Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,265
- 23,198
Dikteta wa Ujerumani enzi hizo, Adolf Hitler, hata angetembea uchi, hakuna mjerumani ambaye angethubutu kumwambia hajavaa nguo na hivyo achutame. Kuthubutu kumkosoa kwa namna yoyote kulitafsiriwa kama kusaini hati ya kuomba hifadhi gerezani na mara nyingi huo ndio ulikuwa mwisho wako wa kuonekana tena.
Kuwa chini ya ulinzi wa GESTAPO kwa sheria iliyojulikana kama sheria ya usiku na ukungu, wengi sana walipotea na hadi leo hawajulikani walipotelea wapi. Dikteta ni adui mkubwa wa utawala unaofuata sheria na kuheshimu katiba na kwetu Watanzania tuna mengi ya kujifunza kutokana na historia ya madikteta duniani.
Madikteta hustawi kwa mbolea ya woga na damu ya wachache wanaothubutu kupaza sauti zao kudai haki, uhuru na usawa bila ubaguzi kwa sababu zozote zile. Ukandamizaji huanza taratibu kwa kusoma alama za nyakati na mwitikio wa wananchi na kama haukupingwa kwa nguvu zote na wananchi hustawi na kukomaa.
"Aliyeonja damu ya mtu haachi," alituasa Hayati Baba wa Taifa na kutuonya kwamba kiu cha wanywa damu hakipungui bali huongezeka baada ya kuonja. Kwa mlevi wa damu mambo ambayo yangefanyika kwa kificho huanza kufanyika mchana kweupe kwani mtu kama huyo hana ubinadamu tena anapotwaa madaraka.
Tunavyozidi kuwakumbatia hawa wanywa damu tutegemee kuwapoteza vijana wetu wanaothubutu kuhoji kulikoni! Je kinachotuongoza ni woga au ujinga?