Mwalimu Nyerere Ni wimbo au tunamfuata?

FAHAD KING

JF-Expert Member
Sep 14, 2017
301
373
Kutoka mwandiko wa dhahabu wa Padre Privatus karugendo
Cc:Mwananchi 2016

Editing:Kwa baadhi ili kuleta uhalisia wa tarehe

Ni mwaka jana tu (October 14:Miezi miwili iliopita) tumetoka kwenye kumbukizi ya miaka 20 ya kifo cha Baba wa Taifa letu,Mwalimu Nyerere apumzike kwa amani. Kwa asilimia kubwa,Watanzania wengi wanamkumbuka Mwalimu na kumlilia na kuimba sifa zake. "Kama sio juhudi zako nyerere ...."

Ni watanzania wachache sana wenye matatizo yao ambao wanampiga madongo mwalimu.Sifa za mwalimu ni Wimbo wa kila siku.Viongozi wa serikali wakitafuta kukubalika kwenye jamii,wanalitumia jina la Mwalimu. Vyama vyote vya siasa vikitaka kukubalika kwenye jamii na kwenye siasa zao vinalitumia jina la mwalimu.

Wapinzani wanaipiga vita CCM,lakini huwezi kuta wala kusikia wanampinga vita Mwalimu ambaye ndo mwanzilishi wa CCM.Hawaipendi CCM lakini wanampenda Mwalimu na wanaimba sifa zake

Sasa najiuliza pamoja na kuwauliza watanzania wote.Tunampenda na kumkumbuka Mwalimu na mambo yake au tunabaki kuimba tu sifa za Mwalimu Je,sisi ni wafuasi wa Mwalimu?

Ni wazi kwamba kuna mambo ya Mwalimu ambayo tuliyazika akiwa bado hai.Ujamaa na Azimio la Arusha, vilizikwa Zanzibar. Mavazi ya Mwalimu, yalitupiliwa mbali alipoondoka madarakani.Suti za kimagharibi zilitawala na kuwa kama ushuhuda kwamba wakoloni walitutawala mpaka kwenye akili zetu.Daima tufanane nao kwa kila kitu hadi Mavazi.Tuongee lugha zao,tusomee kwenye shule na vyuo vyao,tuweke pesa zetu kwenye mabenki yao na tuwaruhusu kuja hapa kwetu kuwekeza na kuchota rasilimali zetu kwa faida kiduchu.Wapo wachache ambao bado hadi leo hii wanavaa suti za Mwalimu zile za kichina au Kaunda suti.

Jina la Mwalimu, linatumika kwa mema na mabaya.Wengine wanalitumia kujinufaisha na wengine wanalitumia kujenga jamii iliyo bora na imara.Kuna wanao litumia jina la Mwalimu, ili wakubalike kwenye jamii.Vyovote vile ni kwamba swali ambalo ambalo mtu anaweza kujiuliza ni je,sifa hizi za Mwalimu zinabaki kuwa nyimbo za kuburudisha masikio na mambo yanaishia hapo au tunamfuata? Je, sis ni wafuasi wa Mwalimu? Ni wangapi wanafanya na kuyaishi matendo ya Baba wa Taifa letu?


Mwalimu alipigania uhuru na umoja wa Afrika nzima.Akafanya Tanzania kujilikana kama Kisiwa Cha Amani kwa kupigania Amani.Leo hii Tanzania imekuwa mstari wa mbele kuwafukuza wahamiaji,ambao wamebatizwa jina la wahamiaji haramu.Inasikitisha kuona kwamba hata watu ambao Mwalimu aliwapatia uraia kwa sababu ya sura zao kufanana na zile za nchi jirani,basi wanatuhumiwa kuwa wahamiaji haramu.

Ni wazi kuna mambo mengi ambayo tunafanya kinyume na Mwalimu.Mfano sisi tunawafukuza wahamiaji haramu,wakati Mwalimu alikuwa ameifanya Tanzania kimbilio la kila Mwafrika hata na wengine nje ya Afrika

Kivp waafrika wenzetu wanaitwa wahamiaji haramu wakati Afrika ni kwao?Tumetupilia mbali matendo ya Mwalimu

Mwalimu hakuwa na ushabiki wa vyama vya siasa kama ilivyo sasa.Alikataa katika maisha kufanya siasa za kufungamana.Lakini sisi ukiwa upinzani ikawa na urafiki na CCM,Vyama vya upinzani vinakuona wewe ni msaliti.

Pia CCM hawataki kusikia mwanachama wao ana urafiki na upinzani hata kama ni mgonjwa,ukitembelea wewe ni msaliti. Yeye hakutanguliza chama chake cha siasa,dini yake na wala hakutanguliza kabila lake.

Mwalimu hakutumia hata mara moja lugha za mipasho.Mfano "watawezaa. ..", "CCM ina wenyewe...." "CCM nambari one " na mengine yanayofanana na hiyo.Kwa Mwalimu wazee wetu walisikia "Mvua za kwanza ni za kupandia" "Siasa ni kilimo","Inawezekana timiza wajibu wako...."

