Mwamko wa kisiasa nchini

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,633
11,577
Mabibi na Mabwana najitokeza kuuliza swali ambalo nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara kuhusu mustakabali wa nchi yangu Kisiasa hususani kwa wananchi waishio Vijijini ambako upatikanaji wa taarifa ni adimu.

Ukweli ni kuwa Tanzania inahitaji mapinduzi makubwa sana kisiasa ili kuweza kujenga jamii yenye maendeleo hasa kutokana na mauzauza ya Ufisadi yaliyoanza kufichuka na yanayoendelea kufichuka. Lakini je, Watanzania wote wana mwamko kuhusu hali nzima ya nchi yetu na ubabaishaji wa viongozi wetu waliopo madarakani? Je wale waliopo vijijini ambao kuna baadhi inasemekana mpaka leo wanajua kuwa rais wa Tanzania ni Nyerere na ndiyo wanaoipatia kura CCM bila kujijua kwa kigezo kuwa 'tunampigia kura Nyerere' wana mwamko huu tulio nao wana JF?

Manake nimeona maoni yenye matumaini kutoka kwa wadau mbali mbali ndani na nje ya JF kuwa 2010 CCM (JK) itakiona cha mtema kuni, itawezekana kweli?

Wadau naomba tufumbuane macho kuhusu huu utata ili nami niweze kufahamu mikakati pamoja na maendeleo katika suala zima la kuleta mabadiliko kwenye nchi yetu.
 
Hili suala nimekuwa nikilifikiria sana. Ni kweli kuwa chama tawala sasa hivi kimevurunda sana, na kwa hali yoyote, kama hakitajirekebisha na kujisafisha, ingebidi mwaka 2010 kisishinde uchaguzi. Hata hivyo kama ulivyosema hapo juu, hali inaweza isiwe hivyo kwa kuwa wapiga kura wengi waliopo vijijini bado wanaamini CCm ile ya Nyerere na wana imani kubwa sana na chama hicho.

Mfano mzuri sana ni mfano wa Zimbabwe. Ni vigumu kuamini kuwa bado kuna wananchi wengi wamempigia kura Mugabe, pamoja na hali ya maisha kuwa ngumu na bila hata kuwa na ufumbuzi wa siku za karibuni wa hali hiyo. Bado wananchi wengi wanamuamini Mugabe kama mpigania uhuru aliyewatimua Waingereza na kuwanyang'anya ardhi. (Aliyepewa hiyo ardhi baada ya kunyang'anywa wazungu si hoja!)Vyama vya upinzani vinabadnikwa picha ya uchochezi na kuwa vibaraka wa nchi za magharibi. Nimesikia leo hii kuwa zamani, Wazimbabwe waliokuwa nje ya nchi walikuwa wanapiga simu nyumbani kuuliza hali ya hapo nyumbani. Siku hizi wakipiga simu, watu waliopo Zimbabwe wanawauliza walioko nje wawaeleze kuhusu habari za hapo Zimbabwe! Ina maana kuwa wananchi wa Zimbabwe hawajui habari kamili za hapo kwao.Hapa kuna ukosefu wa habari, au ukosefu wa habari kamili.

Ingawa Tanzania hakuna ukosefu wa habari, naweza kusema kuna ukosefu wa habari sahihi kwa wananchi. Hapa JF tutaongea mambomengi tu kuhusu nchi yetu, namna ya kujikwamua, viongozi wabovu n.k. lakini ni vigumu kwa mwananchi wa kawaida, hasa aliyeko kijijini kupata habari hizo.

Hapa nadhani ni jukumu la vyama vya upinzani, mashirika huru, na wanaharakati mbalimbali kufanya mikakati ya kuwafikishia wananchi habari sahihi kuhusu nchi yao. Wananchi wakishapata habari hizo, itawapa uwezo wa kuamua na kutenda ipasavyo pale watakapohitajika kufanya hivyo, kwa mfano katika upigaji kura.

