Mwalimu Nyerere alisisitiza kuwa Kazi ni Uhai, waajiri na Serikali Mtuthamini waajiriwa wenu

RNA

JF-Expert Member
Mar 27, 2013
1,584
2,683
Habari wana JF, Kwa ujumla ukimuajiri mtu mmoja ujue mtu huyo ana mke na watoto, ana ndugu na marafiki wanao mtegemea.

Lakini pia, umlipa mshahara huyo mtu ataenda nunua unga au mchele kwa mtu mwingine ambae amejiajiri ambae inawezekana bila kazi hiyo angeweza kuwa Jambazi mtaani huko mtaani.

Hivyo Basi Kazi ya mtu mmoja inategemea na watu wengi sana katika kufanikisha uhai wao na maisha yao ya kila siku.

Hizi Serikali inatambua kwamba kuna wafanyakazi wananyanyaswa na kifukuzwa bila sababu Maalumu?

Hivi serikali inatambua kuwa kuna wafanyakazi wanakatwa maslahi yao ikiwemo mishahara bila Sababu za Msingi?

Hivi Hawa waajiri wanatambua kuwa Kazi ni Uhai wa wafanyakazi wao kama Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alivyotambua?

Serikali na Waajiri kwa Pamoja mtambue hizi kazi tunazofanya ndio Uhai wetu hivyo kila mmoja kwa Nafasi yake aboreshe huduma kwa waajiriwa.

 
Ndiyo maana ujamaa ulifeli. Nyerere hataki watu wafukuzwe kazi hata kama shirika linapata hasara.
 
Ndiyo maana ujamaa ulifeli. Nyerere hataki watu wafukuzwe kazi hata kama shirika linapata hasara.
Kuna taaratibu za kufukuzwa lakini hali ilivyo mtu anaweza amka tu huko na kufukuza mtu bila sababu ya msingi
 
Utoro ,wizi etc

Hizo chache. Shirika likiwa linaendeshwa kwa hasara linaweza pia kupunguza wafanyakazi (cost cutting). Mashirika ya umma yalipata sana hasara lakini watu hawakufukuzwa kazi mwishowe yakawa mufilisi.
 
Back
Top Bottom