Mwalimu: ukiwa mkubwa unapenda kuwa nani. Mwanafunzi- napenda niwe Fisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwalimu: ukiwa mkubwa unapenda kuwa nani. Mwanafunzi- napenda niwe Fisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by dosama, Mar 14, 2012.

 1. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Sio utani ni kweli mwalimu mwenzangu kamuuliza mtoto wa chekechea ukiwa mkubwa unapenda kuwa nani mf; daktari, mwalimu, mcheza mpira nk cha ajabu mwanafunzi kamjibu anataka kuwa FISADI.

  Katika kumhoji vizuri amedai kila siku kasikia fisadi wanahela na wanaishi vzr kwa hiyo nae anasoma ili awe fisadi
   
 2. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Yupo pia mtoto wa chakechea anasoma na mwanangu aliwahi kuulizwa akasema anataka kuwa jambazi. Mtoto huyu aliwahi kufanya mambo ya ajabu ikiwemo kuiba vitu vidogo vidogo vya wenzake darasani lakini pia kuwapiga wenzake na kuwaumiza. Nilipopata mashitaka ya kupigwa mwanangu nikaenda kujua kulikoni kwa mwalimu wa darasa ndipo akanisimulia kisa cha mtoto huyo kutaka awe jambazi atakapokuwa mkubwa.

  Pengine watoto wanavutiwa na vitu vinavyotokea wakati wa zama zao au matukio ya mara kwa mara katika jamii bila kujali kwamba wanaelewa kwa kina kile ambacho wanakitaka katika maisha yao ya baadaye
   
 3. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  Hivi hii nayo ni SIASA!? na inastahili kuwa kwenye jukwb hili.
   
Loading...