Mwambieni Rais Magufuli apunguze sauti. Nchi hii bila wazungu ni tajiri kwa kipi?

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
9,064
2,000
Vitu vingi ambavyo Magufuli anaviona kama ni utajiri wa nchi hii vinamtegemea mzungu.

Wazungu wakiacha kununua Tanzanite itageuka kuwa kete za kuchezea bao. Vivyo hivyo kwenye dhahabu, almasi, chuma, bati, n.k . Madini kama uranium hatuyawezi kabisa hata kuyatumia, achilia mbali kuyachimba. Helium hata matumizi yake hatuna.

Bila mzungu utalii wa kila aina haupo na husimama kabisa. Ikiwa watanzania huwa hawaendi kutalii huko kwenye mbuga za wanyama maarufu kama Serengeti, Ngorongoro, Manyara, na Mikumi, nani ataenda Chato?

Sasa Magufuli anaposema nchi hii ni tajiri kwa kuwananga wazungu anaelewa anachosema?

Zimbambwe, Mugabe alikuja na approach hii hii ya Magufuli ya kuwananga wazungu. Matokeo yake umaskini uliowakumba wazimbabwe baada ya wazungu kuondoka na kususa sote tunaujua.

Mwambieni Magufuli, apunguze dhihaka dhidi ya wazungu. Dawa anazotumia yeye kama Rais akiugua, first class medicines, hazitengenezwi Chato. Sasa sijui kaziamini vipi? (Nimechomekea tu jamani).

Wazungu wametutangulia,na wametuwahi wakashika mifumo yote ya kibiashara na kiuchumi. Tuwe wapole, tuwatumikie hawa makafiri ili tupate mradi wetu.

Mkumbusheni Magufuli anachokifanya ni sawa na Matonya kujaribu kushindana na Bakharesa.
 

Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
2,053
2,000
Umeongea vizuri, wakiamua almasi, tanzanite ni kama gololi, haina thamani tumeishaa, wakiamua, meli wanaunda na plastics hiyo Mchuchuma na Liganga ni bure.

Akiamua apige ban ARV dawa zake zisije Bongo, tulio na ndugu walioathirika, tutabeba mizigo mikubwa kulea familia zao.

Everyday is Saturday........ :cool:
 

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
11,765
2,000
Kwa yanayoendelea Tanzania kwa sasa...am just speechless! Ni kama vile niko ndotoni na kwa ninavyohangaika naomba iwe kweli niwe usingizini ili nitakapoamka niweze kuishi tena kwa amani na matumaini kama zamani.

Kama ninayoyashuhudia ni kweli...am dumbfounded! Ni heri niendele kuuchapa huo usingizi kwani kwa woga nilio nao sitamani kuamka na kujikuta miongoni mwa baadhi ya Watanzania ambao michango yao naisoma humu.

Kama aliyeona milango ya shule bado ana mawazo kama ya babu wa babu yangu...inashangaza, inasikitisha, inaudhi na inatisha! Heri niendelee kulala na kama mpo mlio macho nawaomba msijaribu kuniamsha...sitaki kuteseka!
 

Billie

JF-Expert Member
Aug 13, 2011
11,497
2,000
Huyu mzee anatucost kichizi kwa kauli zake za kuwabeza hawa wazungu.Kaka yangu kapack baada ya kampuni fulani ya wamarekani kufunga na kuondoka nchini.
SASA HIVI TUNAAMINISHWA KILA MZUNGU AJAE NCHINI NI MPELELEZI NA UMASIKINI NDO UZALENDO ni.ujinga wa hali ya juu.
 

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
4,799
2,000
Kiukweli ni kauli za aibu zama hizi. Kulaumu wengine kwa madhaifu yetu.Kisa hatuna $$$$ hata kuwakinga wauguzi na wazee wetu,mkuu kafunga mjadala wa chanjo, wapo waungwana wengi wangetusaidia bure bila garama walau kwa kundi maalumu.
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
9,064
2,000
Jana umemsifia Kwa mapambio yote na Leo unamponda?
maisha ya kibongo si mchezo
Kasome vema nilichomsifia
Umeongea vizuri, wakiamua almasi, tanzanite ni kama gololi, haina thamani tumeishaa, wakiamua, meli wanaunda na plastics hiyo Mchuchuma na Liganga ni bure.