Daima Mwalimu alitumia lugha ya kuwaunganisha si ya kuwatenganisha watanzania.Ni bahati mbaya siasa zetu za leo zimetawaliwa na lugha ya mipasho.Ambazo wa kwa kiasi kikubwa zimetutenganisha watu badala ya kutuunganisha.Pia zimejenga chuki.Ndio maana tunauliza ni kwanini tunaendelea kuimba sifa za Mwalimu kama tunafanya kinyume?

hakukipenda chama chake? Au hakuunga mkono sare hizo kwa vile vinachochea ushabiki? Au kuna mtu anajua sababu atueleze? Kwa nini Mwalimu, hakuvaa sare za CCM?.Yeye alikuwa mwenyekiti wa CCM lakini hakuvaa sare za CCM.Jambo la kushangaza ni kwamba baada ya Mwalimu,waliomfuata walianza kuvaa sare za chama Chao. Na kwa vile hadi sasa mwenyekiti wa chama kinachotawala ndiye Raisi wa nchi l,basi tunashuhudia Raisi wa Nchi akiwa kwenye sare za chama chake

Mwalimu, hakuwa na ushabiki wa vyama vya siasa. Hatukusikia hata mara moja akisema "tuwachinje wapinzani " au "tukomboe majimbo ".Mwalimu alijenga hoja,alitetea na alifundisha.Mwalimu alikubali majadiliano na kukubali kushindwa kama mtu mwingine alijenga hoja nzito kuliko yake.Kama wapo waliokuwepo watasema ukweli juu ya hili

Leo hii siasa zetu zimetawaliwa ma mipasho,ushabiki na ushindani wa kijinga.Kwa maana kwamba kama mtu wa CCM amejenga hoja yenye mashiko,hoja ya kizalendo kwa nini isiungwe mkono na wapinzani? Au kama mpinzani amejenga hoja yenye mashiko au yenye uzalendo,kwanini asiungwe mkono na CCM?Kupinga hoja ya mtu bila kutoa hoja ya msingi kumpinga kwa kisingizio cha kutokuwa kwenye chama kimoja cha siasa,ni ushindani wa kijinga. Pia ni dhambi kuendelea kuimba sifa za Mwalimu wakati tunaishi na kufanya kinyume.

Mwalimu hakujilimbikizia mali lakini viongozi wetu wa leo ndo wa kwanza kufanya ufisadi.Mikataba feki,unyonyaji wa kodi za wanyonge na kutukomeza haki za kibinadamu. Watoto wake Mwalimu walisoma shule za ndani lkn vp wanafunzi wa viongozi wa leo?

Ni bahati mbaya kwamba tumebakia kumsifia Mwalimu kwenye nyimbo na kuweka pembeni matendo yake. Inasikitisha kuona nyuma yetu tunaacha kizazi cha mipasho,ushabiki na ushindani wa kijinga.Vijana wetu kama yuko CCM hataki kusikia chochote upande mwingine.Au kijana kama yuko upinzani hayupo tayari kusikia lolote la CCM au la chama kingine

Tukitaka kufanikiwa kama taifa,tuache utamaduni wa kuimba sifa za Mwalimu kwenye midomo yetu.Tuache utamaduni wa kuhubiri maji na huku tunakunywa mvinyo.Tumfuate Mwalimu. Tuache ushabiki wa kisiasa, tuache utamaduni wa kuvaa sare za Vyama vya siasa,tuache utamaduni wa kufungamana,tuache ushindani wa kijinga.Tushirikiane kulijenga Taifa letu kwa kumfuata Baba wa Taifa.

Habari WANA JF

FB_IMG_1578307228444.jpeg
pic+hoja.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa wewe unataka watu wawe watumwa wa Nyerere
Yani tuendelee kuvaa suti za nyerere miaka 20 baada ya kifo chake? Sisi tutakuwa watumwa wake sasa
 
Yale aliyonena na kuyatenda tunaimba tu kama wimbo wa mapenzi kipindi tukiwa tunatongozea!!

Ndivyo wanasiasa wanavyotufanya wananchi!! Wanatuimbia nyimbo ya nyerere wanapokuwa wanayao
 
Vijana, ambao ni wengi. Ambao ndio sisi. Ambao wakati Nyerere anakufa tulikua na miaka 10 kwenda chini...au tuseme 15. Hatuna chochote cha kumkumba nacho huyo Mwalimu.

Aende tu, watu wanamdharau Yesu, Muhammad, sembuse Mwalimu?

Aaah.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni itikadi tu na kila mtu ana zake. Labda mm naweza kumshukuru kwa kuongoza harakati za ukombozi. Na sio kutupa uhuru maana nyuma ya jukwaa la uhuru kuna mengi sana...



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom