Mwamko wa Biashara kwa watanzania ni tatizo nini kifanyike? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwamko wa Biashara kwa watanzania ni tatizo nini kifanyike?

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by che-guavara, Dec 15, 2011.

 1. che-guavara

  che-guavara Member

  #1
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwamko wa Biashara miongoni mwa watanzania wengi bado ni tatizo. tatizo hasa liko wapi, na ufumbuzi wake uweje? mi ntajaribu machache lakini wengi tunaweza tukashirikiana majibu na utekelezaji wake kwenye maeneo tunayoishi na jamii tunazoishi nazo tukawa na mijada midogo in the form of community meetings kuona jinsi gani tunaweza kuchangia mawazo yetu kupitia mawazo tutakayopata kupitia thread hii.

  changamoto
  1. biashara inaonekani si ajira bali ni kitu cha kufanya kwa waliokosa kazi za maofisini
  2. kufanya biashara ni kazi ya watu wajanja wajanja decent people hawatafanikiwa
  3.wanaoweza biashara ni watanzania wa-asia si kazi ya watanzania (weusi)
  4. kufanikiwa basi kwanza uwe mwizi mwizi, zulumati, usiwalipe vizuri wanao kusaidia, n.k
  5. biashara ni uchuuzi tu sio kilimo,ufugaji au ujenzi
  6. huo mtaji unatoka wapi?

  cha kufanya.
  1. kuwe na mijadala midogo ngazi za wakazi wa mtaa au kila kitongoji, miji, wilaya na kanda kuangalia namna ya kujikwamua


  mwisho.
  >msomaji wa thread hii uchukue jitihada za kuwaelimisha na wengine pia wasomaji hapa great thinkers .naomba kutoa hoja
   
 2. L

  LAT JF-Expert Member

  #2
  Dec 15, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  kweli kabisa,

  mazingira ya ufanyaji biashara ni magumu kwa wale wanaotaka kuanzisha biashara mpya (start ups), kunatatizo la mitaji ilhali watu wengi sana wana mawazo mazuri sana ya biashara, masharti ya mabenki kutoa mikopo ni kikwazo pia
   
 3. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #3
  Dec 15, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  Mkuu Ujasiriamali wa Tanzania una mlololongo mwingi sana.
  - Hili la watu kuchukulia Ujasiriamlai au Biashara kama altenative ya mtu kukosa kazi lina sababishwa na Mambo mengi sana.

  1. Nchi yetu Ilikuwa ya kijamaa, so vitu vingi vilikuwa vinapatikana bure mfano
  - ELIMU BURE
  - MAJI BURE
  - MATIBABU BURE NA KAZALIKA

  - Hapa kwenye Ujamaa Watanzania wengi walikuwa hawaoni umuhimu wa kufanya biashara kwa sababu kulikua na maduka ya ushirika, kulikuwa na vitu kama RTC mtakumbuka, vitu vyote vilifanyika kwa ushirika, mashamba ya ushirika.
  - Watanzania ikabidi wano soma wote wawe wanaajiriwa make business inafanywa na serilaki na Wahindi wachache tena kwa kibali cha Nyerere.
  - WATOTO WENGI WALIO KUWA WANAZALIWA WALIKUTA WAZAZI WAO WANAFANYA KAZI KWENYE EITHER MASHIRIKA YA UMA AU SERIKALINI SO NA WAO WAKAWA WANALITH MAMBO YA WAZAZI WAO YA KUFANYA KAZI ZA KUAJIRIWA KUMBUKA SUCCESSES IS GERNETIC
  - Hili la ujamaa limeendelea kutuathiri hadi leo hii, tukiamini hata mchele ukikosekana sokoni Serikali ndo inatakiwa ilete huo mchele

  2. Story za Wazazi
  - Wazazi wanamchango mkubwa wa kumuandaa mtoto kuja kuwa na mafanikio- Kwa hili wazazi nazani hapa ni asilimia 100% huwa wana wasisitizia watoto tangia wakiwa chekechea wasome kwa bidii waje kuwa Mameneja, wapate kazi nzuri kwenye mashirika makubwa, mfano wapate kazi Benki wawe mameneja wa Mabenki, so mtoto anakuwa anasoma kwa bidii akitageti kuja kupata kazi nzuri tiyali ameisha tagetiwa aje kuajiriwa, hapo mawazo ya kujiajiri hayapo tena
  - Hakuna mzazi anae mwambia mtoto wake asome aje kuwa mfanya biashara mkubwa hapa nchini

