Mwalimu wa Kanisa ahukumiwa miaka 30 kwa kosa la kulawiti

tyc

JF-Expert Member
Feb 25, 2014
1,179
2,955
Mahakama ya Mkoa wa Kinondoni imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela Elisha Mushi, mkazi wa Ubungo Kibangu baada ya kuthibitika kumlawiti mtoto wa miaka minne kanisani.

Mushi, ambaye alikuwa akifanya kazi ya kufundisha watoto kanisani anadaiwa kutenda kosa hilo Februari 19, mwaka huu katika Kanisa la Embassy Kingdom.

Hukumu hiyo ilitolewa juzi na hakimu mkazi wa mahakama hiyo, Ester Mwakalinga baada ya kuwasikiliza mashahidi saba wa upande wa mashitaka, akiwamo mtoto mwenyewe, mama mzazi pamoja na mchungaji wa Kanisa la Embassy Kingdom aliyekiri kumfahamu mama mzazi wa mtoto aliyetendwa.

Mashahidi wengine ni daktari wa Hospitali ya Sinza Palestina aliyempima mtoto huyo pamoja na askari wa Kituo cha Polisi Osterbay. Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Ester alisema kutokana na ushahidi uliotolewa na mtoto mwenyewe pamoja na vielelezo vilivyowasilishwa, mahakama imejiridhisha pasipo shaka yoyote kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa analotuhumiwa nalo.

“Kutokana na vielelezo vilivyowasilishwa, ikiwemo ripoti ya daktari (PF3) na ushahidi wa mama na mtoto mwenyewe, mahakama imejiridhisha pasipo shaka kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo, hivyo inakutia hatiani kwa kosa la kulawiti,” alisoma Hakimu Ester.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Hilda Kato aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshtakiwa huyo ili iwe fundisho kwa watu wenye tabia ya kufanya vitendo vya udhalilishaji na kikatili kama hivyo katika jamii.

Source: Gazeti la Mwananchi
 
Baada ya kuanza kusoma hapo juu nilishtuka kidogo baada ya kukuta jina linafanana na la baba angu mkubwa. Ila baada ya kuendelea kusoma, nimejiridhisha kuwa sio yeye. Huyo mpumbavu aende na yeye akachumishwe tembele huko segerea ili iwe fundisho kwa wengine
 
Baada ya kuanza kusoma hapo juu nilishtuka kidogo baada ya kukuta jina linafanana na la baba angu mkubwa. Ila baada ya kuendelea kusoma, nimejiridhisha kuwa sio yeye. Huyo mpumbavu aende na yeye akachumishwe tembele huko segerea ili iwe fundisho kwa wengine

Mtu kama huyu dawa yake nae akabidhiwe kwa Nyapala kama wawili ashughulikiwe kwa muda wa miezi minne
 
Ila kiukweli Tuition, Sunday Schools na Madrasa hizi sehemu ni za kuziangalia kwa makini sana.

Huko watoto wetu wanafanyiwa mambo mabaya ila hawasemi kwa kuogopa.

Wazazi tuwe na tabia za kupeleleza na kuwauliza watoto maendeleo yao ya huko wanakoshinda.
... tuition mwalimu amfundishe mtoto nyumbani; Sunday school nenda na mtoto kanisani wanakuwa na sehemu yao ibada ikiisha rudi na mwanao. Ukimwacha azurure kama kuku wa kienyeji uwezekano wa kufanyiwa ukatili ni mkubwa.
 
Back
Top Bottom