Miaka ya nyuma kulikuwa na elimu ya watu wazima ambayo ilikuwa inaendeshwa na serikali/chama. Pamoja na kujua kusoma na kuandika, elimu ya watu wazima ilitolewa kuelimisha wananchi sera za chama na serikali. Sijui kwa wakati huu wa mfumo wa vyama vingi, elimu hiyo, hasa elimu ya uraia (civic education) inatolewa na nani, na mada yake inahusu nini?

Hapa nadhani ni jukumu la vyama vya upinzani, mashirika huru, na wanaharakati mbalimbali kufanya mikakati ya kuwafikishia wananchi habari sahihi kuhusu nchi yao. Wananchi wakishapata habari hizo, itawapa uwezo wa kuamua na kutenda ipasavyo pale watakapohitajika kufanya hivyo, kwa mfano katika upigaji kura.

Kwenye hili, wa kulaumiwa ni sisi wananchi kwamba kwa nini wananchi hawana elimu ya siasa tuliyonayo JF, sio kosa la CCM.
 
Kwenye hili, wa kulaumiwa ni sisi wananchi kwamba kwa nini wananchi hawana elimu ya siasa tuliyonayo JF, sio kosa la CCM.

FMEs Unaposema kuwa tuwalaumu wananchi kwa kutokuwa na elimu ya siasa na si CCM napata utata manake kwa mfano Mtanzania aishiye kijijini ambako hata umeme hajui ni nini, njia za mawasiliano angalau kama barabara ni duni au hazipo kabisa pamoja na ukame kumsumbua mara kwa mara; ataweza vipi basi kujua kuwa kuna kitu kinaitwa elimu ya siasa ilhali hali yake ya kimaisha inamlazimisha kujishughulisha tu na kutafuta mlo wa siku moja ilimradi siku zisogee?

Pia kama Serikali ambayo inaongozwa na CCM haitafanya jitihada za kuwafikia wananchi wote ni kwa nini basi tusiilaumu kwa kuwanyima watu hawa haki yao ya kimsingi yaani elimu hiyo ya uraia?

Hivyo basi tuwalaumu hao watu kwa kukosa ujuzi kuhusu jambo ambalo hata hawajui/hawatambui kama lipo?
 
Mabibi na Mabwana najitokeza kuuliza swali ambalo nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara kuhusu mustakabali wa nchi yangu Kisiasa hususani kwa wananchi waishio Vijijini ambako upatikanaji wa taarifa ni adimu.

Ukweli ni kuwa Tanzania inahitaji mapinduzi makubwa sana kisiasa ili kuweza kujenga jamii yenye maendeleo hasa kutokana na mauzauza ya Ufisadi yaliyoanza kufichuka na yanayoendelea kufichuka. Lakini je, Watanzania wote wana mwamko kuhusu hali nzima ya nchi yetu na ubabaishaji wa viongozi wetu waliopo madarakani? Je wale waliopo vijijini ambao kuna baadhi inasemekana mpaka leo wanajua kuwa rais wa Tanzania ni Nyerere na ndiyo wanaoipatia kura CCM bila kujijua kwa kigezo kuwa 'tunampigia kura Nyerere' wana mwamko huu tulio nao wana JF?

Manake nimeona maoni yenye matumaini kutoka kwa wadau mbali mbali ndani na nje ya JF kuwa 2010 CCM (JK) itakiona cha mtema kuni, itawezekana kweli?

Wadau naomba tufumbuane macho kuhusu huu utata ili nami niweze kufahamu mikakati pamoja na maendeleo katika suala zima la kuleta mabadiliko kwenye nchi yetu.

Na mie nifumbulie fumbo- Mwamko wa kisiasa nchini na habari adimu vijijini-Huu ni utata au?

Hiyo hapo juu bai ze wei

"Ukweli ni kuwa Tanzania inahitaji mapinduzi makubwa sana kisiasa ili kuweza kujenga jamii yenye maendeleo hasa kutokana na mauzauza ya Ufisadi yaliyoanza kufichuka na yanayoendelea kufichuka."