  3. Story za Walimu, shule za misingi, Sekondary na Vyuoni.
  - Hapa mtoto akifika shuleni hukutana na hadith za asome aje kuwa mtu fulani Meneja, Chuoni napo anaambiwa asome aje kuwa mtu fulani

  4. Story za marafiki
  - Watoto tangia wakiwa wadogo hupigiana story za kuja kufanya kazi kwenye makampuni makubwa kama kwenye migodo, TRA, BANADARINI NA KAZALIKA, Na hizi story ziko hadi vyuoni huko.story za kufanya kazi TRA

  5. Mfumo wa Elimu yetu
  - Elimu yetu inaandaa watanzania kuwa mameneja na kazalika na haiandai wanafunzi kujiajiri, Hata vyuo vikuu nako ingawa kuna somo la ujasirimali na kuna vyuo vinatoa Degree za Ujasiraimali kama Mzumbu, UDOM na kazalika, Hawa wanafunzi wanao somea hizi kozi ukiwauliza ndoto zao wote ni kuajiriwa. Na kweli wakigraduate unakutana nao wakiwa wamebeba Bahasha za vyeti wakitafuta kazi.
  - Hapa ni kwamba ni vigumu sana kuja kufundisha ujasiriamali mtu ameisha kuwa mkubwa na tangia akiwa mtoto aliambiwa na wazazi wake asome aje kuwa meneja.

  6. Serikali yetu
  - Hamna vivutio vya kutosha kuwa atract watiu waingie kwenye ujasiriamali, mfano mikopo, grant na kazalika, nchi zingine unakuta kuna vivutio vingi sana vya watu kujiajiri wenyewe.

  7. Extended familly yetu.
  K
  wa kweli huu mfumo nao some time unalemaza watoto, kivipi,
  - Mtoto hajishighulishi akiamini ndugu zake wana uwezo watamsaidia tu mfano Wajomba, Mashemeji, Mashangazi, Kaka, Dada, Mama mdogo, Baba Mdogo, Mabinamu na kazalika na kweli huyu kijana akiwa na tatizo akiwafuata hao ndugu zake wanamsaidia, so hapa hawezi pata akili za kijiajiri wakati ndugu zake wapo na wanamtoa.

  NINI KIFANYIKE HAPA?

  - Wazazi
  Wabadili mfumo wa kulea watoto wao, wawafundishe mfumo wa kujitegemea zaidi wakuja kuwa wafanya biashara badala ya kuajiriwa

  - Walimu nao
  Wajaribu nao kubadili akili za wanafunzi kutoka kuajiriwa kuwa waajiri

  -Gavament
  Iweke vivutio vya kutosha, itafute pesa za kuwakopesha graduate wanao kuwa tiyali kujiajiri, kama wanaweza kutumia bilion 60 kwenye uhuru wanashindwaje kutafuta hata bilion 50 za kuanza kuwakopesha graduate na vijana wengine wa mtaani?

  - Vijana wenyewe
  Waache story za kufanya kazi TRA, BENKI, TANAPA na kazaliki wapige story za kuwa waajiri


  - Vyuo vyetu navyo
  - Katika kutoa Elimu za ujasiriamali au Degree za ujasiriamli wajaribu wajaribu kuwa practically zaidi kuliko theoreticall. Mfano kweny mafunzo wawe hata wanaleta wafanya biashara wakubwa na waliofanikiwa wanakuja kutoa lecture mara mojamoja

  - Haya mambo ya kufundishwa elimu ya Ujasiriamali na watu walio ajiriwa yana kuwa haya hamasishi watu kujiajiri
   
 4. M

  Malila JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Naomba nichangie kutokea kwenye uzoefu kidogo nilio nao. Njia mojawapo ninayo iamini kwa sasa inaweza kutusaidia kujenga mitaji ni kuunganisha nguvu zetu ktk vikundi vidogo vidogo ili hatimaye vyombo vya fedha viweze kuchangia kutupa mitaji zaidi.

