku la kura. Hawa ndio wanyonge na ndio Umma wenyewe wa Watanzania. Waswahili wanasema ukikosa la Mama basi hata la Punda, kwa maneno haya nasema wananchi hawatoki CCM kwa sababu Chadema ni chama bora zaidi isipokuwa CCM imewatupa na Chadema ni chama kinachotetea wanyonge hivyo kuifanya siasa ya Tanzania ni baina ya Wanyonge na Matajiri.

  Chadema hawana lazima ya kufanya chochote zaidi ya kuendelea kuwashawishi wananchi tofauti baina ya Magamba (Matajiri) na Magwanda (Wanyonge) na kujinafsibisha wao wenyewe wana belong upande gani..CDM haitachukua nguvu zaidi kuendelea kuwashawishi wananchi nani mwenye kusimamia maslahi yao maana wao wenyewe wanajua umaskini wao wa hali na mali ndio chimbuko la kukikataa chama hiki.. Maadam hesabu kubwa ya wananchi leo hii ni maskini, wanyonge, maisha yamezidi kuwa magumu basi hata sera na mikakati ya kisiasa haziwezi kuwasaidia kitu ikiwa madai yao ni kuweka chakula mezani. Chadema itaendelea kuwazoa wananchi maskini hadi pale CCM itakapo gundua kwamba Matajiri hawawezi jenga nguvu ya Umma ktk nchi maskini.
   
 4. m

  manucho JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Hamna strategic plan wala counter attack hapa tena.
   
 5. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #5
  May 11, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mzee Mwanakijiji nakubaliana na wewe kwa asilimia 100, kinachoonekana CDM haikutegemea kupokea wanachama wengi kiasi hiki. Lakini cha ajabu hatuoni mikakati inayofanyika ya kuwalea, kupokea ni rahisi lakini kuendelea kuwatunza ni kazi. Kila leo tunasikia mikutano ikifanyika lakini hatujasikia hata siku moja ufunguzi wa ofisi kubwa angalau ya Mkoa achilia mbali ofisi za wilaya. Wanachama bila ofisi ni kujidanganya. Ukipata muda pitia thread yangu hii ambayo maudhui yake hayatofautiani sana na yako.

  CHADEMA haijajiandaa kuunda serikali

  Baada ya serikali ya CCM kupoteza imani kwa wananchi Chadema kimeonekana kuwa kimbilio la mwisho kwa wanyonge na wasio wanyonge. Kwa sababu hiyo lazima CDM kitapata wanachama wapya wengi, lakini pamoja na hayo sioni kama CDM kimejiandaa au kinajiandaa kwa ujio huo.

  Najua CCM kwa vile wana serikali ina vitengo vingi na uwezo mkubwa hata wa kuwaahidi wanachama wake u-DC nk kitu ambacho CDM hawana. Lakini tunajua CDM ina taasisi yenye muundo wa serikali (serikali ya majimbo), ina vitengo vyake na idara zake kuanzia wilayani, majimboni, mikoani, hadi taifa, kwa hiyo kwa vyovyote vile haiwezi kushidwa kuwa accomodate wageni hasa wanaokuja tayari na CV zao mkononi kama kina Millya.

  Lakini cha kujiuliza, CDM kama taasisi, viongozi wa wilaya wako wapi, viongozi wa mikoa ni akina nani, je, sera ya majimbo inaongozwa kwa organs na structure zipi mbona hazijulikani? Chama kama taasisi hakiwezi kukamilika kama hivi vyombo viko dormant vikisubiri ujio wa mtu mmoja (Slaa) kufanya mkutano wa hadhara na kuondoka. Hivi leo nikienda Masasi kwa mfano nimuulize m/kiti wa tawi anaweza kumjua kiongozi wake wa jimbo ni nani? Kama hamjui je CDM wanatekelezaje kwa vitendo sera yao ya serikali za majimbo, au iko vitabuni tu?

  What I'm trying to advocate here is that, CDM kipanue wigo wa utawala wake isijibane sana makao makuu, i-practice kwa vitendo sera yake ya majimbo wananchi waanze kuizoea. Hawa wanachama wapya wanaokuja waungane na viongozi wenyeji (of course baada ya kuwa-screened) wagawane hayo majimbo, wajitanabahishe huko kiasi kwamba tukisema jimbo la kanda ya Ziwa kwa mfano tujue nani atakuwa answerable kusimamia uhai wa chama kwa kuanzisha matawi, kuingiza wanachama, kuanzisha miradi n.k. Nafikiri huo ndio mfano mzuri kwa chama kinachojiandaa kushika dola.