Akiamua apige ban ARV dawa zake zisije Bongo, tulio na ndugu walioathirika, tutabeba mizigo mikubwa kulea familia zao.

Everyday is Saturday............................... :cool:
Magu asicheze na wazungu. Hata hiyo mitambo inayomlinda inatumia satellites ambazo ni mali zao. Asiwakoromee.
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
9,064
2,000
Huyu mzee anatucost kichizi kwa kauli zake za kuwabeza hawa wazungu.Kaka yangu kapack baada ya kampuni fulani ya wamarekani kufunga na kuondoka nchini.
SASA HIVI TUNAAMINISHWA KILA MZUNGU AJAE NCHINI NI MPELELEZI NA UMASIKINI NDO UZALENDO ni.ujinga wa hali ya juu.
Tuna rais wa ajabu haijawahi kutokea
 

Ooh yes

Senior Member
Jul 31, 2020
141
225
Vitu vingi ambavyo Magufuli anaviona kama ni utajiri wa nchi hii vinamtegemea mzungu.

Wazungu wakiacha kununua tanzanite itageuka kuwa kete za kuchezea bao. Vivyo hivyo kwenye dhahabu, almasi, chuma, bati, n.k . Madini kama uranium hatuyawezi kabisa hata kuyatumia, achilia mbali kuyachimba. Helium hata matumizi yake hatuna.

Bila mzungu utalii wa kila aina haupo na husimama kabisa. Ikiwa watanzania huwa hawaendi kutalii huko kwenye mbuga za wanyama maarufu kama Serengeti, Ngorongoro, Manyara, na Mikumi, nani ataenda CHATO??

Sasa Magufuli anaposema nchi hii ni tajiri kwa kuwananga wazungu anaelewa anachosema? Zimbambwe, Mugabe alikuja na approach hii hii ya Magufuli ya kuwananga wazungu. Matokeo yake umaskini uliowakumba wazimbabwe baada ya wazungu kuondoka na kususa sote tunaujua.

Mwambieni Magufuli, apunguze dhihaka dhidi ya wazungu. Dawa anazotumia yeye kama rais akiugua , first class medicines, hazitengenezwi Chato. Sasa sijui kaziamini vipi? (Nimechomekea tu jamani).


Wazungu wametutangulia,na wametuwahi wakashika mifumo yote ya kibiashara na kiuchumi. Tuwe wapole, tuwatumikie hawa makafiri ili tupate mradi wetu.

Mkumbusheni Magufuli anachokifanya ni sawa na Matonya kujaribu kushindana na Bakharesa.
mi najionea maisha yamekuwa magumu balaa yani nashindwa kusaidia wazazi ndg na marafiki walionisaidia enzi nasoma marafiki nimepoteza naonekana najidai siwasaidii mwaka wa 7 kazini wala daraja sijapanda,mungu tusaidie huyu mze baba alegeze kidogo
 

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
5,000
2,000
Wacha uoga wewe
Wakuogopwa ni Mungu tuu
Sasa kwa taarifa yako baada ya mungu ni mzungu!!ndio mnajidanganya hivyo?!!unadhania wazungu wamuweke kati(meko)atatoboa?!! Hata kama akili yako imehifadhiwa na sterling wa filamu(god must be crazy) kule lumumba huwezi shindwa kulijua hilo!!
Huyo mungu ndio atanunua hayo madini yako?hiyo bajeti yako asilimia kubwa wao ndio wanakusaidi, licha ya kujifanya kuwa wafrika ndio tuna mjua mungu sana, mbona ndio sehemu yenye watu makatili sana, na vitendo vya kishezi, kuliko sehemu yoyote ile duniani?!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom