Mwami Theresa Ntare VI wa Heru - Chifu wa kwanza mwanamke

Ila wazungu na waarabu walituweza itachukua miaka 10,000 kuondoa mizizi waliyoiweka kwenye DNA zetu na hapo ndipo tutakuwa huru.
Namwona mwamba kapiga way ili apate kuonekana naye kachana nywele kama mzungu.
 
Alipata nafasi ya kwenda kusoma Ulaya enzi ukoloni nafasi maalum za watoto wa machifu.Alihitimu mafunzo ya ya sheria.Alikuwa msaada mkubwa sana wa kisheria wakati wa kudai Uhuru,hasa kwenye mikataba ya kimataifa.

Mengi hayajulikani katika historia ya utoto wa Mwami Theresa Ntare, lakini inaaminika alikuwa mtoto wa kike pekee wa Chifu Ntare. Inaelezwa kwamba Mwami Thereza Ntare alitawazwa uchifu baada baba yake Mwami Ntare kukosa mtoto wa kiume.

Baada kutawazwa uchifu ilibidi atafutiwe mchumba kutoka ukoo wa Chifu Lusimbi wa Kalinzi hivyo akawa ameolewa na kijana wa kitutsi kutoka Kalinzi akiitwa Bw. George Shinganya.

Kulingana na mila za Kiha, Mwami haolewi. Akiolewa inabidi ahame milki yake ya Uchifu ili akawe mke wa huyo muoaji. Hivyo basi, Mwami Ntare hakuolewa na Bw. George Shinganya. Bali familia ya Mwami ndiyo iliyolipa mahari kwa familia ya Bw. George Shinganya. Hivyo, Jina la Shinganya likaondolewa na akaitwa George Ntare.

Baadaye ndoa ya Mwami Theresa Ntare na George ilivunjika na Mwami Theresa Ntare akaoana na Mwami Louis Dantes Ngua wa Ufipa(Huyu ana asili ya uchifu wa Ufipa). Kuna nadharia zinazoeleza pia kuwa Mwami Theresa Ntare alipata pia kuwa mke wa Chifu Makwaia wa Usukuma. Lakini hakuna ushahidi wowote juu ya hilo
Wakati wa zama hizo jamii nyingi za Kiafrika zilitajwa kuwaweka nyuma wanawake hasa katika masuala ya Uongozi. Hilo halikumfanya Mwanamama Mwami Theresa Ntare asiweze kuongoza vizuri na kishupavu jamii yake ya Waha wa Heru huko

Hakuishia hapo, mama huyu aliweza kushika wadhifa mkubwa ambapo alikuwa ni Mkuu wa machifu wote Tanganyika akipokea kijiti kutoka kwa Chifu Petro Itosi Marealle mwaka 1958. Makabidhiano yalifanyika shule ya sekondari ya Mzumbe, na mpaka sasa Mzumbe kuna bweni linaitwa Ntare.

Mwani Theresa Ntare aliheshimika kama chifu wa Kasulu yote na sio tu Heru alisimamia vyema msimamo wa Baraza la Machifu mwaka 1958 na kuunga mkono juhudi za TANU katika kudai uhuru.

Mwami Theresa Ntare alikuwa ni mmoja ya Wabunge wachache wa Baraza la Kutunga Sheria la Tanganyika kabla hata ya Uhuru wa Tanganyika.

Aliendelea kuwa Mbunge mpaka miaka ya 1980, lakini kabla ya hapo aliachia uchifu Disemba 9, 1962, Katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam nchini Tanganyika. Hapo alikaribishwa kama Malkia wa Heru kwa Ngoma Maalumu kutoka Ngome ya Malkia wa Heru kwa heshima kubwa.

Inaelezwa alifariki miaka ya 90
20230627_023103.jpg
20230627_024643.jpg
20230627_024623.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app

20230627_023103.jpg

20230627_024643.jpg
20230627_024623.jpg
 

Similar Discussions

16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom