Mwalimu Nyerere kuhusu vijana

Iwaay

Member
May 21, 2016
36
55
Mwl.Julius k.nyerere kuhusu vijana wa Tanzania
…...."Tunataka kuona katika Taifa hili vijana jeuri na wenye kujiamini; si vijana waoga, akina “ndiyo bwana mkubwa". Vijana wenye ujasiri wa kuhoji na kupiga vita mifumo ya jamii isiyoshabihiana na matakwa na matarajio ya jamii ya Kitanzania. Ni kazi bure kwetu, na kwa kweli ni ubatili mtupu, kuwa na Taifa lenye “silaha” za kisasa lakini vijana wake ni waoga."....
Naingiwa na mashaka kama vijana wa Leo tuna sifa hizo
Sifa za vijana wa Leo
-waoga
-Tusiofuatilia mwenendo wa nchi yetu
-wavivu wasiopenda kazi
-walalamikaji pasi na utendaji
-wasio na maamuzi
Mwalimu Nyerere katika umri kama wetu alikua akiwaza namna ya kuutafuta Uhuru wa Tanganyika . Tuamke vijana tuhoji bila woga tunapopaona hapaendi sawa tupambanie maendeleo ya Taifa
Kidemokrasia na kiuchumi tusikubali kukandamizwa wazee hawa waliojaa kwenye maofisi na idara nyeti za serikali ndo wametufikisha hapa
Vijana tubadilike tuamke kwa ajili ya maendeleo yetu na kizazi kinachokuja. Tukumbuke tukikaa kimya leo tutakuna kuulizwa na wajukuu kjpindi tukiwa wazee afu tutajibu nini?. Amkeni tuamke tujenge tanzania yetu.
 
Wazee wako vizuri vijana kina Gwajima wanakula kondoo then wanapiga watu risasi bashite
 
Hakika Mwalimu alinena sasa yana timia.
 
Back
Top Bottom