Uchaguzi 2020 Mwambie mwenzio hakuna kususia uchaguzi, nenda kamchague mtu wako

Rufiji dam

JF-Expert Member
Feb 20, 2020
3,796
8,771
Shime wana, shime akina baba, shime Wafanyakazi, shime Wafanyabiashara. Hakuna kususia uchaguzi kama ilivyotokea uchaguzi ama uchafuzi wa serikali za mitaa. Tujitokeze tukumbushane. Fanya maamuzi sasa inawezekana tena unaweza kuendelea na furaha kama unayo.

Tutoke kwa wingi.
 
Hakuna nafasi nyingine zaidi ya October kwa mtz kulipiza kisasi dhidi ya Utawala huu dhalimu, kwa sababu mbili. Moja atohitaji Tena kura zenu atakumalizieni visasi vyake vyoote akijua arudi tena hivo hakuhitajini.

Pili kwa Moto anaopelekewa baada ya kuamini upinzani imekufa anaweza akabadili katiba ili akuteseni milele vizuri. 5 yrs watumishi wameteswa kisa tu hisia eti walimpigia kura Lowasa, kimara na ubungo wakabomolewa hisia tu waliipigia chadema. Sasa Leo mnajaa mikutano ya Lisu Hali itakuaje akishinda si ndo tutalimia kucha.

October ndo nafasi pekee ya kulisambaratisha jiwe, tukikosea tena tumekwisha tutavunjwa vunjwa na jiwe Hadi tuchakae
 
Na bahati mbaya zaidi

narudia tena

NA BAHATI MBAYA ZAIDI KWENU

Hamkuwahamasisha watu wenu kwenda kujiandikisha/kurekebisha taarifa zao kwenye daftari la mpiga kura, mlikuwa bize kutengeneza matukio ya kuvunjana miguu ili muisingizie serikali lakin mambo yakawageuka, sasa mnategemea hao wapiga kura wanatoka wapi, au na hili mnategemea YUENI kupitia BIBISII waje wawaongelee?
 
Na bahati mbaya zaidi.

narudia tena.

NA BAHATI MBAYA ZAIDI KWENU

Hamkuwahamasisha watu wenu kwenda kujiandikisha/kurekebisha taarifa zao kwenye daftari la mpiga kura, mlikuwa bize kutengeneza matukio ya kuvunjana miguu ili muisingizie serikali lakin mambo yakawageuka, sasa mnategemea hao wapiga kura wanatoka wapi, au na hili mnategemea YUENI kupitia BIBISII waje wawaongelee?
ccm wanaojitambua watampa Lissu
 
Sijajiandikisha, simply nshaanchana na politics baada ya lowasa kututuliza 2015 na sijawahi kunafaika nazo, kila mtu acheze mechi zake, mimi nnapambana na yangu, ila kiukweli ningejiandikisha basi, kura yangu ni kwa magufuli, lissu ataturudisa miaka 10 nyuma, nikimsikia kuhusu majimbo ndio nnaona 30 years back
 
i hope hatutalia tumeibiwa kura zikiwa chache

matumaini mengi hadi tunajitoa fahamu
Njaa haina chama, kwa hiyo njaa iliyotuchapa kwa miaka mitano itatufanya tusiipe kura CCM. Wale mataga wa ngazi za juu ndio waliofaidika mno maana wana majumba ya kifahari na magari ya kifahari. Ila wale wa ngazi za chini hawawapi kura ccm.
 
Ni kweli kabisa ndio maana mnashirikiana kusomba watu na wanafunzi kwenye maroli. Huu umoja na mshikamano wa usombaji ni dalili njema kwa chama.
Umati wa watu unaomsubiri barabarani Raisi wa mioyoni mwa Watanzania huwa wanasombwa na nani kuletwa hapo
 
Njaa haina chama, kwa hiyo njaa iliyotuchapa kwa miaka mitano itatufanya tusiipe kura CCM. Wale mataga wa ngazi za juu ndio waliofaidika mno maana wana majumba ya kifahari na magari ya kifahari. Ila wale wa ngazi za chini hawawapi kura ccm.
Huko unapopaita ngazi za chini ndio kuna mamilioni ya kura za CCM sasa
 
Umati wa watu unaomsubiri barabarani Raisi wa mioyoni mwa Watanzania huwa wanasombwa na nani kuletwa hapo
Unasombwa na madereva wa malori pamoja na wenyeviti wa kamati ya usombaji wa kila kata na wilaya. Pia maagizo kutoka juu kwa waalimu kusomba wanafunzi.
 
Back
Top Bottom