My take-mapinduzi ya siasa yapo na tumeendelea kuliko Nchi nyingi barani Afrika. Ukweli tunahitaji mapinduzi makubwa Kiuchumi na sio Kisiasa.

Nafikiri itakuwa sahihi kusema chimbuko la Ufisadi nchini-Ufisadi wa habari vijijini-na mwamko wa Kiuchumi na Habari Vijijini.:confused: "Mwamko wa Kisiasa" ilishapitwa na enzi

Inatisha-"Chukua Chako Mapema" ni mwamko mzuri wa kiuchumi-haina siasa sasa.:cool:
 
Mkulu Ndugu,

Heshima mbele mkuu, nimesema wakulaumiwa ni mimi na wewe, yaani wananshi wenye upeo lakini tumeshindwa kuwafikia wananchi na kuwaamsha, CCM has nothing to with that, the matter of fact wananchi wajinga ni the better kwa viongozi wabovu,

Sasa acha kulaumu everybody else, lakini sio wewe na mimi, lete mikakati ya namna tutakavyowaamsha wananchi.
 
nakubaliana na Mkuu FMES......sisi hapa JF tunafanya juhudi gani kuhakikisha hizi taarifa zinawafikia wananchi kule nyumbani/vijijini

Hili suala lilishajadiliwa sana, nakumbuka hatua kadhaa Mkuu Dua alishauri kutumia hata mitandao ya simu ambazo siku hizi zimetanda kila kona hadi vijijini.........ingawaje si vema kum-convinience mtu kwa tarifa ambazo hazitarajii.....si mbaya hata mara moja/mbili kwa mwaka inatosha.

Kulikuwa na mkakati Mkuu Invisible alituwekea hapa ili taarifa za JF ziweze kuwafikia walio wengi....nafikir zilikuwa halted kiaina.

anyway mimi wewe na yule tutumie kila aina ya uwezo wetu tuanze kuwasiliana na jamaa zetu huko vijijini.

wengi wetu hapa tuna uwezo huo na tuutumie sio kwa kueleimisha siasa tu bali hata kusaidia wanajamii wetu kielimu nk, na kuunga piamkono juhudi za maendeleo sehemu mbali mbali........na hili tutalitambua kama tukiwa tunarudi mara kwa mara nyumbani na kujionea wapi twawezakuelimisha na kusaidia.....tukisubiri vyama sijui na serikali.........kw amwendo huu tutakuwa tunasubiri kiama
 
Kijarida cha Jamboforums, kisichofungamana na chama chochote, kitakachosambazwa nchi nzima, kitakachotoa elimu ya siasa ama kwa bure au kwa bei ya chini kabisa, kitakachosambazwa nchi nzima na kuchapishwa kila baada ya wiki mbili.

Makala za uwakilishi zitaandikwa hapa, kuchujwa umakini, kupigiwa kura halafu kuchapishwa.

Funds zitatoka kwa members hapa na watutakiao mema.Tayari tuna waandishi wa habari na watu wa media wenye uzoefu na uchapishaji.Ikibidi hata kutengeneza soft copy itakayosambazwa bure kwa email kwa wawakilishi tofauti nchini kote halafu wawakilishi waweze ku print, kama wataweza kufanya huduma bure au kuuza kwa bei nafuu ili kurudisha gharama za uchapishaji yote ni sawa.

In any case Jamboforums need a newsletter, period.

Angalau na watu wa vijijini wapate mwamko wa kujua nini kinaendelea.Tunaweza kuweka habari za kisiasa, maendeleo ya bunge, wabunge na performance zao, ahadi za serikali kuu na utekelezwaji wake, data za kiuchumi nk.

Kwa sasa huu ndio mchango wangu.
 
Na mie nifumbulie fumbo- Mwamko wa kisiasa nchini na habari adimu vijijini-Huu ni utata au?

Hiyo hapo juu bai ze wei

My take-mapinduzi ya siasa yapo na tumeendelea kuliko Nchi nyingi barani Afrika. Ukweli tunahitaji mapinduzi makubwa Kiuchumi na sio Kisiasa.

