Mwalimu Nyerere aliniambia - Hans Kitine

Kitine mnafiki tu huyo, mfa maji, ye amesahau alimpeleka mkewe ulaya kutibiwa jipu.
Kuona tunda moja bovu sio maana yake kuachana na mti wote mbwiga...."Just because you found one bad apple, doesn't mean you give up on the whole tree".:tape::amen:

Hata kama alimpeleka mkewe kutibiwa jipu sijui chunusi....Alichosema kwenye kongamanao kina MANTIKI au HAPANA?????Ndicho tunachojadili kwa sasa...Mbona Mzee wa Tembo kakiri akiwa Njombe Kwamba Chama Chenu Magamba Kweli kimechafuka wakati mchafuaji mmoja wapo ni yeye!!!!
:A S-confused1:
 
Nyerere alukua hana vision. Alitaka hayo madini yabaki chini ili iweje. Huyu mzee alikua na akili ya kimaskini sana. Angekua anajali vizazi vya badae basi angewajengea mazingira mazuri watoto wake kuliko kuwaacha wanaganga njaa.
 
Kitine anaikosoa serikali kiasi unaweza usihisi kama alikuwa mkuu TISS.
 
Jana UDASA naona habari nyingi zimesemwa lakini hakuna anayetaka kusema alicho kisema Kitine mbele za watu .I also loved him he careless na titles za akina Muhongo maana anaona watu wanalia na Titles wakati Nchi haiko sawa .
Mwalimu Nyerere aliniambia , Hans msije kuruhusu kuchimba maliaasili kwa haraka , maana mtapata laana .Acheni Watanzania wajimbue ndipo wachimbe maliasili yao .Mkiharikisha kuchimba , mtadhurumiwa na mtalaaniwa -Hans Kitine

Sasa mwana JF kama ulifuatilia unasemaje kuhusu kauli yake ? Aliongelea pia rushwa kwa uchungu mkubwa .Na kutoboa kwamba alicho ambiwa na Mwalimu amesha waambiwa wakubwa na watawala nadhani alimaanisha Rais na akaishia kusema na hata wewe Muhongo nilisha kueleza whata Mwalimu said .

Sijaona kokote hauli hii inaongelewa .Je ni kwa bahati mbaya au ndiyo njia ile ile ?

Kitine ni Namba Nyingine na hata TISS Wanamwogopa na Kama Wanabisha Wajitetee humu ndani JF Kwani Wapo Wengi tu. Wenzenu Nchi Zilizo Makini ktk Intelligence Director wa Idara Nyeti Kama hiyo Akisema Jambo basi Litachukuliwa Kwa Tahadhari Kubwa Mno ila Siyo Kwa Bongo. Tupo Nyuma Sana na Wengi Wenu TISS Hans Kitine Amewafundisha Kazi Akiwemo hata Premier Wenu ( Handsome Boy a.ka. Wa Kulialia ).
 
Ingekuwa sio Membe nisingemjua kachero Kitine kwa undani! Achana nae hana issue kwa usafi gani aliokuwa nao ? Tangu atuletee risiti za hospitali ya wanyama kuwa ndio mkewe katibiwa hapo sina hamu naye kabisaa!

Ha ha haaaaa haaaaaaaa!!!! Aisee!!!! Ama kweli hii ni JF burudani mpaka asubuhi.
 
Nyerere alukua hana vision. Alitaka hayo madini yabaki chini ili iweje. Huyu mzee alikua na akili ya kimaskini sana. Angekua anajali vizazi vya badae basi angewajengea mazingira mazuri watoto wake kuliko kuwaacha wanaganga njaa.

LIKE from Isalia
 
Jana UDASA naona habari nyingi zimesemwa lakini hakuna anayetaka kusema alicho kisema Kitine mbele za watu .I also loved him he careless na titles za akina Muhongo maana anaona watu wanalia na Titles wakati Nchi haiko sawa .
Mwalimu Nyerere aliniambia , Hans msije kuruhusu kuchimba maliaasili kwa haraka , maana mtapata laana .Acheni Watanzania wajimbue ndipo wachimbe maliasili yao .Mkiharikisha kuchimba , mtadhurumiwa na mtalaaniwa -Hans Kitine

Sasa mwana JF kama ulifuatilia unasemaje kuhusu kauli yake ? Aliongelea pia rushwa kwa uchungu mkubwa .Na kutoboa kwamba alicho ambiwa na Mwalimu amesha waambiwa wakubwa na watawala nadhani alimaanisha Rais na akaishia kusema na hata wewe Muhongo nilisha kueleza whata Mwalimu said .