  Chama hakiongozwi kwa kutegemea head office (ikulu), head office inachotakiwa ni kutoa directives, highest decision-making na support lakini day-to-day activities zinafanywa na organs zilizo chini yake, lakini kwa CDM the opposite is true, chama ni Mbowe, Slaa, Zitto basi, wanaonekana kana kwamba wao ndio wanaopokea directives na wao ndio wanafanya day-to-day activities.

  Chama kinaonekana kama kimepwaya kipo makao makuu na kwa wananchi lakini hapa katikati hakuna kiungo kabisa, wanachama wanaelea elea tu hakuna wa kuwa handle kiasi kwamba siku yeyote wanaweza ku-deflect. Kama bado unapanda majukwaani kuomba watu wajiunge wakati hujajiandaa kuwa accomodate ni uzembe na upungufu wa strategies. Inauma sana chama kama kinapata nguvukazi na kushindwa kuitumia.

  CDM wasiishie tu kumfanyia tafrija kubwa Millya na wengine watakaojiunga, wajiandande ni vipi wanatumia hizo nguvu mpya zinazoingia kuimarisha chama na kuandaa makada wake tayari kwa kuongoza serikali. Lakini kama chama kitaendelea kutegemea head office tutarudi kule kule kwa Pinda kutokuwa na uwezo wa maamuzi hadi amsubiri rais arudi toka ziarani.

  Luteni. ​
   
 6. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #6
  May 11, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  CDM should take in Topsail.

  Tend to the Wananchi whistle.

  Blow till thou burst thy wind, if room enough!!

  An lastly, shud amass all the kamandas in the front line come the 7th august parliament..
   
 7. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #7
  May 11, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Ili Jambo lolote lifanikiwe ktk dunia hii linahitaji NIA,SABABU na UWEZO.Hivi unafikiri Chadema ilipendwa na wananchi hivi hivi bila haya mambo matatu niliyoyaainisha hapo juu?Chadema wanayo nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi,sababu wanazo na uwezo pia wanao.Ni nani Leo hii angedhani kuwa chama hichi kingekuja kukubalika na wananchi Kama inavyoonekana sasa?Chama chochote cha siasa chenye nia ya kweli ya kuwatumikia wananchi ni lazima kiwe na mipango endelevu,wananchi waliopoteza matumaini ambao ni wengi ndio hao hao unaowaona wanajiunga na harakati hizi za ukombozi wa kweli(Chadema).Kuichukia au kuipenda ccm kuna sababu zake vivyo hivyo kuichukia Chadema au kuipenda(kuikubali)sababu zipo pia.
   
 8. M

  Mkandara Verified User

  #8
  May 11, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  @Luteni mkuu wangu a true revolutionist.. sidhani kama wewe ni revolutionist kutokana na chama bali imani yako wewe ndio inakuongoza. Na ndivyo hali ya wananchi wengi sasa hivi wanayataka mapinduzi kwa udi na Uvumba hivyo haijalishi kama Chadema wako tayari au laa maana sasa hivi ni kazi yao wenyewe wananchi. Chadema imechukua nafasi baada ya kujikita zaidi kuijenga dhana hiyo ya mageuzi hivyo Chadema ni chombo tu kinachotumiwa kuwawakilisha..

  Ikiwa JK ameweza kulitangaza baraza la mawaziri mara tatu na katika hao nusu yake ni watu wa kawaida kabisa itakuwaje watu washindwe kuelewa kwamba Chadema haina mtihani mkubwa ktk maandalizi maana ni wanyonge sio wajinga ndio wanajiunga na chama hicho. Zaidi ya hapo wenye NIA, SABABU na UWEZO wa kukiondoa chama CCM madarakani ni wananchi wenyewe sio swala la Chadema tena sasa hivi na wale wenye kutafuta madaraka watajipanga.
  Na muhimu kuliko yote, sii kweli kwamba matajiri ndio waliosoma ama wenye elimu na uwezo wa kuongoza nchi kwa sababu tu walifanikiwa ktk kuiba ama ufisadi bali kati ya hawa wanyonge wanaojiunga Chadema leo wamo wasomi wazuri sana na kikubwa zaidi wamechagua Uzalendo kutangulia maslahi yao binafsi - hii ndio advantage ya Chadema sasa hivi. Chadema ni chama na chama ni WATU hivyo, CDM inaendelea kuzoa wananchi wenye kila aina ya sifa, ujuzi na uzalendo na haya ndio maandalizi yenyewe. Arab spring imetokana na WATU kuchoka wenyewe na vyama vimejihusisha tu na harakati hizo leo hii vyama ambavyo havikuwa na nguvu kabisa ktk nchi hizo ndio wamejizolea kura bungeni na wanaongoa nchi zao (Tunisia na Misri).
   
 9. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #9
  May 11, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Utazamisho wako ni mzuri ingawaje ungeingia ndani kupima mikakati ya hivi vyama viwili.

  CCM wanasumbuliwa na maadui wengi, baadhi ya watano ni:-

  1. UFISADI si wa mali tu bali na wa akili, wanafanya hila kwenye kila jambo kwa imani kuwa hawaonekani, mfano ubadhilifu serikalini, chaguzi zote, kuingilia mahakama (hoping bunge linajinasua). Kama mla nyama ya watu hawana uwezo wakujitenga na ufisadi

  2. Imejijengea maadui kati ya wananchi kwa kulinganisha ahadi na delivery, maadui wabaya zaidi ni wenyewe kwa wenyewe katika kugombania ngawira za ufisadi. Kwa hiyo watasalitiana tu.

  3. Mkakati wa kusubiri kufanya counter attack unasutwa na reality on the ground. Kwa kawaida counter attack inafanikiwa kwa kutumia a weak defence base and drilled tactics, lakini pia na mbinu za mashambulizi yenyewe. CCM wanategemea makosa ya CDM ambayo makosa ya CDM machoni pa wananchi wengi ni consolation wanayoitafuta kama majibu mbadala ya tabu zao ambazo hazina majibu toka kwa watawala. Ulinzi wa CDM unatoka na nguvu yao ya mashambulizi ambayo yamefanikiwa kuwachosha CCM hadi wanaonekana wasanii kwa jitihada zo zote wanazofanya.

  4. Hawana rasilmali watu wanaoamini itikadi ya CCM; ushahidi ni mashindano ya ufisadi ndani ya chama chao, pia watu waadilifu ndania ya chama kupuuzwa kwa kauli na matendo.

  5. Hawana mkakati wa kutafsiri uchumi kwa wananchi wa kawaida; kinachoonekana ni tofauti ya kiuchumi kati ya wao na wananchi; mwangalie Nape kwa kipindi kifupi alivyopendeza.

  Walichobakia nacho ni historia ya akina Nyerere, akina Sokoine na mtandao wa chama ambao hauna mwongozo. Akina Nyerere na falsafa zao hawakupata fursa za kusahihisha failures zao, kwa hiyo ni mtaji mufilisi

  CDM wana adui mmoja tu naye ni dola kuwa tawi la CCM, wanalijua na wanakabiliana nalo kwa gharama

  CDM wana mapungufu

  1. Chama kinapanuka haraka kuliko rasilimali walizo nazo (nakubaliana na wewe). Wanataka kuhamishia chama kwa wananchi wanaojua au waliojua chama kimoja cha mapinduzi. Wananchi ambao msingi wa elimu yao ya uraia ni ile ya ndiyo mzee, na uchumi wa kaya duni (njaa)

  2. Vijana na viongozi wengi hawana uzoefu wa kuwabana na kuwakaba CCM kidiplomasia mbele ya wananchi. Wanaingizwa kwenye kusingiziwa kashfa kwa mkakati wao.

  3. Hawana rasilimali za kutosha za kuwajengea uwezo makada na viongozi wa ngazi zote kwa kuwaimarisha kudeliver na kusimamia kinachotakiwa na wananchi na baadae dola.

  4. Kwa kiasi cha vijana wazuri waliopo sina uhakika wa succssesion plan ya uongozi wao wa juu hapo baadae.

  Nguvu yao kubwa ni kuaminiwa na umma angalau kwa sasa hata kama CCM watazinduka kufanya Counter Attack.

