Kijogoodi
JF-Expert Member
- Mar 29, 2021
- 1,363
- 2,372
Tukiwagusa Acacia tutashitakiwa MIGA alisikika Lissu msomi aliyesomeshwa kwa kodi za watanzania lakini badala yake tukaja kulipwa billion 700 na Acacia ikafutwa na ikaundwa kampuni mpya ya Twiga ambayo Tanzania tuna hisa 16% na kwenye top management ya kampuni wapo watanzania. Kupitia kampuni mpya ya Twiga watanzania wameendelea kupata gawio la mabilioni ya fedha kila mwaka zinazotokana na mauzo ya madini.
Lissu alilipwa na nani kuwadanganya watanzania? Lisu ni msaliti aliyechangamka.
------------ ------- ---------- --------
Dodoma. Sakata la makinikia limetinga bungeni baada ya Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina kuhoji kwa nini Serikali ilikubali kupokea sh. 700 bilioni zilizotokana na kesi za malimbikizo ya madeni ya makinikia badala ya sh. 360 trilioni ambayo ni madai halali kwa Tanzania?
Mpina amehoji swali hilo la nyongeza katika kipindi cha maswali na majibu bungeni leo Alhamis, Septemba 22,2022.
“Kwa nini Serikali ilikubali kupokea sh. 700 bilioni kutoka katika kesi za malimbikizo ya madeni maarufu kama makinikia badala ya Sh360 trilioni ambayo ni madai halali katika nchi yetu?” amehoji.
Akijibu swali hilo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema Serikali haijakubali kupokea fedha hizo (Sh700 bilioni) na kuacha Sh360 trilioni, isipokuwa ilipeleka malalamiko kuhusu kampuni za madini.
Hata hivyo, kabla ya kumaliza kulijibu swali hilo, Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson alimkatisha na kutaka ufafanuzi wa majibu ya Serikali yaliyotofautiana na swali la msingi lililoulizwa na Mpina.
Akijibu swali hilo, Waziri Mwigulu amesema Serikali haikupokea kimya kimya fedha hizo (Sh700 bilioni) na kuacha sh. 360 trilioni bali kilichofanyika ni kwa Serikali kupeleka malalamiko kwenye kampuni za madini.