Mwambe: Tumuache Rais Samia, anafahamu wapi atafikisha Nchi yetu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,268
2,000
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Geoffrey Mwambe amesema anatamani wale wanaojaribu kutoa ushauri wa hapa na pale kuhusu nini Rais afanye wampe nafasi afanye kazi yake. Ameeleza hayo leo Bungeni Dodoma

Amesema, "Anaifahamu kazi yake, alikuwepo kwenye kupanga mipango na yeye ni sehemu ya mipango hii tunayotekeleza kwa sasa. Mimi ningependa kushukuru kwa ushauri lakini tumuache Rais. Anafahamu wapi atafikisha Nchi yetu"
 
mwamba_ngori

JF-Expert Member
Aug 31, 2019
222
250
π‘—π‘Žπ‘šπ‘Žπ‘› π‘ π‘œπ‘šπ‘’π‘‘π‘–π‘šπ‘’ π‘‘π‘’π‘€π‘Žπ‘Žπ‘β„Žπ‘–π‘’ π‘€π‘Žπ‘˜π‘’π‘π‘€π‘Ž π‘šπ‘Žπ‘Žπ‘šπ‘’π‘§π‘– 𝑀𝑒𝑛𝑦𝑒𝑀𝑒.....ΰΌ†ΰΌ†
 
Freddie Matuja

JF-Expert Member
Jul 21, 2018
1,171
2,000
Mfalme Nebkadnezer wa Babel alikuwa na washauri mashuhuri wenye weledi kwa nyakati hizo; yet akahitaji wasaidizi wake wamtafutie new blood kutoka kwa vijana kama "think tank"

Ukifuatilia simulizi za biblia utaona Meshack, Shadrack, Abednego na Daniel ndipo nao wakawa moja ya tranees wa kuja kumtumikia mfalme.

Nadhani sio sawa watu kuzibwa midomo maadam tuna vichwa na vinafikiri.

Sio vibaya Rais kupewa ushauri, na nadhani ni makosa walio kwenye uongozi kututaka tukae kimya. Hata JPM tulimshauri kwa namna moja au nyingine. Rais atakuwa na utashi wa kukubali au kukataa mashauri tunayotoa Watanzania kupitia platform mbalimbali.

Eneo pekee tunajua hatuwezi ni kumshinikiza Rais, labda asiwe mtenda hak ndipo tunaweza kushinikiza haki itendeke.

Rais ni muajiriwa wa Watanzania na analipwa mshahara na posho kwa kodi za Watanzania, Watanzania hawana Rais mwingine zaidi ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na ni vema wakamshauri.

Yeye awe na maamuzi achukue ushauri upi na upi auache.

Wakati mmoja JPM alikaa na watu wa madini kwa nyakati tofauti akaketi na wafanyabiashara wa level za kawaida; akashauriana nao na kuja na mapendekezo amboyo yalikuwa na tija kwa Watanznia.

Mungu mkuu mwenye uwezo wote kaweka wazi kwenye biblia na amemtaka mwanadamu aende na washaurine; "come and let us reason together"

Tumshauri madam President Samia Suluhu Hassan kwa staha. Ni haki yetu kikatiba kumshauri kama muajiriwa wetu. Tusimshinikize.

Na kama itawezekana Rais Samia atafute think tank nje ya circle ya utawala; anaweza kuwa na parallel system ya think tanks; hawa watampa ushauri bora unlike immediate subordinates;

Hawa watampa all materials facts kwa maslahi ya nchi, immediate subordinates watashauri kwa woga kulinda ugali.

Tumshauri Rais wetu kwa staha.

Freddie
 
Kumbisalehe

JF-Expert Member
Nov 25, 2014
717
1,000
Ni vitu vya ajabu kila mtu akijiskia tu anaandika au kusema kuwa anashauri Rais afanye hiki au kile. Hii tabia ya ovyo kabisa. Rais ni taasisi ina watalaam wa kila eneo. Mbona Mbona Magufuli au Kikwete hapakuwa na hizi kelele?

Ifike mahali ujinga usijidhihirishe sana. Anajua kazi yake na ana team ya wataalam wa kila aina. Tufanye kazi kila mtu eneo lake shambani, ofisini, kiwandani au katika biashara, hiyo ndio namna ya kulisaidia taifa. Hasa kwa kulipa kodi.
 
Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
89,989

Hakuna ubaya watu kutoa maoni yao!

Uhuru wa maoni ndo uhai wa demokrasia.
 
Benny Haraba

JF-Expert Member
Dec 7, 2012
7,034
2,000
Lazima tumshauri, nchi siyo kampuni binafsi ,lakini Rais kama taasisi asikurupuke kuufanyia kazi kila ushauri, maana hata humu tunaona wanaoshauri wengine hamna kitu 'a Country is not a Company'
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
107,462
2,000
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Geoffrey Mwambe amesema anatamani wale wanaojaribu kutoa ushauri wa hapa na pale kuhusu nini Rais afanye wampe nafasi afanye kazi yake. Ameeleza hayo leo Bungeni Dodoma

Amesema, "Anaifahamu kazi yake, alikuwepo kwenye kupanga mipango na yeye ni sehemu ya mipango hii tunayotekeleza kwa sasa. Mimi ningependa kushukuru kwa ushauri lakini tumuache Rais. Anafahamu wapi atafikisha Nchi yetu"
Mwambe naye ni chumia tumbo tu hana lolote lile zaidi ya kuendeshwa na njaa tu
 
Bondpost

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
4,129
2,000
Lazima tumshauri, nchi siyo kampuni binafsi ,lakini Rais kama taasisi asikurupuke kuufanyia kazi kila ushauri, maana hata humu tunaona wanaoshauri wengine hamna kitu 'a Country is not a Company'
I would say, a country is not a personal property.
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
13,534
2,000
Mbona walikuwa hawamshauri hivyo jiwe?
Lazima tumshauri, nchi siyo kampuni binafsi ,lakini Rais kama taasisi asikurupuke kuufanyia kazi kila ushauri, maana hata humu tunaona wanaoshauri wengine hamna kitu 'a Country is not a Company'
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom