Mwalimu Nyerere kwanini alimwambia Mzee Mwinyi maneno haya?

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,291
Habari zenu ndugu zang, ama baada ya salam ningependa kuwaombea heri ya mwaka mpya. Ndugu watanzania wenzangu, historia yetu inatuambia kuwa baba wa Taifa mwl J.K. Nyerere aliiongoza nchi yetu kwa takriban miaka 20 na ushee.

Katika uongozi wake wa kipindi cha miaka tajwa hapo juu, mwl Nyerere alitengeneza misingi ya taifa ambayo ndio inatuongoza mpaka leo kama vile kutengeneza katiba mpya na kuachana na ile ya wakoloni, kuanzisha azimio la Arusha, kuondoa mambo ya udini na ukabila nchini, alileta nidhamu na uwajibikaji ndani ya nchi, alipambana na mafisadi, pia vita dhidi ya maadui watatu wa taifa ambao ni elimu, ujinga na maradhi.

Lkn pamoja na mazuri mengi aliyofanya kwa nchi, pia kuna mabaya yake aliyoyafanya kama vile kuwadhibiti wanaompinga mpaka kufikia hatua ya kina Kambona na wengineo kukimbia nchi, uchumi kuangukia na nchi kuwa ktk umasikini wa kutupa kuliko pelekea kutaka kupinduliwa nk.

Tukija kwa mzee Mwinyi yeye aliikuta nchi ikiwa hoi bin taaban, hazina ilikuwa tupu kiasi kwamba hata kuwalipa baadhi ya wafanyakazi wa serikali mishahara yao ilikuwa ngumu (pengine hii ndio ilikuwa sababu ya lile jaribio la mapinduzi).

Bidhaa muhimu kama vile mchele, unga, sukari, mafuta ya taa na kupikia, sabuni za kuogea na kufulia vyote hivi vilikuwa havipatikani madukani.

Kwahiyo mzee Mwinyi alikuwa na kazi ya kuhakikisha bidhaa hizo muhimu zinapatikana katika maduka, mikoa na maeneo yote nchi nzima kwa kuruhusu watanzania na wale wasiokuwa watanzania kuleta bidhaa hizo nchini ila kwa kufuata sheria za nchi, pia akadhibiti wahujumu uchumi waliokuwa wanapiga hela enzi za mwl Nyerere kwa kuanzisha oparation ''fagio la chuma", maana kuna watu waliokuwa wanajineemesha kupitia system ya ugawaji, yan unakuta kila nyumba mnapewa kilo moja moja ya sukari kwa matumizi ya wiki nzima kwahiyo ukihitaji zaidi ya hiyo kilo moja inabidi umpe au uwape wale waliokuwa wanasambaza bidhaa hela ili akuletee kimya kimya nyumban kwako.

Pia akawa na kazi ya kuhakikisha madawa yanapatikana kwa wingi nchini nzima, vituo vya afya (hospital) zikaongezeka, pharmacy nyingi zikafunguliwa, nguo na viatu vya mitumba na madukani zikaanza kuingia nchini, uchumi ukaanza kuimarika, mishahara ikaanza kulipwa bila mizengwe, hali ya maisha ya kila mwananchi mmoja mmoja ikaanza kubadilika kwa kuwa bora zaidi ya mwanzo, demokrasia ikazaliwa upya nk.

Lakini pamoja na yoyote aliyofanya na yeye alikuwa na mabaya yake kama vile kutokuwa mkali kwa wale wote walioichezea nchi chini ya utawala wake, kuvunja azimio la Arusha nk. Sasa basi nikija katika kiini cha mada hii naanza na hotuba aliyowahi kuitoa baba wa taifa akiilaumu serikali ya mzee Mwinyi kwa kushindwa kurithi mazuri yake, badala yake wakarithi yale mabaya yake. Sasa ninachojiuliza hapa ni mazuri gani hayo ya mwl Nyerere ambayo mzee Mwinyi aliyatelekeza? Na mabaya yapi hayo ya mwl Nyerere ambayo mzee Mwinyi aliyakumbatia?

Mwenye ujuzi wa haya mambo naomba aje atufahamishe vizuri. Lkn pia naomba mada hii isitumiwe kuwachafua wazee wetu waliolitumikia taifa letu kwa nguvu zao na akili zao. Tujadili kwa faida yetu wote hapa JF.
 
Habari zenu ndugu zang, ama baada ya salam ningependa kuwaombea heri ya mwaka mpya. Ndugu watanzania wenzangu, historia yetu inatuambia kuwa baba wa Taifa mwl J.K. Nyerere aliiongoza nchi yetu kwa takriban miaka 20 na ushee. Katika uongozi wake wa kipindi cha miaka tajwa hapo juu, mwl Nyerere alitengeneza misingi ya taifa ambayo ndio inatuongoza mpaka leo kama vile kutengeneza katiba mpya na kuachana na ile ya wakoloni, kuanzisha azimio la Arusha, kuondoa mambo ya udini na ukabila nchini, alileta nidhamu na uwajibikaji ndani ya nchi, alipambana na mafisadi, pia vita dhidi ya maadui watatu wa taifa ambao ni elimu, ujinga na maradhi. Lkn pamoja na mazuri mengi aliyofanya kwa nchi, pia kuna mabaya yake aliyoyafanya kama vile kuwadhibiti wanaompinga mpaka kufikia hatua ya kina Kambona na wengineo kukimbia nchi, uchumi kuangukia na nchi kuwa ktk umasikini wa kutupa kuliko pelekea kutaka kupinduliwa nk. Tukija kwa mzee Mwinyi yeye aliikuta nchi ikiwa hoi bin taaban, hazina ilikuwa tupu kiasi kwamba hata kuwalipa baadhi ya wafanyakazi wa serikali mishahara yao ilikuwa ngumu (pengine hii ndio ilikuwa sababu ya lile jaribio la mapinduzi). Bidhaa muhimu kama vile mchele, unga, sukari, mafuta ya taa na kupikia, sabuni za kuogea na kufulia vyote hivi vilikuwa havipatikani madukani. Kwahiyo mzee Mwinyi alikuwa na kazi ya kuhakikisha bidhaa hizo muhimu zinapatikana katika maduka, mikoa na maeneo yote nchi nzima kwa kuruhusu watanzania na wale wasiokuwa watanzania kuleta bidhaa hizo nchini ila kwa kufuata sheria za nchi, pia akadhibiti wahujumu uchumi waliokuwa wanapiga hela enzi za mwl Nyerere kwa kuanzisha oparation ''fagio la chuma", maana kuna watu waliokuwa wanajineemesha kupitia system ya ugawaji, yan unakuta kila nyumba mnapewa kilo moja moja ya sukari kwa matumizi ya wiki nzima kwahiyo ukihitaji zaidi ya hiyo kilo moja inabidi umpe au uwape wale waliokuwa wanasambaza bidhaa hela ili akuletee kimya kimya nyumban kwako. Pia akawa na kazi ya kuhakikisha madawa yanapatikana kwa wingi nchini nzima, vituo vya afya (hospital) zikaongezeka, pharmacy nyingi zikafunguliwa, nguo na viatu vya mitumba na madukani zikaanza kuingia nchini, uchumi ukaanza kuimarika, mishahara ikaanza kulipwa bila mizengwe, hali ya maisha ya kila mwananchi mmoja mmoja ikaanza kubadilika kwa kuwa bora zaidi ya mwanzo, demokrasia ikazaliwa upya nk. Lkn pamoja na yoyote aliyofanya na yeye alikuwa na mabaya yake kama vile kutokuwa mkali kwa wale wote walioichezea nchi chini ya utawala wake, kuvunja azimio la Arusha nk. Sasa basi nikija katika kiini cha mada hii naanza na hotuba aliyowahi kuitoa baba wa taifa akiilaumu serikali ya mzee Mwinyi kwa kushindwa kurithi mazuri yake, badala yake wakarithi yale mabaya yake. Sasa ninachojiuliza hapa ni mazuri gani hayo ya mwl Nyerere ambayo mzee Mwinyi aliyatelekeza? Na mabaya yapi hayo ya mwl Nyerere ambayo mzee Mwinyi aliyakumbatia? Mwenye ujuzi wa haya mambo naomba aje atufahamishe vizuri. Lkn pia naomba mada hii isitumiwe kuwachafua wazee wetu waliolitumikia taifa letu kwa nguvu zao na akili zao. Tujadili kwa faida yetu wote hapa JF.
Paragraph bas mzee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyerere hakumwambia Mwinyi kwamba hakurithi mazuri yake, karithi mabaya yake.

