Mwambie mdogo wako anaenda shule kusomea taaluma sio kazi, anaweza kusoma uhasibu akawa dobi

Aug 9, 2018
95
293
1. Mwambie anaenda kusomea taaluma sio kazi. Anaweza kusoma uhasibu akawa dobi.

2. Mwambie Kufaulu Taaluma sio Kufaulu maisha.

3. Mwambie Kupata alama nyingi sio kujua mambo mengi.

4. Mwambie akifika chuo atakutana na watu wa mikoa tofauti na hata majiji. Ila akumbuke anatokea Mtwara, tena kule ndanindani.

5. Mwambie Marafiki wa chuo hubadilika kila baada ya semester. Kuendelea kung'ang'ania wale wa awali ataisoma namba.

6. Mwambie semester1 atakuwa na wapenzi wengi sana ila atumie kinga kwa gharama yoyote ile.

7. Mwambie makundi makundi chuoni humaliza hundi mfukoni.

8. Mwambie Boom huwa linakuja ila Laki5 ya chuoni sio Laki5 ya nyumbani.

9. Mwambie chuoni atakutana na semina mbalimbali za ujasiriamali ila chaajabu kila mtu anauza ubuyu na kalamu. Ajaribu bahati yake.

10. Mwambie ajiandae kupokea lawama na hata kuachana na yule mpenzi wake aliyemwacha nyumbani.

11. Mwambie wahadhiri (Lecturers) wa kitanzania wanajua kila kitu na wako juu ya sheria hivyo kama ni wa kike ajifunze kusali.

12. Mwambie Chuoni kuna Makanisa na Misikiti. Wanafunzi ni zaidi ya 1000 lakini waumini ni wachache. Akumbuke kusali.

13. Mwambie kama ni wa kike,marafiki zaidi ya 3 hatoweza kudumu nao. Watagombana tu.

14. Mwambie kwa "Kapuku",kila mtu huwa anataka kuwasaidia wazazi awapo chuoni lakini kuna nyakati inakuwa nje ya uwezo wetu.

15. Mwambie Simu na nguo za gharama ni muhimu lakini sio lazima.

16. Mwambie marafiki wanaokuwa naye kipindi hana hela asiwasahau.

17. Mwambie chuoni ni sehemu ya kutengeneza Connection na watu muhimu.

18. Mwambie zile bata alizokuwa akiskia zikibadilika asishangae.

19.Mwambie pia baada ya kumaliza chuo haina maana amewin maisha. Hapa ndipo msoto mpya unapoanzia.

20. Mwambie Maisha ni mafupi sana Adumu kumcha Mungu na kufanya mambo mazurii, Lastly Asimdharau mtu yeyote.

Over
 
Nahisi ni Yeye maana si kwa uzuri huu,Amosi where U?
 
Weka kwenye sauti Mkuu,nice Message.

....that is true laki tano ya chuo hasa ya boom sio pesa kabsa ndani ya mwez 1 au 2 unakuwa mweupee peee,sijui zina nn zile pesa aisee..
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom