Mwalimu Nyerere hakuwahi kuvaa vazi la CCM 'kijani na njano'?

Ikwanja

JF-Expert Member
Jul 12, 2011
2,082
581
Screenshot from 2015-03-21 10:58:05.png
Rangi za Chama Cha Mapinduzi

Wapendwa wana JF

Imekuwa ni kawaida sasa kwa viongozi wengi wa CCM kuvaa mangu ya kijani na kuonyesha kuwa wao ni wapenzi na Makada wa chama hicho.

Nafahamu kuwa Nyerere ndiye alikianzisha chama hicho enzi za wakulima na wafanyakazi
, sasa naomba kwa yeyote mwenye picha ya Nyerere akiwa katika mangua hayo ailete hapa JF. Maana haya manguo sasa hivi yanatumika kwa wizi na ufisadi tuu, je nyerere aliwahi kuyavaa?

Wote mkikumbuka sawa sawa manguo haya ya kijani yalianza kuvaliwa na Mzee nkapa na ndipo wizi ukaanza na ndipo uzalendo ukaisha, Please please wana JF naomba Picha ya Nyerere akiwa kwenye kijani au njano kama ipo, hii itanisaidia kuendelea na utafiti wangu.


Majibu: Kwanini Nyerere hakuvaa sare za CCM!


KWA karibu wiki nzima iliyopita, wanachama na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamekuwa wakisambaza ujumbe mfupi wa maneno (sms) unaodai kuwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere hakuwahi kabisa kuvaa sare za Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambazo ni suruali nyeusi na shati la rangi ya kijani "kwa sababu alikuwa amekichoka".

Katika hali hiyo, waongo hao pia walidai alikuwa hazitaki sare hizo kwa sababu alikuwa na kinyongo nacho kwa kwenda kinyume cha malengo na misingi yake, hivyo wapiga kura wa mwaka 2015 wanapaswa waking'oe madarakani na kuiweka Chadema ili kumuenzi.

Nadhani nitumie fursa hii ndogo kutoa ufafanuzi wa jumla kwa wote waliotumiwa meseji hiyo ya kijinga,waliosoma thread mbalimbali zilizojadili hilo ama kuulizwa kwa namna yeyote ile.

Wakati Mwalimu Julius Nyerere alipokuwa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM kuanzia Februari 5, 1977 hadi Agosti 16, 1990 alipong'atuka, sare hizo za chama zinazotumika sasa zilikuwa hazijaanza na hata kufikiriwa kwa namna yoyote.

Badala yake, suarali hizo nyeusi na shati hilo la kijani lililoshonwa katika sura inayofanana na kombati hasa za mgambo na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), zilikuwa ni sare tu za Umoja wa Vijana (UVCCM) na chipukizi wake. Halikuwa vazi la TANU wala la CCM.

Sare zinazotumika sasa ambazo ni suruali au sketi nyeusi pamoja na mashati hayo ya kijani zimeanza kutumika wakati tayari ameng'atuka Uenyekiti wa Taifa wa CCM na kubaki tu mwanachama namba moja aliyekuwa na kadi Na. A 1.

Hata aliposhiriki kwenye vikao kama vya Kamati Kuu ya CCM, Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) au Mkutano Mkuu wa Taifa pia hakufanya hivyo akiwa mjumbe isipokuwa mgeni mwalikwa ambaye siyo lazima avae sare.

Katika kipindi chote alipokuwa Rais wa chama kilicholeta Uhuru cha Tanganyika African National Union (TANU) na hata Mwenyekiti wa Taifa wa CCM hadi alipong'atuka, wajumbe wa vikao vya chama walikuwa wakishona sare hususan mashati kutokana na vitenge vilivyobuniwa maalum kwa ajili ya tukio husika.

Mfano ulipofanyika Mkutano Mkuu wa Taifa wa uchaguzi mkuu au pengine NEC, Makao Makuu ya Chama yalikuwa yakitoa kitenge maalum na kuwasambazia wajumbe nchi nzima ili kila mmoja ashone shati lake. Hapakuwa na sare hizi nyeusi wala za kijani kama sasa. Zote zilianza wakati Mwenyekiti wa Taifa wa CCM akiwa Alhaji Ali Hassan Mwinyi baada ya mwaka 1992.

Zilianza baada ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa nchi ya vyama vingi vya siasa tofauti na mwanzo ilipokuwa ya mfumo wa chama kimoja ambacho pia kilitajwa kwamba ni CCM.

Zilibuniwa kwa sababu ya kuwatambulisha wana CCM wanapokuwa kwenye vikao vyao wenyewe, mikutano yao na hata vinginevyo ili kuepuka kuingiliwa kwa namna yoyote ile na mtu asiyehusika na shughuli zao.

Mtu anayesema vinginevyo au kumhusisha Mwalimu kukidhi matakwa yake ya kisiasa kwa kutaka kuwadanganya wapiga kura, kumtumia kwa utapeli au kuwataka wapiga kura waje waiweke madarakani Chadema mwaka 2015 kwa madai kuwa CCM ilishatengwa mpaka na mwasisi wake ni mzandiki na juha wa kisiasa.

Chadema wamekuwa wakihaha na kutafuta namna na mbuni mbalimbali za kuungwa mkono hasa katika kipindi hiki cha mpito kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2015, kwa kueneza uzushi huu wanaamini kuwa itakuwa ndio kujisafishia njia ya kwenda ikulu, jambo ambalo hakika ni mwendawazimu wa kufikiri, labda mtu asiye fikiri sawasawa ndiye anayeweza kurubuniwa kwa njia hiyo.

