Mwalimu Nyerere katika harakati na utunzi wa mashairi,historia isiyojulikana na wengi.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,297
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,baba wa Taifa la Tanzania kama anavyojulikana kwa wengi.

Mbali na kuwa mwanasiasa,mwalimu na mpigania uhuru wa Tanzania na Afrika,pia alikuwa ni msanii,mtunzi na mwana taaluma wa ushairi jambo ambalo ni wachache sana hufahamu hilo.

Niliwahi pokea simu siku moja toka kwa mtu ambae hakutaka kutaja Jina lake lakini alikuwa akiniuliza maswali kuhusiana na shairi moja niliwahi andika liitwalo "NGUVU MWISHO WA AKILI" .

Katika mazungumzo na mtu huyo alinambia kwamba "zamani watunzi na waandishi wengi wa mashairi Tanzania walikuwa ni viongozi waandamizi wa serikali"

Nilifikiria sana kauli ya mtu huyo na kuwaza hasa sababu yake ya kuniuliza maswali kuhusu Shairi hilo na mpaka kufikia kunieleza kuhusu viongozi waandamizi wa serikali.

Kuna wakati niliwaza sana kufahamu wanasiasa washairi Tanzania na bahati nimeanza kuwafahamu wachache sana ambao bado nafuatilia kupata japo tungo zao mbili tatu lakini Leo acha niwaletee shairi moja ambalo nimebahatika kulipata mahali likiwa lineandikwa na Baba wa Taifa,Mwalimu Julius K. Nyerere.




Sheikh Kandoro sikia

1.Sheria husaidia
Kuijenga Tanzania
Siyo kazi ya sheria
Nchi kutuharibia.


2.Kila nchi ina nia
Inayoikusudia
Vilevile ina njia
Itakayoipitia.


3.Tanzania tuna nia
Ya kujenga ujamia
Na njia ya kupitia
Ni wote kusaidia.


4.Kijiji chaturadhia
Kisima kujipatia
Lamgambo limelia
Watu wakahudhuria.


5.Wakakubali kwa nia
Kisima kujichimbia
Aliye wakatalia
Kukuye wakamlia.


6.Akaenda kushtakia
Kwa hakimu wa sheria
Kwamba wamemuonea
Kuku wake kumlia.

7.Hakimu akasikia
Akaita jumuia
Wakaja akawambia
Nyinyi mwavunja sheria.

8)Basi nawahukumia
Faini shilingi mia
Na sabini za fidia
Au jela kuingia.

9)Hakimi wakamwambia
Itatushinda fidia
Hata na faini pia
Heri jela kuingia.

10.Wakafungwa kwa sheria
Na maji wakamwachia
Mwenye kuku kuumia
Pamwe na hakimu pia.

11.Huko ni kusaidia
Adui wa jummuia
Nasi kazi za sheria
Ila ya maharamia.

12.Kazi hasa ya sheria
Kusaidia raia
Si nia kuwavunjia
Wanapojisaidia.


Ni moja kati ya mashairi alowahia andika Baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage nyerere.




Idd Ninga
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Shairi zuri kweli kuhusu masuala haya ya sheria.
====
Ila hiyo habari ya mashairi kutungwa na viongozi waandamizi imenistua.
 
Back
Top Bottom