Sijaona kokote hauli hii inaongelewa .Je ni kwa bahati mbaya au ndiyo njia ile ile ?


Mkuu Lunyungu heshima mbele habari za masiku.

Huyu mzee Kitine akiongea ni lazima asikilizwe kwa makini maana alikuwa jikoni.

Unajua hawa watu kwa nchi zingine wanakuwa wanakula pesa ya nguvu kutokana na kufanya "after dinner speeches" na mazungumzo tu ya kusaidia semina elekezi, sema tu kwa Tanzania inakuwa ngumu.

Ama kwa hakika huyu Hassy Kitine na wazee wengine kama Augustino Mahiga, mzee Mzena Emilius na hata mzee Siyovelwa ni watu wa kuheshimiwa sana, kwa maana kwamba ni wataalam wa masuala mbalimbali ya kustawisha usalama wa taifa.

Hawa wazee wanafahamu kila kitu, nani anafanya nini nani mla rushwa alieshiba, nani ni FISADI namba moja na ni nani jambazi na kule Ikulu kuna majambazi wangapi.

Kwahio alichokisema kinaweza kuwa hakunuia kumwaga mtama lakini mtama huo umeenda hadi JF, si unafahamu hiyo?

Halafu mkuu, bado huyu boss anakunywa kahawa pale Gymkhana Club au ana sehemu mbalimbali?
 
Kuna maneno kitine pia aliongea " asilimia 99 ya uchumi wa tz unamilikiwa na watu laki moja (kwa milion 45 ni asilimia 0.002) naona wadau iliwapita mnakumbuka mipasho ya prof muongo
 
hivi mtu akishatoka katika serikali ndio anakuwa mshauri mzuri ??? Alifanya jitihada gani akiwa madarakani, na wapo wengine walishika nafasi za juu kuliko huyo na wenyewe sasa ndiyo wanaona wanachokioka. Ukiwa ndani ya serikali unasafiri kwenye gari "tinted" huonekani kama nawe ulikuwemo !! Ukitoka ndiyo tukuone ???????????
 
Kwa mleta mada na wachangiaji baadhi huyu Mzee anaitwa HASSY KITINE na sio HANS Kama wengi mlivyomtaja na kumuelezea. Nawakilisha.
 
Nyerere alukua hana vision. Alitaka hayo madini yabaki chini ili iweje. Huyu mzee alikua na akili ya kimaskini sana. Angekua anajali vizazi vya badae basi angewajengea mazingira mazuri watoto wake kuliko kuwaacha wanaganga njaa.

mtazamo wako unakasoro kubwa., nimaombi yangu kwamba siku moja utagundua nakumuomba radhi mwalimu.

R.I.P Mwalimu
 
Hakuna tatizo lisilo na solution.
Kweli tunalaumu viongozi na watawala wetu, lakini wakati huohuo setup ya mind zetu sisi watu wa kawaida ni kuota kuwa katika position zao ili tuchote kadri iwezekanavyo. Watu wanahaha katika siasa au kugeuza kila kitu kuwa siasa kwa sababu ndiyo njia rahisi ya kujikita katika ukwapuaji wa level ya kitaifa.

Universal law of attraction of mind inasema Kila wazo hugeuka kitendo au kitu halisi mara likomaapo.
Mtanzania wa kawaida kabisa anaota na kujaa matamanio ya siku moja kukaa amhali ambapo atavuta pochi kiaina fulani katika namna ambayo haina jina jingine zaidi ya WIZI.
Kwa hiyo wale walioko madarakani kwa namna moja au nyingine wanatekeleza ndoto, maono au mawazo yetu. Na sisi pia katika ulimwengu wa huo wa ndoto na mawzo tunawaunga mkono kwa kutamani kuwa wao kwa mioyo yetu yote na akili zetu zote. Ndiyo maana WIZI mkubwa ndani ya serikali hauitwi wizi. Neno Mwizi linauhusiano na vibaka wadogo wadogo wanaoibia watu CHENI, pochi, kuku,baiskeli, pikipiki na mahindi au ndizi shambani.
Wizi mkubwa wa Mabilioni Benki kuu au katika idara ya serikali TRA au shirika la umma siku zote hupewa jina tofauti.

Meneja wa Bandari anahusishwa na Upotevu wa Billioni moja.
Mkurugenzi wa ATC asimamishwa kwa matumizi mabaya ya fedha za shirika.
Karani wa TRA aondoka na KITITA cha Millioni mia tisa na kuyoyoma.
Waziri aidhinisha matumizi mabaya ya fedha za serikali
Daraja la UVINZA limekuwa likitengewa fedha kwa miaka 30 lakini kwa muda wote huo limeshindwa kujengwa kwa ukosefu wa fedha.