Mtu anayetaka kujua ukweli akaingie maktaba yoyote yenye picha za vikao vya TANU au vya CCM vya wakati ambao Mwenyekiti wa Taifa alikuwa Mwalimu Julius Nyerere.

Hapo atakuta kwa mfano, wajumbe waliokuwa ni maofisa wa majeshi kama JWTZ, JKT, Jeshi la Polisi au Jeshi la Magereza kwa sababu kilikuwa kipindi cha mfumo wa chama kimoja tu cha siasa utakuta wamevalia sare zao halisi za kijeshi kama ilivyo nchini China, Korea Kaskazini, Vietnam au Kyuba hadi hivi leo.

Wachache kati yao ni pamoja na Jenerali Mirisho Hagai Sarakikya, hayati Jenerali Abdallah Twalipo, Jenerali David Musuguri, hayati Jenerali Mwita Kyaro, hayati Luteni Jenerali Silas Mayunga, hayati Meja Jenerali Mwita Marwa na kadhalika.

Mbali na CCM kutokuwa na sare katika kipindi hicho chote, hata Chadema yenyewe licha ya kuanzishwa na Mzee Edwin Mtei tangu mwaka 1992, lakini ni majuzi tu wakati Mwenyekiti wa Taifa wa sasa, Freeman Mbowe alipokuwa akigombea urais mwaka 2005 ndipo alipokuja na mavazi ya khaki na kutangaza kwamba hatayavua "mpaka kieleweke".

Hakusema kwamba yanakuwa sare za chama hicho lakini ilipofika mwaka 2010 ndipo idadi kubwa ya wanachama wakayafanya kuwa maalum kwa ajili hiyo.

Leo kwa mfano mtu akiuliza kama Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema aliyetangulia kabla ya Mbowe, hayati Bob Makani amewahi kuvaa sare hizo za khaki jibu lake ni "hapana", lakini haimaanishi kwamba alikuwa hakipendi chama hicho isipokuwa vinginevyo.

Mbali na Makani, hakuna pia picha yoyote inayomuonyesha mwasisi wa Chadema, Mzee Edwin Mtei akiongoza kikao chochote cha Kamati Kuu, Baraza Kuu la Taifa, Mkutano Mkuu wa Taifa au pengine akihutubia popote wakati wote alipokuwa Mwenyekiti wa Taifa huku akiwa na kombati hizo za khaki.

Narudia tena kuwa hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere hakuwahi kuvaa sare hizo za CCM zinazotumika sasa siyo kwa sababu alikuwa hakipendi chama chake na kudai hivyo ni ujinga wa kufikiri.
 
Walianza na bendera yao. Baada ya mfumo wa vyama vingi kuanza wakatafuta utambulisho zaidi.
 
Nikweli historia ipo wazi kwamba mwl. hakuwahi kufikiria kuvaa magamba ya njano na kijani,naona kuna mtoa hoja anaye dai kwamba hii imekuja wakati wa vyama vingi kuongeza utambulisho mara baada ya bendera ya chama kimoja,historia inaonesha vyama vingi vilikuwa active sana wakat wa kupigania uhuru na baada ya uhuru,tumeondoa vyama vingi1965 kikatiba kwa sababu za wakati ule,ujio wa 1992 ni urejesho siyo uanzilishi.
 
Kahiyo hawa magamba wanaojipendekeza kwake tuwafanyaje, Maana wao ni magamba na mwalimu hakuwahi kuwa na gamba. inabidi tuwaeleze vizuri wananchi walitambue hilo
 
naunga mkono hoja, siku hizi mtu anatinga kijana ili akapige mingo yake ya ufisadi, ukiwa unasafiri na gari ndogo ukivaa kijani hata polisi hawa kukagui kwny zile check point.
 
naunga mkono hoja, siku hizi mtu anatinga kijana ili akapige mingo yake ya ufisadi, ukiwa unasafiri na gari ndogo ukivaa kijani hata porisi hawa kukagui kwny zile check point.

Kumbe kijani inatumika kama traffic light inapowaka kijani hata gari iliyobeba magendo inaruhusiwa kupita. Ndiyo maana Rage kupanda kwenye jukwaa na silaha akiwa amevaa nguo za kijani, kwa polisi wa magamba siyo 'issue'.
 
hata mie nitafurahi nikiiona picha ya mwalimu kavaa manguo ya rangi ya kisamvu.rangi mbaya machoni .
 
Mkuu umeleta topic nzuri sana maana hawa magamba wanamtumia sana mwalimu kwenye kampeni zao. Sasa Chadema ianze kuwaambia wananchi kuwa CCM ya leo ni ya Mafisadi tu ya nyerere aliondoka nayo mwenyewe alipofariki. Hii imekaa vibaya mno kwao itawapiga vibaya mno mpaka watayakimbia hayo mavazi. Fatilia vizuri kama utakuta mtu aliyevaa haya manguo kama ni mchovu, mengi utakuta yanahemea juujuu tu kama KOMBA wa TOT!
 
Mkuu umeleta topic nzuri sana maana hawa magamba wanamtumia sana mwalimu kwenye kampeni zao. Sasa Chadema ianze kuwaambia wananchi kuwa CCM ya leo ni ya Mafisadi tu ya nyerere aliondoka nayo mwenyewe alipofariki. Hii imekaa vibaya mno kwao itawapiga vibaya mno mpaka watayakimbia hayo mavazi. Fatilia vizuri kama utakuta mtu aliyevaa haya manguo kama ni mchovu, mengi utakuta yanahemea juujuu tu kama KOMBA wa TOT!

Ni kweli kabisa, yaani hayo mangu ni wizi, utapeli, uongo, ujambazi, uzinzi, umbumbu, na yote haya alianzisha Mkapa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom