Mwambe: TRA igawanywe na kila Idara ijitegemee kama ilivyokuwa awali yaani Income Tax Dept, VAT Dept na Customs

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
63,651
95,979
Mbunge wa Masasi aliyewahi kuwa Waziri wa Biashara na Uwekezaji mh Mwambe amesema mifumo ya sasa ya TRA siyo rafiki, imejaa Uonezi na ni Sumbufu.

Mwambe amesema hii inatokana na kila mmoja pale TRA kujiona anajua kila Kitu hali inayopelekea usumbufu mkubwa kwa Walipa kodi na hata miongoni mwa Wafanyakazi wenyewe.

Mwambe amependekeza TRA igawanywe na iwe na Idara zinazojitegemea kama ilivyokuwa awali kabla ya Sanare.

Idara hizo ni Income Tax, VAT Dept na Customs.

Mh Mwambe alikuwa anajadili Ripoti ya CAG.

Chanzo: TBC
 

KingCobra95

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,150
3,095
Akiambiwa atetee kisomi hii hoja kwa maandiko na tarakimu ataweza? Au kaongea tu ili mdomo usinuke. Sababu sielewi ikigawanywa hao waonevu nao hawatagawanywa?
 
3 Reactions
Reply
Top Bottom