  Sustainability kwa mikakati ya vyama vyote itategemea wananchi wanaelimika kiasi gani kudai haki zao na kukiamini chama kimojawapo. NAAMINI COUNTER ATTACK YA CCM IKO "FOILED" NA NGUVU YA UMMA KULIKO CDM KWA MIAKA MITANO IJAYO
   
 10. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Tathimini yako ni sahihi...CHADEMA hawana "Proper flow of Managerial Netwerk".....mshikamano wa kiungozi upo juu ktk ngazi ya Taifa na Mkoa..ukishuka chinì hakuna netwerk nzuri..waliopo Wilayani,Tarafani,kata,kijiji,kitongoji na ktk kaya wanajiongoza wenyewe,hawana muunganiko na Mkoa wala Taifa...wanahamasika bila kuwa na muongozo!at the end of the Day wanabaki kama makinda ndani ya kiota bila Mama Mlishi. Tembelea vijijini watu wamehamasika sana,wanataka mabadiliko kwa ghalama ya hamasa na kauli za viongoz wa kitaifa,wala si pesa na khanga,wanahitaji miongozo ya kimuundo na kimkakati toka Mkoa na Taifa lakin hawapati...faida iliyo mikononi mwa Chadema ni kuwa watu wanataka changes...maisha ni magumu na wanahisi mbadala wao ni Chadema,pia kuna Taifa lipo ktk mabadiliko ya kizazi(Generation transional)...wengi ni walozaliwa wakati au baada ya Uhuru..wanahisi kizaz chao kinahitaji kujiongoza bila msbda wa wapgania Uhuru,wanapenda kuona upya wenye upya wa kiutawala....haya yote ndo yanaleta hamasa híi ya kimacdiliko,na ndo advantage ya Chadema'lakini chadema kama chama hajijawa na mpango mkakati wa Taifa mpaka kaya!ndo mana maelfu wanaohama CCM wanaishia ktk shamrashamra za viwanjani ktk kurudisha kadi,bbda ya hapo wanabaki bila muongozo kama Makinda ndani ya kiota bila mtetea!.'wajipange,wawe na mfumo wa Taifa hadi kata.'.bbdae itakuwa kama soko la bongo...i.e Simba na Yanga....Kajumulo,Mtibwa,Pan-Afriican,Mseto,Nyota Nyekundu zilikuja zikawika kwa msimu,zikapata watu wenye hamasa wasio ratibiwa..mwishowe zikapotea,.lakn Simba na Yanga zinadumu ktk mioyo ya watu japo zinaendeshwa kisanii, mana hata izo Pan Afrikan ni uzao wa Simba/Yanga......CCM itaenflea kutawala kimachalemachale kama Chadema haitabadili mtindo wake na kusuka mfumo wa kiutawala unaowaunganisha viongozi wa Taifa hadi kata!.....I STAND TO BE CORRECTED
   
 11. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #11
  May 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Wakuu

  Hii inaweza kuwa moja ya topic nzuri kabisa. Kitu kimoja muhimu ambacho tunapaswa kujua ni kwamba mambo haya pia hayatokei kwa bahati mbaya. Yanatokea kwa sababu kuna kazi imefanywa na inaendelea kufanywa kwa umakini na watu makini. Kazi hii haifanywi na viongozi tu, wengi wenu hapa pia mnahusika kwa namna moja ama nyingine katika kufanikisha matunda ya struggle hii kufanikiwa, hasa katika kuiondoa CCM.

  Mikakati ya CCM kutaka kuendelea kubaki madarakani, by any means necessary inafahamika. Lakini kazi makini niliyosema inafanyika kufanikisha struggle hii, hata kufikia wananchi wanaasi CCM mchana pia inafanya kazi ya kuangalia na kumjua adui mapema kabla hata hajachukua hatua ya kujibu mapigo.

  Kila hatua inayopigwa na CHADEMA katika struggle hii mbali ya kutuma salaam za kishindo kwa watawala, pia zinapeleka maumivu makali SANA kwa CCM na watawala, hivyo kama chama makini, lazima kiwe makini mithili ya mwindaji anayejua nini cha kufanya baada ya kumjeruhi kifaru.

  Mikakati ya CCM, kujibadilisha badilisha, haijaaanza leo na inayofanyika leo inajulikana si ile itakayofanyika kesho. Kitu cha msingi ni kujua madhara na matokeo yake kila mara tu inapokuwa inafikiriwa au inapokuwa mezani tayari kwa utekelezaji...na kikubwa zaidi ni kujenga uwezo wa kuzikabili na kuziharibu. This is a war. Hakuna asiyejua hivyo, unless si mpiganaji mahiri.

  Ninachokiona katika maandishi ya baadhi ya watu, pamoja na kwamba wanaweza kuwa wanatoa precautions ni kuanza kuwa watabiri. Wanatabiri kuwa CHADEMA kimekaa tu na kuangalia haya yakitokea "kwa bahati mbaya".

  Kwamba wapiganaji wako vitani, wameshamjeruhi adui vya kutosha, wanazidi kusonga mbele, lakini eti hawajui hatua ya pili wanapaswa kumpiga wapi na wapi adui huyo na kutompatia kabisa nafasi ya kujitibu kiasi cha kurudi na nguvu zote, hii si kweli wakuu.

  Unaposikia na kuona leo wanachama maelefu wamejiunga Kagera, Ngara si bahati mbaya, kuna watu wako field, yuko Wilfred Mganyizi Lwakatare pale na Mama Congesta Lwamlaza, mama mpambanaji mahiri kabisa kwenye mageuzi kwa miaka 20 sasa.

  Suala la new thinking how to move the struggle and how to move on with the struggle kwa kila hatua inayopigwa linafanyiwa kazi kila kunapokucha. Mambo hayawezi kubadilika kila siku kisha chama makini ambacho kinajua na kutambua kuwa ndiyo TUMAINI PEKEE la Watanzania, kibaki vile vile, kiutendaji, kimikakati, kioganaizesheni, mipango ya muda mfupi, kati na muda mrefu na kuchukua hatua, kilivyokuwa juzi. No!

  Kazi inafanyika, tena ile dhana ya hakuna kulala inafanya kazi kweli kweli siku hizi, kwa sababu nadharia ya falsafa ya nguvu ya umma sasa iko matendoni kwa kasi. Ni principle iliyo ya kawaida kabisa katika uchumi, kuwa mzalishaji makini anapaswa kuwa na projection ya namna ya kuzalisha, hasa kuongeza wingi na ubora wa bidhaa pale ambapo mahitaji yanaongezeka sokoni, wakati huo huo kuwajua washindani (wapinzani) wake, uwezo wao na n.k.

  Kusisitiza tu tena; umakini ule ule unaosukuma wimbi hili ambalo kila mtu sasa analisikia na kuliona kwa wazi, kwamba Watanzania sasa wanaamua kuonesha UASI kwa CCM waziwazi, ndiyo utakaoendelea kunolewa kwa ajili ya kujua nini kinafuata katika mapambano haya. Hii ni vita. Si lelemama hivi. Wapambanaji wako alarmed. Twendeni sote sasa...tukalikomboe taifa.

  Maadui wetu wanajulikana. Sasa wamefikia wanne, ujinga, maradhi, umaskini na CCM.
   
 12. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,717
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  Kuchukua tahadhari ni muhimu na i wish ningejua CDM wamejiandaa vipi na kuweza ku-sustain hili wimbi.

  Lakini nikubaliane na mmoja wa wasemaji hapo juu:

  1.CDM waendelee kupiga amsha amsha kama ambavyo kwa muda wamekuwa wakifanya ili wananchi wajue kuwa kuna maisha nje ya CCM na hakuna lisilowezekana kama watakuwa tayari kwa mabadiliko

  2.Ilivyo maisha yanazidi kuwa tight...pamoja na CCM kuweka strategic people katika sehemu nyeti..nadhani wamechelewa, wamekumbuka shuka kumekucha. ubaguzi wa kimakundi na jinamizi la ufisadi vimewatafuna sana na kwa muda mrefu, wakati hauko upande wao, they are bound to loose, its inevitable.

  3.CCM wanaweza kuanzisha counter attack lakini haitoweza kufanikiwa..wameoza mno, na harufu kali ya uvundo inatoka katika miili yao kiasi kwamba si siri tena. namna pekee ya wao kufanikiwa ni kujivua gamba kikweli kweli na si kisanii kama hivi walivyofanya na baraza la mawaziri.

  tunataka kuona yafuatayo kwa mfano:
  1.mawaziri wezi ambao mbunge Filikunjombe aliwashutumu pale mjengoni na akasema ushahidi upo wakifungwa jela
  2.kesi za ufisadi mfano wa EPA...akina JEETU PATEL, KAGODA wameishia wapi? kesi ziishe na wezi waende segerea
  3.MRAMBA, YONA NA MGONJA..kesi yao vipi? hatuisikii tena....hawa waende jela
  4...na mengineyo mengi na la karibuni kabisa ni ahadi ya RAIS kuwa kila mkuu aliyesaidia wizara kufanya madudu kiasi cha waziri kulazimika kuwajibishwa naye anawajibika.

  Mkuu Mwanakijiji, ukitazama hiyo orodha hapo juu kwa uchache...unahitaji total overhaul of the system..hicho ni kitu ambacho CCM hawawezi kukifanya, yao ni FUNIKA KOMBE basi....na hilo KOMBE bahati mbaya sana CAG kalifunua tena kwa msaada wa RAIS kutoka CCM yenyewe...ntaeleza.

  Kwa wale wanaoweza kusoma financials and audit reports na ni wasomaji wazuri wa magazeti, wanafahamu kuwa kwa miaka kadhaa tangu JK aingie madarakani, aliruhusu hizi Audit Reports za CAG ziwe published. Hapo ndipo tulipoanza kupata ushahidi wa kuwa mchwa ni wengi kwa kiwango cha kutisha ndani ya system. Thanks to him mwaka huu amekwenda step moja mbele kwa kuruhusu report hiyo ikasomwe bungeni(sifahamu kama iliwahi kusomwa bungeni katika wakati wowote wa historia ya tanganyika huru)....asante rais wangu kwa hilo.

  Suala linarudi je, CCM inao ubavu wa kufanya hiyo overhaul???? SIDHANI.

  ...Am sorry to say kwa hao makada wa CCM, wamechagua kushindwa, maandishi yapo ukutani yanasomeka...SAA YA UKOMBOZI NI SASA.
   
 13. MWANA WA UFALME

  MWANA WA UFALME JF-Expert Member

  #13
  May 11, 2012
  Joined: Sep 10, 2010
  Messages: 578
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wimbi hili la kuikataa ccm na kwenda chadema ni kama tu uzi uliokuwa umening'inia na ulikuwa unasubiri tu kusukumwa kidogo.

  Strategic positioning ya CDM inahitajika katika kusustain grassroots structures na kujijengea wigo wa nguvu.

  Siamini kuwa kubadilishwa kwa uongozi wa ccm, iwe ni mawaziri au wakuu wa wilaya kunaweza kuleta mabadiliko yoyote kwa ccm maana watu ndio hawataki kuwasikia.

  Kama ni reactive moves, tungezitegemea tokea wabadilishe uongozi wao wa juu wa chama ambapo kina nape, na wengine walijiunga. That was a moment that a core change for ccm was expected.

  Chochote ambacho kinaweza kubadilisha nguvu ya ccm kwenye uwanja wa siasa kwa sasa ni kugusa maswala ya msingi ambayo wananchi wamekuwa wakiahidiwa kila kukicha.

  Wakati umaskini unazidi kuongezeka kwa kasi na wimbi la inflation kubaki juu, huduma mbovu za afya, maji, elimu nk. vikizidi kuzorota, kasi yeyote ya kuweka uongozi mpya haiwezi kuwa na faida kama mabadiliko ya haya hayagusi maswala msingi kwa wanachi.

  So far ni wakati wa CDM kutumia hii prolonged loophole ambayo kuzibika sio leo, kwa kuimarisha mizizi both psychologically and structurewise.
   
 14. mlaizer

  mlaizer JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 234
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  well said,nadhani ni muda muafaka kwa CDM kujipanga ili kuweka utaratibu wa kuwa-maintain hawa wanachama kwani ongezeko hili la wanachama ni kubwa sana kwa kuendelea kutegemea kila kitu kutoka makao makuu.
   
 15. F

  FJM JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Kuna mambo kama manne hivi CDM wanatakiwa wazingatie.

  1. Screening and orientation: Kwa sasa wananchi wameanza kuamini Tanzania bila CCM inawezekana. Na kubwa zaidi waonaona CDM kama chombo kinachoweza kuwavusha salama kutoka kwenye dimbwi la hali mbaya ya maisha. CDM wanatakiwa waanzishe kitengo cha kuchuja na kutoa orientation ili kwanza kujua nia na dhamira ya wanaoingia (hasa viongozi wanaohamia CDM toka vyama vingine) na pia kujiridhisha kwamba kweli hawa watu wako compatible na mission/vision ya CDM. Kitengo hiki kiwe makini ili kuhakikisha only samaki ambao wanaweza kukunjika ndio wanakaribishwa.