  Njia ya pili ni kila mmoja kuanzia pale anapoweza. Kuna dogo mmoja toka chuo kikuu, aliomba msaada wa mkopo, lakini alitumia boom lake vizuri kuanza kukusanya uwezo ili kufikia ndoto zake.

  Njia ya tatu ni kujifunza toka kwa waliojenga mitaji yao kwa njia za haki, hii ni njia ngumu sana kwa sababu inachukua muda mrefu, kwa wapenda mkato hailipi.

  Njia ya nne, ni kumtumikia kafiri/baniani ili upate mradi wako. Kwa mfano, mimi napenda kilimo sana, lakini mtaji nilikuwa sina, ikabidi nikubali kutumwa ili kuanza kukusanya mtaji, kukopa haikuwezekana kwa sababu sifa zinazohitajika nilikuwa sina.

  Naomba niishie hapa kwa leo.
   
 5. che-guavara

  che-guavara Member

  #5
  Dec 15, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi na hoja zote.kama ni hivyo basi mi naona sehemu ya kuanzia ni kwenye mfumo wa elimu.kwa sababu tulibadili mfumo basi swala hili liingizwe kwenye mitaala yetu.
   
 6. J

  JAY2da4 JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kikubwa ni attitude tuliyojijengea katika jamii yetu.Ukianzia katika familia,mfumo mzima wa elimu yetu na jamii iliyotuzunguka,tunaamini kuajiriwa ni bora kuliko kujiajiri,hasa linapokuja suala la security.Tena hasa tuliobahatika
  kusoma ndo kabisa suala la kujiajiri hatulipi umuhimu maana shuleni wametufundisha kuja kuajiriwa.

  Nakupa mifano hii hapa;
  1.Mr.A kamaliza chuo kikuu mwaka2007 anafanya kazi Airtel,mshahara Tsh 1M kwa mwezi,tai masaa yote.
  2.Mr.B kamaliza chuo kikuu mwaka 2007,kwa vile ndoto zake ilikua ni kujiajiri,akanunua machine ya kutengeneza
  ice cream,pia anatengeneza juice fresh,akaanza hiyo biashara.Ana idea nyingi lakini zingine zinahitaji mkopo mkubwa
  ila akaona aanze na hiyo anayoweza ili baadae ajipanue kadri anavyozidi kuizoea biashara.

  *Jamii itampa credit nzuri sana Mr.A kwa kuajiriwa Airtel ,jamii hiyo hiyo haitampa credit Mr.B kwa sababu ana degree
  halafu anauza ice cream,kwa nini asitafute kazi.

  Hawa watu wa wawili baada ya miaka 15,kama Mr.A atabaki hapo Airtel kwa muda wote huo,na Mr.B akaendelea na
  biashara zake ,usiku na mchana akibuni aina mbalimbali za biashara.Basi ni dhahili Mr.B atakua mbali sana,si ajabu
  ukamkuta kaajiri watu zaidi ya 30 na ana cash flow ya Tsh 200M kwa mwezi .Na Mr.A atakua kashapewa promosheni
  kazini,na mshahara wake umefikia Tsh 3M.Ndo wakati huo jamii itaanza kuanza kumpa credit Mr.B na kumuita boss.

  Mitaji ni tatizo kwa kweli,interest rate zipo juu sana.Nchi tajiri duniani business loan interest zipo kuanzia 2% hadi 7%.
  Lakini hili lisiturudishe nyuma,lazima tukabiliane nalo.Kitu kingine ni bana ni sera mbovu za serikali,unaweza ukawa na wazo
  zuri la biashara na ukawa unahitajia baadhi ya vibali kutoka serikalini ili uenze kuanzisha hiyo business,kwa kweli utajuta
  kuzaliwa Tanzania,utazungushwa sana.

  Mabadiliko inabidia yaanzie kwa wazazi tuwaandae watoto wetu kuja kujiajiri,tuwatolee mfano wahindi wao wamejikita katika
  kujiajiri .Na huku nje naona asilimia kubwa ya wahindi waliopo ughaibuni wanapendelea kujiajiri,tofauti na sisi.


  " remember the story of the Balloon seller in the beach. When ever there is a slump in the sales the balloon seller would fill one balloon with oxygen and release it. When the balloon goes up to the sky, children who are playing around would see the balloon and the sales would go up. One day as usual, he released a balloon. Seeing that one child come to him and asked this question "If you release a Black balloon, will it go up?" The balloon seller replied to that little boy, "The colour of the balloon doesn't make any difference, what is inside the balloon is the matter and it is taking it up."

  Hata katika biashara kinachotujenga ni kile kilichomo moyoni mwetu,sio rangi,wala kabila,wala urefu wala ufupi,wala kuzaliwa katika famillia bora.
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na mawazo ya wadau wengi hapa, ila tatizo kubwa ninaloliona ambalo linaathiri malengo ya wengi kutofikiwa ni dharau na kuchagua aina ya ajira kwa maana ya kutoangalia kipato ila kuonekana una tie shingoni.

  Ukiona ughaibuni watu wanajali nini ataingiza mfukoni hata iwe ni kuzibua vyoo ambavyo vina risk kubwa na dao kupanda hivyo kumwezesha kuliko kushinda kwenye keyboard ambayo haikuwezeshi ila utaendelea na hewala kama mtwana kwa mtwa.

  Biashara ndogo ndogo tunazodharau ndizo chimbuko la kufanya makubwa, kwani elimu ni ufunguo ambao ni investment ya uhakika ukiitumia vema. Tusitarajie mambo ya pekee au mitaji, ila ukituliza kichwa utaweza kutumia vema elimu yako kuanzia hata na kuuza nyanya, ukondakta nk. Machinga wengi wamefanikiwa kusimama bila elimu kutokana kumaliza kandambili, iweje mwenye elimu ushindwe kubuni njia ambayo itakufaidia?

  Nawapongeza ambao pesa za mkopo wanazitumia kuanzisha biashara, kwani baada ya kuhitimu hawatamaliza nauli kuzunguka maofisini kuomba kazi, bali kutumia muda wao mwingi kuimarisha biashara na kujizatiti zaidi katika kujiajiri. Wengi vyuoni wanaishi maisha ya starehe sana, na weekend ni kuishia kujirusha kwa mwigo wa bila gf/bf hakuna burudani ya maraha. Pesa hizo ungeisave na kusubiri kwamba ipo siku nitajiburudisha nikishakuwa na source ya uhakika baada ya kutaabika wengi wangefika mbali.

  Mikopo ni mizuri lakini pia ni kitanzi ambacho hata nchi zilizoendelea wanajutia. Taasisi za pesa ni biashara na wala si huduma, na matokeo yake foreclosure zinawachanganya watu akili zao na kukata tamaa ya maisha. Binafsi nisingependelea huu utaratibu wa mikopo vinginevyo umejiamini na biashara unayokusudia.

  Pendekezo, turudi kwa Nyerere kama vijana watatu au wanne chuoni wakiamua kuungana na kuchangia kidogo walicho nacho kisha kuanzisha biashara, inaweza kuwaletea matunda. Baadaye biashara ikishaanza kuimarika wanafungua matawi kadiri ya idadi yao, kisha watakuwa wameshaimarisha malengo yao, na kuondokana na kuilalamikia serikali kupata ajira wakati serikali hana nafasi ya kuajiri watu wote hawa, kwani vyuo ni vingi sana na kila mwaka wanahitimu maelfu huku wanaostaafu ni mamia.
   
 8. Dio

  Dio JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 1,278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  mkuu hapa umenena,naomba hii comment yako niichukue niiweke kwenye blog yangu umenikuna sana,
  gonga hapa uicheck blog yangu
  http://gshayo.blogspot.com
   
 9. che-guavara

  che-guavara Member

  #9
  Dec 16, 2011
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mikopo ni mizuri lakini pia ni kitanzi ambacho hata nchi zilizoendelea wanajutia. Taasisi za pesa ni biashara na wala si huduma, na matokeo yake foreclosure zinawachanganya watu akili zao na kukata tamaa ya maisha. Binafsi nisingependelea huu utaratibu wa mikopo vinginevyo umejiamini na biashara unayokusudia.

