Mwalimu wa madrasa ahukumiwa miaka 80 jela kwa kumbaka binti wa miaka 15

Mahakama ya mkoa Mwera imemhukumu Mussa Nassibu Ismail (21) ambaye ni Mwalimu wa madrasa Kiboje wilaya ya Kati, mkoa wa Kusini Unguja kutumikia miaka 80 jela na faini ya shilingi milioni 3 kwa kosa la kushindwa kujizuia matamanio yake na kumbaka na kumtorosha mtoto wa kike mwenye miaka 15.

Akitolea ufafanuzi wa kesi hiyo Hakimu wa Mahakama hiyo Said Hemed Khalfan chini ya Mwendesha Mashtaka wa Serikali Shumbana Mbwana, amesema kuwa mtuhumiwa alifanya makosa ya kumbaka na kumtorosha mtoto huyo kwa siku mbili tofauti kati ya Oktoba 18, 2019 na Novemba 2 mwaka huo huo majira ya saa 3:00 asubuhi na saa 9:00 alasiri wakati mtoto huyo akiwa katika mazingira ya madrasa huko Kiboje.

Akisoma hukumu hiyo kwa mtuhumiwa Hakimu Khalfan amesema kuwa mtuhumiwa alikuwa anakabiliwa na mashtaka manne, ambapo mashtaka mawili yalikuwa ni ya kubaka na mengine ni ya utoroshaji.

Baada ya Mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka Hakimu amesema kufuatia adhabu namba 6 ya mwaka 2004 ya sheria ya Zanzibar, mtuhumiwa amehukumiwa kutumikia miaka 30 kwa kila kesi moja ya kubaka na katika kesi mbili za kutorosha atatumikia miaka kumi kwa kila kesi na zote atazitumikia kwa pamoja!

Chanzo: EATV
Sasa hivi mahakama za znz zinatenda haki,hawa wasenge ni kuwafunga tu wakaolewa huko gerezani
 
Back
Top Bottom