Mwalimu Nyerere: Urais ni mzigo

Waziri kivuli

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
2,987
3,450
Mwalimu aliwahi sema urais ni mzigo kwa mtu yeyote mwenye nia njema!Akasema ukipita mahali ukaona wananchi wana dhiki na njaa,unashika tama huku ukijisemea kimoyo moyo kuwa huu ni mzigo wangu!
 
Jk akasema Urais ni Kazi Ngumu sana na anatamani Siku ziishe akapumzike tukamuita Kilaza
 
Aaah, ilikuwa zamani mzee wangu. Ukifufuka leo unaweza ukafariki jumla na husitamani hata kuiona Tanzania. Huyu wa leo anasema kila raia abebe msalaba wake, hata kama amezaliwa leo. Na tunapoelekea watoto walio katika matumbo ya mama zao watakuwa wanauliza wapo wapi kabla hawajazaliwa?
ikitokea wakajua ni Tanzania basi watabaki kwenye matumbo ya mama zao mpaka jamaa atoke Madarakani.
 
Na Rais Magufuli ameubeba huo mzigo kama Mwl ulivyosema kila akipita huko na huku ni shida tupu na amekuwa akionyesha njia ktk kutatua matatizo mbalimbali ya wanainchi ktk ziara zake.

Tumeona alipokwenda Uwanja wa ndege JKN, Muhimbili,Bandarani,TRA,Mwanza na sasa yuko Shinyanga,Dodoma,Singida,Kagera n.k
 
Mwalimu aliwahi sema urais ni mzigo kwa mtu yeyote mwenye nia njema!Akasema ukipita mahali ukaona wananchi wana dhiki na njaa,unashika tama huku ukijisemea kimoyo moyo kuwa huu ni mzigo wangu!

Hiyo kazi watu huitaka sana pasipo kujua MIZIGO, MAAMUZI na magumu YANAYOAMBATANA na urais yanakutegemea wewe.
Hii ikiwa ni pamoja na kukosa UHURU wako binafsi na hivyo huwezi kwenda kumsalimia shangazi ama mjomba utakavyo.
Hii kazi si rahisi.
Obama aliingia ofisini akiwa na nywele nyeusi sasa hivi kichwa kimejaa nywele nyeupe sababu ya STRESS ya kazi za urais. Mwingine ANAKUSOA, Mwingine HAKUPENDI ni stress tupu.
MZIGO.
 
Mwalimu aliwahi sema urais ni mzigo kwa mtu yeyote mwenye nia njema!Akasema ukipita mahali ukaona wananchi wana dhiki na njaa,unashika tama huku ukijisemea kimoyo moyo kuwa huu ni mzigo wangu!
Si ndio maana tunamshangaa Lowassa kutumia gharama kubwa na nguvu nyingi kutafuta Urais!! Anakimbilia nini kule mpaka analazimisha kuwa Rais kwa namna yoyote ile??? Huyu ni wa kuogopwa kama Ukoma!!
 
Si ndio maana tunamshangaa Lowassa kutumia gharama kubwa na nguvu nyingi kutafuta Urais!! Anakimbilia nini kule mpaka analazimisha kuwa Rais kwa namna yoyote ile??? Huyu ni wa kuogopwa kama Ukoma!!
Nami najiuliza,kuna nin ikulu mpaka watu wagombee hivyo?Wengine mpaka masamasoti na push up ili tu wafike huko!
 
.......Urais mgumu sanaa.....naona wengine wanakimbia majukumu yao wanaendelea ubabe usio na busara! Suala la ukame na njaa kusaidia jamii ni jukumu lake kabisa ila amewageuka wananchi anawaona wapuuzi wameshampa urais wabebe misalaba yao wenyewe!! Tusije tukarudia kosa!!
 
Uraisi ni Mzigo
Cha ajabu Lowassa, Aliona ni Keki ile hadi akahama Chama, dk ya 90 ya mchezo.
Alifikia hatua ya kutanua kama magari barabarani baada ya kuona kapigwa chini CCM. Akaukatizia denge urais.

Zile clip za video za Mwalimu Nyerere zitawasaidia watanzania mpaka wale wa mwaka 2085.
 
Back
Top Bottom