Mwalimu Nyerere alihusika na siasa za Zanzibar kabla ya Mapinduzi?

Hanga alinyongwa na Karume, kumbuka Hanga hakuwahi kuwamo katika serikali na Muungano, yeye alikuwa Waziri Mkuu wa Zanzibar. Babu ambaye alikuwa waziri wa mipango na uchumi alishtumiwa kuhusika na mauaji ya Karume, hivyo akashikwa na kuwekwa kizuizini hapa Keko. Baaya ya kuonekana hana hatia aliachiwa huru na Nyerere, akaamua kwenda Ulaya; hakuomba ukimbizi kukimkimbia Nyerere kwani tayari alikuwa alikuwa kuzuizini hapa hapa kwa karibu miaka miwili. Nakushauri usisikilize sana porojo za mtaani sana, tafuta ukweli; upo tu.

Ina maana Nyerere alimwuuza au alimchuuza Hanga?
 
Nyerere hakuwa anammmiliki Hanga na wala Hanga hakuwahi kufanya kazi chini ya Nyerere. Uhusiano baina ya Karume na Hanga lilikuwa ni jambo la ndani ya Zanzibar. Ninafahamau historia ya Hanga kukimbilia Guinea, halafu akarudi Dar, na baadaye akarudiswa Zanzibar ambako ndiko mauti yalipomkuta, na watu wa vijiweni wakatafuta sanbabu ya kumnyooshea kidole Nyerere. Lakini kwa vyovyote vile hayo yalikuwa ni mambo ya ndani ya Zanzibar, ambayo mpaka leo yanafanyika. Mpaka leo Zanzibar bado ina mahakama yake!
 
Mkuu asante kwa clarification
Lakini ina maana Nyerere alijua fika Kassim Hanga yatakayomkuta endapo atarudi Unguja
 
Leo tarehe 12 January ni Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, nachukua nafasi hii kuwatakia nyote heri na fanaka za Mapinduzi na kukutakieni maadhimisho mema ya sherehe ya kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa watakao shereheka kwa wale wenye kumbukumbu njema, na kwa vile Mapinduzi Matukufu yale pia yaliandamana na umwagaji damu, natoa pole kwa wenye kumbukumbu chungu.
P
 
Nyerere hakuwa anammmiliki Hanga na wala Hanga hakuwahi kufanya kazi chini ya Nyerere. Uhusiano baina ya Karume na Hanga lilikuwa ni jambo la ndani ya Zanzibar. Ninafahamau historia ya Hanga kukimbilia Guinea, halafu akarudi Dar, na baadaye akarudiswa Zanzibar ambako ndiko mauti yalipomkuta, na watu wa vijiweni wakatafuta sanbabu ya kumnyooshea kidole Nyerere. Lakini kwa vyovyote vile hayo yalikuwa ni mambo ya ndani ya Zanzibar, ambayo mpaka leo yanafanyika. Mpaka leo Zanzibar bado ina mahakama yake!

Huo mstari wako wa mwisho, una maana Kassim Hanga alihukumiwa mahakamani?
 
Mkuu asante kwa clarification
Lakini ina maana Nyerere alijua fika Kassim Hanga yatakayomkuta endapo atarudi Unguja
Nyerere alijuaje? Kwanza Hanga hakurudishwa Zanzibar kwa nguvu; alirudi kwa hiari baada ya majadiliano ambapo alitegemewa kuendelea kuwa Waziri Mkuu wa Zanzibar.

Huo mstari wako wa mwisho, una maana Kassim Hanga alihukumiwa mahakamani?

Hakushitakiwa kwa sababu Karume alijiamulia kuwa jamaa yule anyongwe kinyemelea tu.

Kunyongwa kwa Hanga kinyemela ndiko kulikosabababisha watu kama Abdulrahman Babu na kanali Mahfudhi wahifadhiwea na Nyerere baada ya mauajai ya Karume kwa kuhofia kuwa huenda nao wanenyongwa kinyemela kwa vile tayari walishashukiwa kuhusika na mauaji yale.
 
Nyerere alijuaje? Kwanza Hanga hakurudishwa Zanzibar kwa nguvu; alirudi kwa hiari baada ya majadiliano ambapo alitegemewa kuendelea kuwa Waziri Mkuu wa Zanzibar.

Hakushitakiwa kwa sababu Karume alijiamulia kuwa jamaa yule anyongwe kinyemelea tu.

Kunyongwa kwa Hanga kinyemela ndiko kulikosabababisha watu kama Abdulrahman Babu na kanali Mahfudhi wahifadhiwea na Nyerere baada ya mauajai ya Karume kwa kuhofia kuwa huenda nao wanenyongwa kinyemela kwa vile tayari walishashukiwa kuhusika na mauaji yale.
"Hakurudishwa kwa nguvu" wakati mara ya mwisho kuonekana alikuwa kizuizini.
 
Discussion hii nilishaichoka sasa; watu wa Zanzibar wanaipenda sana. Tukifunga thread moja wanaazisha thread nyingine. Wanapenda sana kumzungumza Nyerere kuliko hata viongozi halisi waliowaletea mapinduzi yale na kuingiza visiwa hivyo kwenye muungano. Sijaona mtu anaandika lolote kuhusu uongozi wa Karume, Babu, Natepe, Okelo, Thabit Kombo, na viongozi wengine wa zanzibar wakati huo. Historia ya Zanzibar yote imekuwa ni ya Nyerere tu.

Mkuu Gaijin:

Kitabu hicho unachosema, tulishakijadili sana hapa, na niliwahi kuleta PDF version yake ya Kiswahili. Ukisaka thread za mwaka 2007 utapata majibu mengi sana.
Wazanzibari lawama zote za matatizo yao ya kisiasa na hata muungano wanamtwisha Nyerere ila wao upande wao wanajitia upofu.

Hii imekuwa mbinu nzuri ya wanasiasa wa huko kupata madaraka kupitia wapiga kura wanaoaminishwa matatizo yanaowakabili chanzo ni Nyerere.
 
Nyerere aliamini ''Binadamu wote ni sawa na Africa ni moja''! narudia tena sijakosea na .....Africa ni moja. so Nyerere alikuwa na haki ya kujihusisha na Siasa zote za Africa ikiwa ni pamoja na Zanzibar.

Akiwa Mwenyekiti wa nchi zilizo mstari wa mbele! ilikuwa lazima afanye hivyo! na alifanikiwa sana, ambayo leo imezaa SADDAC, Tunajivunia!

Wanao leta chokochoko Zanzibar ni Machotara wa kitumwa, wanaodhani waarabu wanawapenda sana kuliko weusi!
 
Back
Top Bottom