Nyerere alikuwa anawakosoa Watanzania waliokuwa wanamsema kwa mabaya yake, kwamba hawakuangalia mazuri yake.

Kauli ambayo ilikuwa ya kujipendelea. Rais akifanya mazuri kafanya kazi yake anavyotakiwa.

Katika kumpima rais, lazima mabaya yaangaliwe zaidi ya mazuri.

Ndiyo maana mpaka leo George W. Bush anakumbukwa kwa kuiingiza Marekani katika vita kijinga Iraq, Ingawa alisaidia sana Africa kwenye vita vya Malaria na UKIMWI.

Mkapa kaanzisha taasisi nyingi, kalipa madeni, lakini mpaka leo watu wanamsema kwa mauaji ya Pemba.

Katika jamii ya watu wanaojipanga kufanya vizuri zaidi, mabaya ni muhimu sana kuyamulika zaidi, ili yasirudiwe.

Mazuri ni sehemu ya mambo yanayotegemewa kufanywa.
 
Nyerere hakumwambia Mwinyi kwamba hakurithi mazuri yake, karithi mabaya yake.

Nyerere alikuwa anawakosoa Watanzania waliokuwa wanamsema kwa mabaya yake, kwamba hawakuangalia mazuri yake.

Kauli ambayo ilikuwa ya kujipendelea. Rais akifanya mazuri kafanya kazi yake anavyotakiwa.

Katika kumpima rais, lazima mabaya yaangaliwe zaidi ya mazuri.

Ndiyo maana mpaka leo George W. Bush anakumbukwa kwa kuiingiza Marekani katika vita kijinga Iraq, Ingawa alisaidia sana Africa kwenye vita vya Malaria na UKIMWI.

Mkapa kaanzisha taasisi nyingi, kalipa madeni, lakini mpaka leo watu wanamsema kwa mauaji ya Pemba.

Katika jamii ya watu wanaojipanga kufanya vizuri zaidi, mabaya ni muhimu sana kuyamulika zaidi, ili yasirudiwe.

Mazuri ni sehemu ya mambo yanayotegemewa kufanywa.
Oh hapa nimekupata vizuri mkuu Kiranga
 
Mazuri alimaanisha azimio la Arusha... sikiliza hotuba yote ... alisema anasoma biblia anaona kasoro lakini azimio la Arusha haoni kasoro kabisa
 
Mazuri alimaanisha azimio la Arusha... sikiliza hotuba yote ... alisema anasoma biblia anaona kasoro lakini azimio la Arusha haoni kasoro kabisa
Mkuu,

Ukiambiwa kuna dawa nzuri kabisa ya kuua virusi vyote vinavyosababisha ugonjwa, lakini hiyo dawa tatizo lake moja, inaua virusi vyote mpaka na mgonjwa itamuua.

Hapo utafanyaje? Utaikubali hiyo dawa na kusema ni nzuri kwa sababu itaua virusi vyote?

Hiyo ndiyo dawa aliyotupa Nyerere.
 
Mazuri alimaanisha azimio la Arusha... sikiliza hotuba yote ... alisema anasoma biblia anaona kasoro lakini azimio la Arusha haoni kasoro kabisa
Yeye hakuna kasoro kwa sababu ikulu sukari ilikuwepo, maziwa ya maji/ya unga yalikuwepo, mchele ulikuwepo, unga ulikuwepo, mafuta yalikuwepo.

Sasa huku uraiani hali ilikuwa mbaya mpaka kufikia watu kunywa uji wa chumvi, ugali na mbili nk. Hivyo azimio hilo lilikuwa linatuumiza wananchi wengi na kuwaneemesha viongozi wachache serikalini.
 
Back
Top Bottom