Mizizi
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 1,275
- 391
Kwa taarifa nilizozipata leo hii kutoka kwa wadau wa Mwalimu nyerere Memorial Academy ni za kusikitisha sana. Cha kusikitisha zaidi ni kwamba, mambo haya yanafanywa na vijana, ambao tulitegemea wangeleta mabadiliko na kusahau ile kasumba iliyokuwa ikishusha hadhi ya baadhi ya vyuo mbali mbali hapa nchini! Kinachotokea Mwalimu Nyerere ni kwamba kuna baadhi ya walimu wamesahau wajibu wao wa kuwasimamia wanafunzi wao ili kufikia malengo yao ya kitaaluma na badala yake wamejigeuza miungu watu.
Haya yametokea hivi karibuni pale wanafunzi wa kada mbalimbali walipohitajika kuandika ripoti zao za tafiti mbalimbali kama utaratibu unavyoeleza. Kinyume na matarajio, baadhi ya wanafunzi hasa wa kike ambao wasimamizi wao ni wanaume vijana kukutana na vikwazo mbalimbali. Wengine walitakiwa kupeleka ripoti hizo nyumbani kwa walimu nyakati za usiku. Waliokataa kufanya hivyo wamefikia hatua mbaya, hata kukataliwa kupokelewa ripoti zao na hivyo kuwepo uwezekano wa kurudia mwaka! Cha kushangaza, ni kwamba, hawa wanaofanya haya wengine wamesoma ndani na nje ya nchi, na wameona ni jinsi gani huko walimu walivyo committed na helpful kwa wanafunzi wao kama wao walivyosaidiwa kwa hali ya juu. Cha ajabu ni kwanini wanaamua kuwafanyia ushenzi kama huu watanzania wenzao.
Kuna mwalimu mmoja baada ya kufanya upumbavu kwa mwanafunzi mke wa mtu, mumewe akaamua kutia timu chuoni, mwalimu alipolazimishwa kuipokea ripoti ya mwanafunzi na mkuu wake akamwambia yule mwanafunzi amwite mumewe wasaishe wote,mwanafunzi alipoambiwa vile akaamua kufikisha malalamiko kwa mkuu wa yule mwalimu, ndipo akabadilishiwa msimamizi, ndipo yule mwalimu wa awali akamfuata huyu mwalimu na kumpa maelekezo kwamba, ahakikishe yule mwanafunzi anarudia mwaka ama yeye anaunja urafiki nae.
Majina ya hawa walimu wote ninayo, na kuna mengi yaliyofanywa hapo chuoni, ikihitajika tutayaweka hapa.
Sasa najiuliza, haya mambo mbona hayafanani na falsafa ya Mwalimu kama chuo kilivyobeba jina lake? Ama ndio hujuma za makusudi kukihujumu chuo hiki kwa malengo maalumu?