Mwalimu Nyerere: Kuna wanasiasa wanaouza heshima zao kwa sababu ya pesa. Ukiwapa pesa watatukana kweli kweli, wako tayari kusaliti nchi

Nigrastratatract nerve

JF-Expert Member
Sep 4, 2019
1,395
3,899
Hawa watu huwa wanapewa pesa kwa masharti ya kuongea maneno waliyoandikiwa na wafadhili wao.

Hii nimeifananisha na tabia ya jamaa mmoja wa nchi ya Tanzania alikuwa akilipwa na ACACIA kuitukana Serikali.

Jamaa waliomtuma kuongea yale maneno walimchagulia hata matusi ya kutukana.

Kama ilivyo kawaida mshahara wa dhambi ni mauti jamaa waliokuwa wakimtumia wakamfyatulia mfano wa risasi ili watengeneze taharuki nchini.

Jamaa yule alikuwa akitumwa aitishe serikali kwamba itashitakiwa, jamaa aliingia kichwa kichwa wakamlamba mifano ya risasi.

Jamaa yule alitelekezwa na wadhamini wake.
 
Bado muda kiasi hotuba baadhi za mwalimu pamoja na parade za Mama Maria Nyerere jukwaani zitatamalaki.
 
Hapo umewasema CCM sasa, maana wao ndio wanaohongwa "BUKU 7" za vocha ili wajekuandika JamiiForums yale wanaofundishwa lumumba.

Hao hao CCM wanaofundishwa chakufanya wakifika bungeni pindi "SHERIA KANDAMIZI" na "MIKATABA YA KUNYONYWA" inapotaka kupitishwa kwa "NJIA YA PANYA (HATI YA DHARURA)"

Mungu akubariki mwandishi wa uzi ameizing.
 
Wale wote waliohama vyama na kuachia udiwani/ ubunge bado wakagombea tena na waliposhinda wakapewa nyazifa si ndio hao malaya unaosema!!?
 
Back
Top Bottom