Mwambie mimi ni mwanaume mwenziye ananiumiza

Hakymungu mnanionea,nyinyi
Hivi kusema kwamba nawewe ulikuwa huna baba ambaye ni mwanaume kama mimi, je mama yako angamfanyia haya haki si angekufa kwa presha ujanani tu yule mzee??

Au huyu mwanaume uliyenaye hajui kwamba namimi ni mwanaume mwenzie na kibaya zaidi nlipitialo mimi nayeye anaweza kulipitia mbona anacheza mchezo usio wa kiungwana na wa ovyo kama choo cha walevi.

Nmezoea kuyaona tu kwenye video ila mbona hata mimi leo yamenikuta,?

Muda mwingine natamani nikusahau lakini siwezi,
Halafu nikukumbushe tu kwamba kuMove on ni kawaida sana nishafanya mara kadhaa huko nyuma kwenye mahusiano kadhaa wa kadhaa lakini sasa hivi naogopa nitampata wapi mwingine kama wewe?? Ambaye kidogo alikidhi vile vigezo vichache nilivyovitaka wife material?

Si unajua kwako nlijifunza namna ya kupenda baada ya kuwasulubu mabinti kadhaa huko nyuma au ndio malipo yangu hapa hapa duniani???

Basi kama kupenda ni dhambi mie basi Nimuombe tu Mungu wangu aniwie Radhii.

Wanasema huwezi kukimbia kile unachokipenda sana,

Mama nikukumbushe kitu kingine kuna wenzako wengi wanalia kwa kudhani mapenzi ni pesa .
Au shida ni ipi au ulimkubali kwa sababu yeye ni mtu mzito hapa TZ katika Wizara X

Lakini mbona umesahau huyo ni kiongozi na mkewe anajulikana nchi nzima na bado ukajiweka kwake kama mzoga wa mbuzi kwa muuza bucha.

Au uliogopa kutenguliwa na ukakubali tu ilimradi vyeo vyako vipande mithili ya mpanda ghorofa??

Wanasema mfa maji haishi kutapatapa Mama,

Nakumbuka ulinisifu mimi ni mwanaume pekee ambae niliweza kukufikisha mara nyingi kule kileleni mlimani kilimanjaro ipasavyo ukawasalimu na waChaga mara nyingi uwezavyo eti Shimbooni shafoo.

Ukawa unantania nmeweza hayo yote eti kwasababu kazi yangu ni kutibu binadamu, hivyo nlikutibu na wewe haswaaa....

Mara nyingine ukasifia eti watu wa mwambao ndivyo tulivyo... ukawa unafurahi sana hata nuru ilianza kuonekana kwenye wajihi wako mzuri na hasira za pasi na sababu zilianza kukutoka Dada wewe.

Muda mwingine ulijilaza kifuanikwangu huku ukiwatukana wale wote waliokupaka shombo la samaki wa feri mwanzo eti kama mimi hujaniona,
popote duniani... na muda huo tupo tukitazama , mechi za Uefa ukamtukana mpaka Ronaldo " Eti mwanaume gani hafugi hata Ndevu"

Ukataka uiombe na selikari iniwekee ulinzi mara sijui inipeleke mbali na upuuzi upuuzi mwingine wa kike unaofariji kama yule binti wa mzanzibar mnamwita Zuchu , si ni wewe yule??

Sasa shida nini , umependa tu uwe na mahusiano na mtu X kwasababu ana mamlaka hapa TZ.

Mbona nlijisemea nmepata ninapopataka , relation with no gender roles, we both hustlers, we both cook, and we both pay ,msichana ambaye uliyaweza yote kwa upendo wa dhati pasi na kifani sio yule goli kipa wa kuomba omba kila leo., akisubiri aletewe

Si ni wewe ulinipa ushauri tufungue goli la bidhaa mbalimbali na nikiri kutokana na usimamizi na akili zako madhubuti project imefika mbali
Sasa hizo akili zako zilishindwa kukuzuia vipi usitumike ??
Au, muda unatongozwa uliziacha kwenye pochi yako ile nene nyekundu ama laa???

Si ni wewe uliforce nikupeleke nyumbani wakujue kwamba ndiyo mke mtarajiwa , ni wewe ndiyo??

Si ni wewe uliforce mwaka jana nikupe Ujauzito familia tuianze mapema , lakini nlikukatalia na kukwambia tujipange kwanza na itapendeza mtoto akizaliwa tukiwa tayari ndoani., kutokana na taratibu za dini yetu

Au kwakua umenizidi kipato , ukikaa kwenye kompyuta masaa 6, na kurudi nyumbani na mwisho wa mwezi fungu nene kwenye akaunti yako? ..
kuliko sisi ambao mpaka tupigane sana ., tuchane chane miili ya watu tuokoe maisha yao usiku na mchana ili tonge lifike mdomoni.

Na nmekwambia kabisa ,kama imeshindikana basi kila mtu afunge furushi lake apite zake.. lakini kumbuka vile huwa unalia lia na kugoma ukataka hata kujidhuru na madawa, kisa tu kukwambia tusitishe safari yetu ya Huba , na ukasema hakuna zaidi yangu kila idara lakini ukasema utaachana na kigogo wako punde, ila imepita miezi mitatu bado unaogopa ata kumtakia hata.

Kweli we ndiye nikupendaye ila nawezaje kuoa mtu ambaye tayari analiwa kwingine kama nyani ashambuliaye mahindi baada ya mwenye shamba kupitiwa na usingizi, huku nikitambua fika.,

Nikasema tuwaite dada zako na wazee kadhaa ili tujue mustakabali wetu ukakataa katakata ukasema bado unanipenda sana na unawatangazia na kuwahakikishia nduguzo kwamba ndoa yetu iko pale pale.

Haya mapenzi mi nishayaghairi mama, lakini bahati mbaya kila nikikuangalia jinsi unavyojiliza na kunikumbusha mambo kadhaa wa kadhaa nakuonea na huruma, sura yako haikupendezi ukiwa katika wimbi la masononeko we ni mzuri zaidi ya neno lenyewe.

Kupendana kwa dhati is not easy, mbona hujawai nionesha dharau hata siku moja ,
Heshima ya mapenzi iko palepale, ila kosa ni kwanini nimejua, kama kuna mume mwenzangu??,

Muda mwingine haujali hata ,mnatumiana mpaka voice notes ukiwa nami ukidhani nmelala siyo, unamwita sweetheart mara baby, mzee kama yule mwenye kitambi kama mkoba, umri wa babu yako mzaa babu yako??

Mama tufanye iwe mwisho tu.
Tusiendelee.

Hizo sio mila na desturi za kwenu kabisa mama yako ,amekusifu mara tele , sana kila nihudhuriapo pale nyumbani kwenu, kumsabahi na kumpelekea vijifurushi vya nafaka kama apendavyo, na umekataa kulisuluhisha hili kwake kwasababu waogopa fedheha .
Mwanamke gani wewe usiyetongozwa ukakataa.??

Lakini wala siamini kama ni wewe??
Huenda si wewe kuna kiumbe cha hovyo toka choo cha makahaba kimekuvaa

Je ningekuwa mimi ungenielewa kweli ?
Si huwaga unalia hadi midomo yako hutetema mithili ya mgonjwa kifafa si ni wewe yule??

Muda mwingine tukiwa nyumbani unanilaghai tu , eti mimi wako peke yako ,

Si ulimwambia kwamba mimi ndimi mpenzi wako ukamtajia na kazi niifanyayo, ukamwonyesha na taswira ya picha yangu., ukanidhalilisha weee , ukabadilisha aina ya gari mimi nikajua ni achievements zako kama vicoba vyako unavyoendeshaga na wanawake wenzio kule kwenye chama vimekuwezesha , kwasababu weledi wako haupimiki ni tofauti na wanawake wengi niwajuo.

Kibaya zaidi hata dereva wa huyo kigogo wako kashakuonja uroda tayari, sijui alikutisha nini , ukamtunuku mwili wako wa thamani au kwakuwa nayeye ana nyadhifa fulani.. sijui hata huyu kigogo atawafanya nini akija kujua au pengine nikuulize swali la mwisho hivi umerogwa siku hizi au??

Mimi sina shida nao hao mafedhuli wenzio wenye madaraka ila nikufahamishe tu kwamba hata la huyu dereva wa kigogo uliemtunuku mwili ,nayo nililijua

IKIWEZEKANA MKUMBUSHE MIMI NI MWANAUME MWENZIE.
... Mmemuelewa?......
 
Back
Top Bottom