Nafikiri itakuwa sahihi kusema chimbuko la Ufisadi nchini-Ufisadi wa habari vijijini-na mwamko wa Kiuchumi na Habari Vijijini.:confused: "Mwamko wa Kisiasa" ilishapitwa na enzi

Inatisha-"Chukua Chako Mapema" ni mwamko mzuri wa kiuchumi-haina siasa sasa.:cool:

Sura ya kwanza; mwamko wa kisiasa ninaouzungumzia ni ile hali ya Watanzania wote kuelewa nini kinachoendelea nchini na pia kuweza kuwa na uelewa, uchambuzi yakini na hatimaye kuwa na uwezo wa kuamua mustakabali wao kisiasana kimaisha kwa ujumla bila ushawishi wa vitu vidogo kama sinia za wali pamoja na pombe.

Pia nakubaliana na wewe kuwa nchi yetu inahitaji mapinduzi ya kiuchumi na hilo ndilo lengo kubwa la kila raia, lakini kwa uzoefu unaweza kuona kuwa nchi haiwezi kuwa na mabadiliko makubwa kiuchumi (Uchumi imara) ikiwa siasa zake zinalegalega. Hii inatokana na ukweli kuwa uchumi wa nchi unategemea mazingira mazuri kisiasa ili uweze kwenda vizuri. Chukulia mfano viongozi wetu wanaolaumiwa kwa kulirudisha nyuma Taifa kutokana na kuiba mabilioni ya fedha ambayo yangeweza kutumika katika kujengea Barabara, shule, vyuo, hospitali nzuri pamoja na huduma nyingine muhimu za kijamii.

Kwamba Tanzania tumepiga hatua kisiasa kuliko nchi nyingi za kiafrika basi hatuna budi kujipongeza, lakini je kwa mtazamo wako hayo mapinduzi unayoyasema yanatosha kiasi kuwa hakuna haja tena kuendelea na mikakati ya kufikisha ujumbe kwa wale ambao hawajafikiwa?

Hivyo basi napendekeza yawepo mapinduzi ya kweli ya kisiasa kwanza ambayo pia yatakuwa changamoto kwa viongozi pindi watakapotambua kuwa wananchi wapo makini na mienendo yao hivyo kupelekea wao kutokufanya mambo ya ajabu kwa kuhofia kunyimwa nafasi za kuongoza tena wakati wa uchaguzi.
 
Kijarida cha Jamboforums, kisichofungamana na chama chochote, kitakachosambazwa nchi nzima, kitakachotoa elimu ya siasa ama kwa bure au kwa bei ya chini kabisa, kitakachosambazwa nchi nzima na kuchapishwa kila baada ya wiki mbili.

Makala za uwakilishi zitaandikwa hapa, kuchujwa umakini, kupigiwa kura halafu kuchapishwa.

Funds zitatoka kwa members hapa na watutakiao mema.Tayari tuna waandishi wa habari na watu wa media wenye uzoefu na uchapishaji.Ikibidi hata kutengeneza soft copy itakayosambazwa bure kwa email kwa wawakilishi tofauti nchini kote halafu wawakilishi waweze ku print, kama wataweza kufanya huduma bure au kuuza kwa bei nafuu ili kurudisha gharama za uchapishaji yote ni sawa.

In any case Jamboforums need a newsletter, period.

Angalau na watu wa vijijini wapate mwamko wa kujua nini kinaendelea.Tunaweza kuweka habari za kisiasa, maendeleo ya bunge, wabunge na performance zao, ahadi za serikali kuu na utekelezwaji wake, data za kiuchumi nk.

Kwa sasa huu ndio mchango wangu.

Naunga mkono hoja yako Mkuu na naamini kuwa hii itakuwa ni hatua moja kubwa sana kuweza kufikia lengo la kujenga jamii yenye Demokrasia ya kweli.
 
Nafikiri Jambo la kufanya ni kutengeneza Rasimu ya nini kiandikwe na kiandikweje na habari zisambazwe kwa njia ipi?
Ili tuweze kufikisha elimu nzuri kwa wananchi wote tz.
 
Back
Top Bottom