  2. Jambo moja kubwa lililoiuwa CCM ni uchu wa madaraka. Watu wanataka madaraka kwa udi na uvumba (pengine kwa maslahi binafsi) na pale wanapokosa inakuwa mgogoro. CDM wa-rewind hii movie ya CCM ili waone vizuri mtafaruku ulianzia wapi na ni wapi walikosea. Then wao CDM sasa waweke 'framework' itakayowasaidia kupata viongozi bila mizengwe lakini pia itambue' personal ambition' za wanachama wake.

  3. Maamuzi magumu vs uwajibikaji: Tuliona matokeo ya maamuzi magumu ya CDM dhidi ya madiwani wakorofi kule Arusha. Watu walitulia i.e Shibuda! Miiko ya uongozi ni muhimu sana na kila mtu aliye kwenye nafasi ya uongozi anatakiwa atambue hilo. Na pale kiongozi anapokwenda kinyume na miiko na maadili ya kiungozi basi kusiwepo na sinema za kimagamba. Maamuzi yafanyike pale pale. Lazima kila mmoja akumbushwe kuwa cheo ni dhamana.

  4. Monitoring & Evaluation: Sambamba na No 1, CDM wawe na in-house team ya watu makini watakao kuwa wanafuatilia 1) muitikio wa chama, 2) loyalty pendulum/public mood hasa kwenye strategic areas (nadhani wanazijua).
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  May 11, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Michango yenu inanipa matumaini...
   
 17. F

  FJM JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  TUMAINI, nimekusoma. Lakini pia ningejikita zaidi kwenye kupea 'upako' kuliko kutoa 'ushuhuda'- if you know what I mean!

  Sentence ya mwisho - imekaa vizuri. Na hiyo iwe ndiyo mission ya CDM
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #18
  May 11, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Yeah! For sure unapaswa kusahihishwa kama ambavyo tayari umejiweka tayari. Wakati mwingine wengi wa watu wanaopenda mabadiliko pale wanapolazimika kuzungumzia network ya CHADEMA hasa katika ngazi ya chini wamekuwa ama kwa bahati mbaya au kwa makusudi wana-succumb kwenye propaganda za CCM.

  Utasikia; chama hiki kipo ngazi ya taifa tu...mara kiko mijini tu...hakiko vijijini. Mara nendeni vijijini sasa mjini wameshaelewa. Huu si uhalisia wa mambo. Wakati mwingine notion kama hizi zimetumika sana kutaka kuhalalisha wizi na hujuma za CCM wanazofanya kwa mgongo wa 'vijijini...tunasubiri maboksi ya vijijini'.

  Ukweli ni kwamba mtandao wa CHADEMA kwa sasa si wa kubeza tena. Hata 'wenyewe' wanajua. Mathalani; juzi katika uchaguzi wa Arumeru Mashariki mnajua kitu kilichokuwa kuwashtua CCM na kuanza kupiga watu wetu vijijini na kuwamwagia tindikali. Ilikuwa ni baada ya kutahamaki kuwa tumeshajikita vya kutosha vijijini kabla yao. Hivyo tutakavyorudi mjini (maeneo ya kujidai) tunakuja kumaliza mchezo. Wakapatwa na kiharusi. Too late. Yaliyobaki ni hadithi.

  Lakini hayo tisa, kumi ni kwamba kwa kiasi kikubwa sana ushindi wa juzi wa Arumeru Mashariki wenyeji ndiyo waliohusika mwanzo hadi mwisho kwa asilimia mia. Namaanisha viongozi wa misingi, matawi, vitongoji, vijiji na kata katika maeneo husika. Kazi hiyo ya kuwahamasisha wanakijiji, kuwafanya wanachama watiifu chini wanaoratibiwa, isingewezekana kama hakuna uongozi ngazi ya chini.

  Wanatambua namna ambavyo kwa muda wa miaka 20, chama hiki kimezidi kukomaa na kujieneza, kikitumia kikamilifu kabisa kila fursa ambayo imepatikana ndani ya miaka hiyo, katika kila aina ya forum.

