#COVID19 Mwalimu sichomwi chanjo ng'o na wakibadilisha utaratibu kuwa lazima basi nitakuwa tayari kuacha hata kazi

Kuna watu wanapenda sana sifa kupitia wenzao sasa nasema rasmi hapa wazi kabisa sitakubali kuchomwa sindano ng'o (maana mmesema ni hiari)

Na hata kama mkibadili gia angani (na kufanya ni lazima kwa makundi fulani- ambapo kivyovyote walimu wataingia) basi nitakuwa radhi kuacha kazi nikafanye mambo mengine tu mtaani

Mmezoea kutupeleka peleka sana ila katika hili binafsi sikubali

Kwa ambao nimewaacha hawajanielewa hapo juu ni kwamba viongozi hawa wa wilayani huku muda mwingine wanatutesa sana na wanapaa sana majina kupitia migongo yetu watumishi

Tunachangishwa elfu tano tano za mwenge kila mwaka tena kimikwara kwelikweli... ila chaajabu mnaambiwa mchango huo ni wa hiari kuonesha uzalendo! Sasa uzalendo gani wa kulazimishwa sijui (Yale yale ya kodi ya uzalendo)

Mnapotekeleza kwa wingi jambo husika basi sifa kwa halmashauri na DC eti basi!
mkuu kwaiyo kutoa elfu 5 ya mwenge wa uhuru kwako unaona shida saaana Mala ngap umechangia harusi na mambo mengine Tena kwa hela nyingi unazalilisha ualimu aisee kua mzalendo kwa nchi yako mkuu

Swala la korona ni sababu zipi zina kufanya uwe na mashaka kias cha kusema bora niache kazi?
Sasa kama ww ndio mtu wa kutoa elimu huko kijijin kuhusu korona daaa aise hii nchi bado tuna safari ndefuuu sana na tutafika tumechoka mnoooo
 
Ukifanikiwa kuacha kazi nitafute nikupe kazi ya ushamba boy ila usije mla mke/binti yangu nami nitakukula X 3 yake.
 
mkuu kwaiyo kutoa elfu 5 ya mwenge wa uhuru kwako unaona shida saaana Mala ngap umechangia harusi na mambo mengine Tena kwa hela nyingi unazalilisha ualimu aisee kua mzalendo kwa nchi yako mkuu

Swala la korona ni sababu zipi zina kufanya uwe na mashaka kias cha kusema bora niache kazi?
Sasa kama ww ndio mtu wa kutoa elimu huko kijijin kuhusu korona daaa aise hii nchi bado tuna safari ndefuuu sana na tutafika tumechoka mnoooo
Uzalendo kuchangia mwenge??
Nini faida za mwenge??
Mm ningekuwa mwalimu hata senti moja siwezi toa kwenye issue ya kijinga.
Nikichangia harusi naenda kula na kunywa je nikichangia mwenge naenda kupata nini?
Mwenge ni kwa ajili ya mapopoma.
 
Chanjo huchanjwi je vidonge vya HIV/AIDS ?
VP dawa za TB ?

vp chanjo za watoto wachanga...?
Huyo Ana akili timamu ndio Mana kaweka msisitizo kwenye chanjo ya UVIKO 19,

Najua Kuna chanjo nyingi ila hi chanjo ya hati ya dharura chomeni nyie mnaoitaka

Nasisitiza Uhuru wa mtu uheshimiwe
 
Back
Top Bottom