Lugha za namna hii ni dalili moja kubwa kwamba watu wa kawaida Vyombo vya habari na nchi kwa ujumla inahusudu na kusujudu aina zote za ukengeufu wenye kutushika shati na kaptula ili tusiondoke hapa tulipo.

Kama njaa na siyo HAKI ndo inatufanya tupige kelele tukiahidiwa tonge kelele zinatuishia au zinakatika kabisa.

Tendo la kuiba ndo tukio la mwisho linalo fanywa na mwizi kukamirisha wizi, tukio la kwanza na muhimu katika wizi ni wazo la kujirudia tena na tena akilini la kupanga njama na kuhalalisha kuiba.

Sisi wananchi tulio wengi, tena wasomi na wenye upeo, katikati ya mawzao yetu tumepanga foleni za kusubiri mambo yajipe ili nasi tukaile nchi kwa staili ya iliwavyo sasa au zaidi ya hapo. Ni lini atapatikana kiongozi/viongozi wenye mawazo ya kujenga nchi kutoka miongoni mwetu wananchi??
Wananchi tuna mawazo mabaya sana sana na pengine ya hovyo juu ya nchi yetu utadhani kuna kipande kingine cha ardhi ASIA, ULAYA au MAREKANI walichopewa Watanzania ili Tanzania ikibuma basi waende huko????????????

Lakini pengine tatizo kubwa kuliko yote ni ukweli kwamba ndani kabisa ya mawazo yetu hatujui tunataka nini.

Tunataka kufaidika na maliasili yetu kama taifa??? au tunataka utitiri wa vijibiashara binafsi kwenye mitaa ya Dar isiyo na majina na anuani??
Tunataka nchi inayofikika kila kona kwa barbara na ndege, vyuo safi vya kusomesha watoto wetu au tunataka utajiri binafsi huku tunaishi kwenye jiji linalofurika na kujaa uchafu kila masika??

Fedha zingekuwa MALI Maghaibhu wote wangekaa nazo huko Ughaibhuni, wasingezileta na kuwapa viongozi wetu ili waruhusiwe KUNAJISI nchi kwa zamu. Tulicho nacho kama nchi ndo chenye thamani. Ni sawa na mtoto ambaye ana kubali kubadirishana sahani ya ugali wa mchicha, maharage na utumbo kwa pipi tatu.

Sababu?? Ugali hauna sukari.

Nina watu ninao wafahamu Tanzania TRA,Bandari, Ikulu na Wizarani nyingi za serikali wanao kwapua karibu Millioni 5 kwa siku kwa namna wanayojua wenyewe. Investment zao ni viduka vya Hardware, vijumba vya hapa na pale vya kupanga, Bar Viosk Malori ya mchanga ,Daldala, Teksi bubu na wengine Bodaboda.
Sioni Mtu yeyote katika hawa wenye pochi akiongelea kuwekeza katika viwanda,vya kubadili raw material zetu kuwa finished product.
Hata nati na bolti ni lazima tuagize China??

Wote tumejikita katika kutoa service, good production tumewaachia wenyewe huko ughaibhuni.

Acha madini, rasilimali zote tulizo nazo Tanzania zinatosha kutuondoa hapo tulipo na kutufikisha mahali fulani pa juu vipandio kumi kutoka hapa tulipo.
 
Mkuu Lunyungu, hata kutafsiri kauli nayo inahitaji uwezo fulani!.
Very unfortunately uwezo huo sio wengi wenye nao, na hapa jf ndio kabisa!, usipotafsiri wewe, usitemee kuna watu humu watakuja kutafsiri!.

Haya mambo ya gesi asili wengine tumeyapigia kelele kitambo!, watu wako bize na politiking kila kitu politics hadi kwenye gesi politics!.

Achana na maneno ya Nyerere, tangu tumegundua gesi, japo hatuna sera wala sheria, lakini tumeishatoa mikataba 22 ya PSA yote kwa makampuni ya kigeni!, kwenye mikataba hiyo we get nothing kwa sababu we know nothing!, kama kwenye madini!.

Baada ya kugawa vitalu hivyo, badala ya kusubiri kwanza hivi vilivyopo vizalishe, tujue mapungufu ya zile PSA, tutunge sera madhubuti, tutunge sheria ya gesi na mafuta ndipo tugawe vitalu awamu ya pili, sisi ndio kwanza tunakimbilia kugawa tena vitalu vingine!, kwa jina la Mungu, tunaibiwa!, tena tutaibiwa big time!.

Ugawaji huu ni shinikizo la makampuni fulani naomba nisiyataje due conflict of interest!.
Yalipopata vitalu vya mwanzo, waliomba kutengeneza mitambo ya kusafishia kule kule majini, serikali ikakataa na kuamua mitambo ya kusafishia lazima ijengwe ardhini na wakaingia mkataba wa ujenzi wa bomba la gesi na Wachina chapchap!.

Kitendo cha kuamua kujenga kituo ardhini, kikawafrustrate watatuibiaje?, ndipo wakaja na plan B, wakaomba vitalu vingine deep sea kule karibu na 200 nautical miles kuingia international sea!. Kuichimba gesi huko na kuisafirisha hadi nchikavu itakuwa very expensive ikihusisha under sea pipes!, hivyo serikali yetu itake isitake, lazima itaruhusu mtambo wa kusafishia wa ndani ya bahari ya kina kirefu!. Sasa hapo gesi itachimbwa, mijimeli ya kiharamia itatia dock international waters, watapitisha under sea horse na kudrain gesi wanavyotaka wao, na kujiendea zao hatuna technica know how ku detect, hata Navy wakiiona hiyo mijimeli kwenye radar zao, hatuna any mandate wala jurisdiction kuulizia lolote kuhusu mijimeli hiyo kwa vile imedock international sea!.

Excuse pekee walomdanyanyia Muhongo ni eti Msumbiji nako wamegundua gesi nyingi, tusipowahi kugawa vitalu vyetu, wawekezaji, watakimbilia Msumbiji!. Kina Muhongo badala ya kufanya intelgence ya hilo, wanakimbilia kugawa upya huku wakipokea free bies za facility visits za ulaya na Canada toka kwa intersted companies ili wapate preferential treatments, tena vile vibasha vyatu sisi waandishi ni tripi tuu kupanda ndege, kula vuzuri, kulala vizuri na tujiallowance tudogo!, wenzetu ni mibahasha minene deposited kule Credit Susie!.
Ama kweli, wajinga ndio waliwao!
Kanisome hapa uangalie nililalamika lini!.

sasa na wewe Pasco unamfichia nini George Bush na Barrick yake kwani nduguyo?ngoja nikusaidie tumechoka sisi.haya someni hapa naibeba nzima nzima kwa lugha yake ya asili ya malkia:"As east african states continue to explore for more oil and gas in their respective regions,BARRICK GOLD EAST AFRICA has said that they have invested 2billion U.S.D in Tanzania due to the GREAT POTENTIAL the country has in oil and gas.Speaking to East African Business Week in Dar es salaam last week,the President and Asset General manager for BG East Africa,Mr Derek Hudson said that Tanzania HAS A GREAT OPPORTUNITY and PROSPEROUS in oil and gas than other East African countries due to the AVAILABILITY OF DEEP WATER...ukitaka kumalizia nenda www.africadetails.com/index.php/news/85-oil-gas/320-barrick-gold-invests-u-s-2-billion-in-tanzania-oil-gas
 
Mkuu Lunyungu heshima mbele habari za masiku.

Huyu mzee Kitine akiongea ni lazima asikilizwe kwa makini maana alikuwa jikoni.

Unajua hawa watu kwa nchi zingine wanakuwa wanakula pesa ya nguvu kutokana na kufanya "after dinner speeches" na mazungumzo tu ya kusaidia semina elekezi, sema tu kwa Tanzania inakuwa ngumu.

Ama kwa hakika huyu Hans Kitine na wazee wengine kama Augustino Mahiga, mzee Mzena Emilius na hata mzee Siyovelwa ni watu wa kuheshimiwa sana, kwa maana kwamba ni wataalam wa masuala mbalimbali ya kustawisha usalama wa taifa.

Hawa wazee wnafahamu kila kitu, nani anafanya nini nani mla rushwa alieshiba, nani ni FISADI nammba moja na ni nani jambazi na kule Ikulu kuna majambazi wangapi.

Kwahio alichokisema kinaweza kuwa hakunuia kumwaga mtama lakini mtama huo umeenda hadi JF, si unafahamu hiyo?

Mkuu niko napambana Mkuu wangu .Mambo mengi kaka .
 
Muhongo hasaidii nchi umeme mpaka sasa hivi nikulia lia tu mzigo mkubwa sana kwa wananchi
 
Back
Top Bottom