  1. Ni kweli mkuu. hapa tanzania ukifuatilia history ya makampuni yaliyouza hisa kwa mara ya kwanza (IPO) zote zilikuwa na over-subscriptions mfano TBL,TWIGA,CRDB, NMB,n.k ni yote tu.na katika IPO wanaoruhusiwa ni watu binafsi(kiasi cha 80% na 20% makampuni.kama pesa kwenye ipo zinazidi almost double inamaana watu wanamitaji ya kutosha kwa kuunganisha nguvu
  mfano.watu 30 wanaweza kutoa shs.2,500,000=Shs.75,000,000/=
  2. wawekezaji kutoka nje wengine ni waliojichangishana mitaji kwenye jamii zao na kupata large sums na kuwekeza.kama tusipoangalia rangi ya baloon.tukawa na vikundi vya watu wachache tunaoshi maeneo au ndugu wa wenye focus moja.nahisi inawezekana.
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ukweli hujitenga na wongo. Umenena iliyo kweli na kuona from all angles.
   
 11. M

  Malila JF-Expert Member

  #11
  Dec 16, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Kwa kuunganisha vibaba vyetu tunajaza debe kisha pipa kisha tank. Mikopo si njia nzuri sana kwa wajasiriamali wadogo,ili kujenga mitaji ni vizuri tuanzie tulipo, kisha twende kwenye mikopo tukiwa na kitu chetu from the grassroots.
   
 12. Habdavi

  Habdavi JF-Expert Member

  #12
  Dec 16, 2011
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 393
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  principle nyingine tunatakiwa ili kutimiza dhana hii ya kujiari ni kwamba linalowezekana kufanyika leo, ni vizuri kuanza. Tuache kuwa na mipango mizuri na idea nzuri bila utekelezaji.
   
 13. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #13
  Jan 5, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Tatizo kubwa la wabongo ni uhoga wa kuthubutu..anaanza kushindwa kabla ajaanza step ata moja.
   
 14. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #14
  Jan 6, 2012
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Nadhani kuna suala ambalo naona pengine wadau hatujaligusia hapa.

  Kuunganisha nguvu za mitaji ni wazo zuri sana, ukizingatia watanzania walio wengi ni wenye vipato vya chini. Bila kuunganisha nguvu za mitaji, ni vigumu kwa mtanzania mmoja kuanzisha kampuni kubwa.

  Lakini hata hivyo, tatizo kwenye kuunganisha mitaji linakuja pale unapogusia suala la UAMINIFU wa watanzania. Baada ya kuunganisha mitaji, ni nani mwaminifu anayeweza kusimamia vyema maslahi yetu sote na sio maslahi binafsi? Mnakumbuka hisa za NICOL? Klichotokea NICOL kitawafanya watanzania wengi kuwa waoga zaidi linapokuja swala la kuunganisha mitaji.

  Masharti ya kukopa yamekuwa ni magumu na interest rate ni kubwa kwa sababu nyingi, lakini moja wapo ni kwa sababu ya risk kubwa inayoambatana na kumkopesha mtanzania. Kama kweli risk ya kumkopesha mtanzania ingekuwa ndogo, mimi binafsi naamini kabisa kungekuwa na ushindani mkubwa katika financing industry. Masharti yasingekuwa magumu kama yalivyo leo na pia hata riba zingepungua kutokana na ushindani amabo ungeletwa na utitiri wa taasisi nyingi za kutoa mikopo.

  Wakenya wengi wanazidi kuajiriwa kila leo hapa Tanzania kwa sababu watanzania wengi si waaminifu katika kazi.

  Bila kuwa waaminifu, watanzania hatuwezi kufika mbali.

  Moja ya sifa ya kufanikiwa ni kuwa mwaminifu. Tunaweza kusema mengi, ila kama watanzania hatuta tambua thamani ya kuwa waaminifu, jitihada zote tutakazofanya zitaishia hewani tu.
   
Loading...