  Mnahitajika ku-qualify statements zenu hapa mnaposema kuwa wale wanaopokelewa baada ya kuhamasika kisha kujiunga kuwa wanachama wanabaki kama makinda bila mwongozo, toeni mifano, wekeni picha ziseme (simaanishi picha halisi) ili tuone uhalisia wa hoja zenu. Maana kama mnafuatilia baadhi ya maeneo uhamasishaji umefanywa na viongozi wa ngazi za chini kabisa bila kuwepo viongozi wa kitaifa.
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  May 11, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Tumaini, Arumeru mashariki ni mfano wa hali ilivyowilaya zote nchini au inawakilisha kama asilimia ngapi ya hali ilivyo?
   
 20. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #20
  May 11, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kaka mm nikubaliane na wewe kwa kiasi na nitofautiane na wewe kwa kiasi vilevile.nakubaliana na wewe kuwa chadema wanashindwa kukabiliana na wimbi kubwa la wanaokimbilia kwao na sababu za kuona kama wanashindwa ni kwa sababu bado tunaamini katika mtindo wa kikoloni wa kutawala.kuna wanaosema chadema hawana nguvu ya kutosha kukamata dola,hii ni kwa sababu ya kulemazwa na mtindo wa ccm wa chama kushika hatamu hata ndani ya mfumo wa vyama vingi.
  rais anakuwa mfalme anateua kila mtu katika uongozi hapo ndipo tulipokwama kitaifa na ndipo tulipokwama ki fikra ndo maana kuna wanaoufikiria mfumo huo wanajiuliza chadema watapata wapi wakuu wa wilaya 150,mkoa,30,wakurugenzi150,makatibu tawala mikoa30,mawaziri 60,makamanda wa poli 40,tss,afisa magereza,rpcs,igp,jaji mkuu na majaji,makatibu wakuu 30,wakurugenzi wa mashirika nk.
  huo ni mfumo chadema wanaukataa na baada ya katiba mpya nafasi zote zitakuwa ninatangazwa watu waombe kazi,wafanye usaili hapo utagundua kazi ya uongozi(si utawala)itakuwa rahisi.

  nikukatalie kuwa ccm haiwezi kubadilika.kila siku wanapanga hila dhidi ya watanzania na wapinzani.kujibu mashambulizi wanaweza kwa wapinzani na si kwa wananchi,wananchi wanataka maisha bora wameshajua nchi yao ni tajiri wameshajua rasilimali zao zinatumiwa vibaya na watawala ccm.
  kujibu mashambulizi ambayo wananchi watayakubali ni kufanya yafuatayo;
  1.kuwakamata wote waliohusika na kila aina ya wizi meremeta,kiwira,richmond,kapunga,nyumba za serikali,trl,ttcl,trl,atc,bandari,viwanda vyote,nbc,sukita,nk.
  2.kuyashitaki mashirika yote yanayokwepa kodi ambayo yanamilikiwa na viongozi.
  3.kuwakamata wote waliouza vitalu na kuruhusu wanyama hai kusafirishwa nje.
  4.kuifuta takukuru.
  5.kuwafukuza nchini wanaoiba madini yetu.
  6.kima cha chini kufikia 350000(pamoja na kuwa kimepitwa na wakati)
  7.kuwalipa wastaafu wa ea pamoja na waalimu madai yao.
  8.kuimarisha tra na kubuni vyanzo vipya vya mapato.
  9.kupunguza matumizi ya serikali.
  10.kuyarudisha mashirika roho ya taifa na kuyapa ruzuku ya kuyawezesha kujiendesha kiushindani ATC,TRL,BANDARI,NAFCO,KIWIRA,TANCUT ALMASI,TTCL NK.
  11.kupunguza ukubwa wa serikali na kuondoa viongozi mizigo kwa taifa nk.

  hayo yakifanyika ndani ya ccm si tu kuwa wanaichi watarudi ccm bali hata dr slaa na mbowe wanarudi ccm.
  mimi sikuondoka ccm kwa sababu ya jina la ccm wala sipo upinzani kwa sababu ni mpenzi wa kupinga kila kitu.
  CCM WAKIWEZA KUFANYA HAYO WANILETEE KADI 10,000 NITAZISAMBAZA KWA WANACHAMA WA CHADEMA NCHI NZIMA KWA GARAMA YANGU.
   
Loading...